Barua ya ole kwa mhe. Ole Sendeka

Barua ya ole kwa mhe. Ole Sendeka

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Posts
2,638
Reaction score
1,218
Kwako Mbunge wa Simanjiro.

Nakusalimu sana kwa Jina la Yesu Kristu na Mwokozi wetu.
Nimeamua kukuandikia ukiwa hapo Dodoma kwenye Bunge la Katiba baada ya kusikia habari za kusikitisha na kuudhi kuhusu kilio chako cha kutaka KURA YA WAZI.

Mhe. Sendeka, nilitamani sana kufika hapo Dodoma ili nionane na wewe uso kwa uso ili uweze kunijibu maswali yangu yafuatayo kutokana na kilio chako cha kulilia kura ya WAZI. Maswali yenyewe ni haya yafuatayo na nitaomba unijibu kwa kupitia mtandao huu wa JF.
  1. Tunajua mtu mzima tena MWANAMME kulia kwa jambo hasa lisilohusiana na msiba ni UCHURO. Maana yake ni kuashiria msiba au huzuni iliyoko mbele yako au wanajamii waliokuzunguka. Naomba uwaambia Watanzania ni nini hasa kilichokuliza?
  2. Katika Chaguzi zote za Ubunge ulizowahi kugombea kama sikosei ni zaidi ya mara 3 umewahi kuchaguliwa kwa kupigwa KURA YA WAZI??
  3. Je,wewe kama Ole Sendeka na Mtanzania mwenye kuipenda nchi hii utanufaika vipi na KURA YA WAZI kama itakubalika kama ulivoililia kwenye kikao chenu cha SIRI???
  4. Tumesikia umenukuliwa na vyombo vya habari kuwa KURA YA SIRI itakizamisha chama chako cha CCM. Je, uweza kunipa sababu 5 kuu za kuifanya CCM izame kwa kutumia KURA YA SIRI?
  5. Chaguzi zote za Rais, Wabunge, Madiwani na hata hao viongozi wa CCM huchaguliwa kwa kura za siri. Iweje leo kwenye Bunge la Katiba kura ya SIRI iwe dhambi???

Nimalize kwa kusema kwamba kama wewe ni Mkristu na muumini mzuri hebu jaribu kusoma BIBLIA na uone neno OLE lilivotumia kwenye Biblia na maana yake. Ole ni neno linaloashilia hatari,anguko na kiyama kwa wanadamu. Biblia imeandika vifungu kadhaa vyenye OLE WAO, OLE WAKE ANAYEFANYA JAMBO FULANI LISILOFAA MBELE ZA MUNGU.

Mhe.Ole Sendeka nami nakumabia: Ole wako kwa KUNG'ANG'ANIA NA KULILIA KURA YA WAZI kwa sababu tu ya MASLAHI YA CCM. Ole wako!!!!!!
 
Ni kweli kabisa. Hilo nalo litaandikwa na litakumbukwa, kama kweli una mapenzi ya dhati na watanzania hawa wa sasa na wajao waambie hawa wanaokuona sasa kwa nini ulilia kwa ajili yao kwa kura ya Wazi, Mungu tayari anaijua nafsi yako hahitaji maelezo, waambie tu Watanzania wanaokuona hivi sasa.
 
Back
Top Bottom