Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewasilisha taarifa rasmi kwa Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), kikieleza wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa na haki za binadamu nchini Tanzania kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Mkutano huo ulifanyika Februari 14 hadi 15, 2026 jijini Addis Ababa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia na kuwahusisha Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU), akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Katika taarifa hiyo ya Februari 13 iliyosainiwa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, imeeleza kuwa mazingira ya uchaguzi yalikuwa na ukandamizaji wa upinzani, kufungwa kwa nafasi ya kisiasa, kukamatwa kwa viongozi wa upinzani na kuzuiwa kwa vyombo huru vya habari. Chama hicho pia kimelalamikia kuendelea kushikiliwa kwa Mwenyekiti wake, Tundu Lissu, anayekabiliwa na shtaka la uhaini.
Aidha, CHADEMA kimeitaka AU kushughulikia madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwemo mauaji, kutoweka kwa watu na matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.
Chama hicho kimetoa wito kwa viongozi wa Afrika kuunga mkono uchunguzi huru wa kimataifa na kusisitiza kuwa uhalali wa uongozi unapaswa kutokana na matakwa ya wananchi yaliyoelezwa kwa uhuru na haki.