Barua ya marehemu mama kwa mwanae - siku tatu baada ya kuzikwa

Barua ya marehemu mama kwa mwanae - siku tatu baada ya kuzikwa

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
BARUA YA MAREHEMU MAMA KWA MWANAE - SIKU TATU BAADA YA KUZIKWA!!!
1735499451143.jpg
Mwanangu Mpendwa,

Nataka ujue kwamba nilikufa kama mwanamke masikini wakati nina Mtoto kama wewe.

Mwanangu, nilitaka kukubariki kabla sijafa, lakini sasa nimeenda na baraka zangu.

Chai ya asubuhi, chakula cha mchana na chakula cha jioni ilikuwa moja ya changamoto zangu nilipokuwa hai, lakini ulitumia pesa kupika vyakula vya kila aina, nyama na aina mbalimbali za vinywaji siku ya mazishi yangu.

Mwanangu, uliipaka maiti yangu kwa kila aina ya manukato ya gharama wakati nilipokuwa hai nilitumia mafuta ya kupikia kama mafuta yangu ya kujipaka kwenye mwili wangu

Ulivisha Maiti yangu kitambaa cha gharama wakati ilikuwa vigumu kuninunulia kanga.
Maiti yangu ilipokuwa Chumba cha Maiti ulikuja kuniangalia mara kwa mara, unajali Maiti yangu kuliko nilipokuwa hai kwanini?

Jambo chungu zaidi ni aina ya jeneza la gharama uliloweka Maiti yangu wakati niliishi kwenye nyumba ambayo haijakamilika nikiwa hai na nilikuwa nikilalia godoro lililochakaa sana

Ulipokuwa mdogo nilikuwa nikishinda na njaa ili upate kula na kushiba, nilikuwa nikivaa kanga moja ili kukupatia nguo za kutosha. Nilidhani utanitunza nikizeeka.

Ulimaliza nyumba, ukaipaka rangi na ukasafisha kiwanja ndani ya wiki moja ili tu kusherehekea Maiti yangu.
Na ukaandika kwa heshima ukisema "Mama, nakupenda sana pumzika kwa amani" - wakati nimekufa kwa moyo uliovunjika.

Hatimaye, mwanangu, niliandika haya kukukumbusha kwamba hakuna mtu mwingine anayependa mtoto kama mama.

Mungu Akusamehe, Nakupenda sana Mwanangu

Ikiwa Unampenda Mama yako, Tafadhali Usipite Bila kuandika Nakupenda Mama ❤️❤️❤️
 
Siku hizi kuna vikundi vingi vya makazini , mtaani nk vya kuchangiana kwenye msiba. Yaani mtu wako akifariki ndio unapewa hela sio mtu wako akiumwa au akiwa hana hela ya kula.

Kwahiyo mtu anaweza asiwe na hela ya kujenga kwao au kuuguza lakini msiba ukitokea akafanya kila kitu kwa sababu vile vikundi vinakuwa vimempa hela sasa kwa ajili ya msiba.

Watu wasioelewa ndio wataanza lawama “mbona anatoa hela ya kupika msibani, mara Jeneza la gharama mara nini sijui na wakati mama yake aliumwa au aliteseka njaa hakumsaidia kumbe ana hela” hawajui huo msiba ndio umeleta hela.

Mungu atusaidie.
 
Back
Top Bottom