Barua ya Loan Board Kuna aliyepata?

mmh baba hela ya ghafla ina uzalendo kweli?leo hii kila ct ina budget ndo ghafla uambiwe laki inakatwa..itatoka wapi nawe ubakiwe na ngapi?lazima mshtuko utokee

pole sana kwa mshutuko! sie tupo na biashara zetu za genge, tunauza nyanya, dagaa, samaki nk nk! sie hatuelewi loan board, sie tunalewa vicoba hata saccos tumeshasahau sasa hv! unajua nchi yetu ya matukio, msimu uliopita saccos ilibamba, msimu huu vicoba inatubamba, sie tunakuaga na ile inayobamba!
 
Najua na ndo maana sibishi kulipa,nachopingana nacho ni hizo terms,na how wanibane kwenye % ya kulipa?while kuna wanaolipa elfu 10 tu kwa mwezi...sisi laki how?

mkuu unajali nini so ndoutamaliza haraka deni hilo, mimi nilishapigwa penati mda mrefu na wamekata mwaka sasa nimezoea!
 
hakuna kuandika barua kupinga amount hiyo?

Kutokana na maelezo yako ya awali wewe mwenyewe huijui amount unayodaiwa - sasa utaandika kupinga kiasi walichotaja wao kwa kigezo gani? Labda badala ya kuandika kupinga uandike kutaka maelezo ya kiasi unachodaiwa. - au ikiwezekana uende kabisa ofisini kwao.
 
lipa tu kaka,na wengine wote lipeni.....hizo loan ni mlizochukua ndio mmewekeza kwenye elimu iliyowafikisha hapo mlipo....haina tofauti na mfanyabiashara anapokopa kuwekeza....wengine hatukupata loan tumelipa wenyewe ni ngumu sana...shukuruni mlipata loan na muonyeshe shukrani kwa kulipa....
 
thanks na maelezo niliyoyapata pia ni haya kwamba niandike barua ya kuomba clarification..nimeshaiandika iko kwa HR nw
 
mkuu unajali nini so ndoutamaliza haraka deni hilo, mimi nilishapigwa penati mda mrefu na wamekata mwaka sasa nimezoea!

du bora deni la benk unajicomit kwa kuwa tayari na amount utakayokatwa so unakuwa hata kimaisha umeshajitune..nakopa hii nitakatwa hii
 
Hawa jamaa Bunge la bajeti likifika tu ndio wanaamka!

si unajua tena tanzania mambo huendeshwa kwa kufuata upepo!!matokeo form4 yaliyosiasishwa yatatoka kabla ya bajeti ya wizara ya elimu ili wabunge wasihoji
 
Mtu yeyote anayebisha au kukwepa kulipa mkopo,huyo ni msaliti. Mimi nilisoma miaka ya zamani lakini kwa sasa ninavojua ukilipa mkopo unampa nafasi mtoto wa maskini mwingine kupewa hizo pesa ambazo utakuwa umerudisha. Jamani hakuna haja ya kuwasema na kuwatukana mafisadi kama sisi wenyewe hatuoni kuwa kutorudisha mikopo tulokopeshwa ni ufisadi na usaliti. Tunawanyima nafasi maskini wengine kusaidiwa kupata elimu ya juu. KOPA MKOPO,LIPA DENI.
 
Duuuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…