Barua ya Diamond ! Duh noma!


Mkuu EMT huyo mtu by law hazijui hatakuja kujua hizo Act zenu na section zake.
 
huwezi jua post ya mleta mada ni kweli au uwongo,btw mi hawa wote nawakubali,namkubali Ally kiba na namkubali Diamond pia ubaya ni mashabiki kujigawa,but kinacho-make sense kama inavyosemekana Diamond kurekodiwa wimbo bure kabla hajatoka,na alipotoka akawa against na waliomsaidia,hiyo sijui kama ni kweli au uwongo but mashabiki wa kiba ndo wanahisi kusalitiwa na kumwona kiba alikuwa mwungana kumsaidia Diamond ila Diamond hana shukrani,mi kwa hao wote sina neno,nawakubali.
 

Nilishazungumza nyie wakaanga sumu hamna lolote zaidi ya chuki na wivu kwa mafanikio ya Diamond ndio maana hamumuoni mwingine yoyote....wewe uliyesoma ila unaamini mtu anaweza kukosea mpaka jina lake kutoka Abdul mpaka Abdallah, unatofauti gani na asiyesoma na roho yako ya mbaya ya kiwizadi?? Tafuta maisha yako diamond sio kikwazo kwa vyovyote kwako,alichonacho anakitafuta.
 
Last edited by a moderator:
kweli kabisa hii barua ya kazi au rafiki?
Be seriousl pleaseee
ustake nianze kudharau barua wanafundishwa la sita jamani
mbona wanafunzi mnatutia aibu walimu wenuuu

Tena wanafunzi wanatia aibu hatari tena hawa wa chuo unapokea barua ya maombi mpaka unasikitika unashangaa huyu mtu kasoma degree ama niaje?? Anuani kwenye bahasha iko juu kushoto hata haieleweki nashangaa sana mie nakumbuka kuandika barua nikiwa darasa la tano/sita hivi na form one!two nikajifunza tena sijui ni kitu gani aisee watoto hawa ni hatareee tena ni sheedaaaahh
 
Pumbavu sana..hii barua imeandikwa na ally kiba
 
Mkuu Matumbo, afadhali umenisaidia... unajua muda wote huu nilikuwa najiuliza hiyo Abdallah imetoka wapi... kumbe ndo wanamaanisha hajui hata kuandika Abdul....!!!

Anyway, hii barua kwenye akili yao ambao walikuwa wanafuata tu mkumbo itawadhihirishia kwamba mengi yanayosemwa kuhusu Diamond ni ya kutunga kama ilivyotungwa au kufojiwa hiyo barua! But all in all, hata kama hajui kuandika, who cares? Watu tunataka pini, basi... na hata kama hajui kuandika basi ili mradi anaweza kuandika mashairi na mwenyewe akayaelewa, is more than enough for me coz' i've no plan to hire this dude as my secretary so why should i care??!!

It's very unfortunately tunatumia majina bandia humu... natamani siku moja ingetokea technical error humu ikaumbua watu na their real identities... tungekuja kupigwa na kihoro... hawa hawa wanaojiona kwamba wao ndo wapo juu kumbe wengine ni shoe shines tu mitaa ya posta halafu wanakuja hapa kelele nyingi!
 

Mkuu,

Hawa watu hata siwaelewi, wanamjua Diamond, kuliko anavyowafahamu yy, Alipopanga, anapojenga,hakwenda shule, yaan they know Everything about him, Unajua inamaanisha nini hii?

Inamaanisha Dogo ni Mkali, otherwise wasingemjua kwa Upana huo, lakini pia hawajiulizi wangapi kati yao Jamaa anawafahamu? Wanapoteza Muda kushindana na Mtu asieshindana nao, wanapoteza Muda kumzungumza mtu asie wajua, Wanapoteza Muda kumchukia Mtu asiewachukia, Yaani Ninyi ndio Mnakonda kwa Roho zenu za Kwann.

They act Funny, Msanii ukiwa chini, kila mtu atataka akusaidie, lakini Ukitoka, basi roho zinaanza kuwauma, its Like wanataka always Uwe chini, Usiwe na Hela, wala usisogee...

Jaman, we need to Support Our artists, Correct them when they r wrong, Forgive n keep Up the Love.

Ally Yupo vizuri, Diamond pia tupo vizuri. Tuwape support, Tuache Ushabiki Nazi.
 

Natamani itokee sasa hivi nichekeee...hahahaaaaa ...
Wale wenye sura kama za baba zao sijui wataziweka wapiii....masuper star wa jf...
 
Sio kweli labda kama hao akina Bob Junior walitaka wawe wanapigwa tag maisha yao yote!!! Kabla hili bifu halijaanza, mwenyewe kwa macho na masikio yangu nilimuona Bob Junior akihojiwa ikiwa Diamond alikuwa anamkumbuka baada ya kumtolea ngoma yake Bob Junior yeye mwenyewe kwa mdomo wake akasema mara kibao dogo akipiga show, lazima amkumbuke Bob Junior sasa labda kama walitaka kumgeuza msukule wao!!! Hili bifu halijaanza zamani sana kwahiyo ni uongo mtupu kudai kwamba alipotoka tu jamaa akawapa kisogo akina Bob Junior. Tumia mfano mdogo tu... Bifu la Ally Kiba na Diamond lilikuja wakati wa Track ta Single Boy ya Ally Kiba... kabla ya hapo walikuwa poa tu! Now tell me, Single Girl imetoka lini na Diamond ametoka lini ndipo utafahamu kwamba hayo maneno ni ya uongo!!

Kuhusu mashabiki kugawanyika, hilo ni jambo la kawaida sana na halizuiliki! Kinachogomba watu ni kufanya fitina kwa mtu ili ashuke na apande wanayemtaka! Yaani kwenye muziki zinaingizwa fitina za kisiasa kama hizo za kufoji barua na kusema ni ya Diamond... mtu unajiuliza, barua ya kwenda JWTZ imefikaje mitandaoni!

Ila ngoja nikuambie jambo moja... unless kama kweli Clouds wanahusika (binafsi siamini hata kidogo) otherwise hakuna mwenye uwezo wa kumshusha Diamond... si kwamba ni mkali sana bali anaongozwa na watu wanaofahamu fitina za muziki wa kibongo! I hate to say this, but trust me, Saidi Fella na Babu Tale ni watu wanaozifahamu fitina za muziki wa bongo kuliko mtu mwingine yoyote yule! Tell me, where's Juma Nature? Ali-mess na Said Fella, na mwisho wake ukawa ndo hapo! Where's the whole stuff called Wanaume Halisi? I know these guys, been wit them in those old days! Wanaume Family chini ya Fella walipigwa sana makopo kwenye ushindani kati yao na wanaume Halisi! Who's the winner hapa tunapoongea? Hawa wapiga kelele kwenye mitandao na majukwaani wala hawana ubavu wa kumsaidia Kiba, kelele zao zitaishia humu humu kama ambavyo kelele zao hazikusaidia kuinusuru Wanaume Halisi...
 
Natamani itokee sasa hivi nichekeee...hahahaaaaa ...
Wale wenye sura kama za baba zao sijui wataziweka wapiii....masuper star wa jf...
Umeona enh... maana humu kuna watu wanajua kutishia wenzao bhana..., aaaaargh, kumbe wapi!
 

Acha kuita Watanzania wajinga wewe ona haya sema baadhi unafikiri ni wote wanafuatilia mziki futa hiyo kauli yako mi kuna watu nawafahamu hawafuatiliagi mzigi acha kujumlisha wote sema baadhi
 
Hahaaahaa eti jeshi la kujenga taifa alafu kwenye mabano JWTZ
Kweli Diamond ni watandale kweli yaani ujanja wote ule amechapia hadi jina la jeshi letu!!!!
 
Natamani itokee sasa hivi nichekeee...hahahaaaaa ...
Wale wenye sura kama za baba zao sijui wataziweka wapiii....masuper star wa jf...

Kama memeeeeeeeeeeew(wema's voice)
 
Acha kuita Watanzania wajinga wewe ona haya sema baadhi unafikiri ni wote wanafuatilia mziki futa hiyo kauli yako mi kuna watu nawafahamu hawafuatiliagi mzigi acha kujumlisha wote sema baadhi
Simple Rule of Thumb... ukiona comment haikuhusu, unaipotezea! Kwahiyo kama unadhani nawe si mmoja wa hao wajinga, ulitakiwa kuipotezea!!
 
Hhhhhhaaaaaaaa CC brenda18

Hahahahahahah...dina mi sitakiiii...cc:mtu fudenge asije akaturukia hapa...watu mafamous humu hatariiiiii....bora mie mnywa uji tu ata mkiniona kidomo changu kimepinda hakuna shidaaaa.... Dinazarde awards za jf jaman zinatolewa wapi mie niendee
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…