Barua ya TFF kuomba miaka 12 ya uongozi BMT yanaswa, Karia na genge lake wakumbuka shuka kumeshakucha

Mwanongwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2023
Posts
879
Reaction score
814
Ni kama mtu anayejifunza kuogelea siku meli inazama. Too late!!!

Imebainika kuwa uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulianza kushinikiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kubadilisha Sera ya Michezo ya Taifa kuongeza ukomo wa madaraka ya uongozi wakati tayari Katiba yao imebadilishwa kinyume na Sera ya Maendeleo ya Michezo na Sheria ya BMT.

Katika barua yake kwa BMT Kumb Na AC 246/301/09A/101/90 ya tarehe 23 Januari mwaka 2024, iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, Shirikisho hilo liliomba Baraza la Michezo la Taifa (BMT) libadilishe Sera ya Maendeleo ya Michezo ya Taifa kwa kuongeza ukomo wa madaraka wa viongozi uwe miaka 12 kutoka miaka 9 iliyopo sasa.

Taarifa kutoka ndani ya TFF inaeleza kuwa mabadiliko ya Katiba ya TFF ya mwaka 2019 yaliyokubaliwa na Msajili wa Vyama vya Michezo mwaka 2020 yalifanyika kwa shinikizo kutoka mmoja wa viongozi wa juu serikalini aliyekuwa anaubeba uongozi wa Karia.

"Msajili aligoma kupitisha Katiba kwa kuwa ilikuwa kinyume cha Sera ya Michezo lakini yakaja maelekezo kutoja juu kwamba ipitishwe hivyo hivyo"

"Walipopitisha waka relax, sasa walipoona uchaguzi wa mwaka huu unakaribia, wakahisi ile Katiba yao inaweza kuwaletea shida, wakaanza kushinikiza mabadiliko ya Sera yaendane na Katiba yao", kilieleza chanzo.

Kwa mujibu taarifa kutoka ndani ya TFF, Rais Karia aliona hatari ya uchaguzi wa mwaka huu 2025, akaanza jitihada na kuweka msukumo BMT wabadilishe Sera ya Michezo na Sheria ya BMT inayohitaji ukomo wa madaraka wa miaka 9.

Katika barua ya TFF ambayo nakala yake imenaswa, TFF waliomba kubadilisha tamko namba 5.2 3 la Sera ya Michezo ya Taifa na kuweka vipindi vitatu vya miaka minne jumla miaka 12 badala ya vipindi vitatu vya miaka 9.

"Inaonekana walishapima na kuiona hatari iliyopo mbele wakaanza kupambana lakini inavyoonekana hawajafanikiwa kwa sababu Sera haijabadilika."

"Wangefanikiwa kubadilisha pengine wangekua salama lakini kwa sasa tabu ipo pale pale"

Kwa mujibu wa barua hiyo inaonekana kulikuwa na vikao vingi kati ya TFF na BMT kujaribu kubadili Sera na Sheria lakini havikuzaa matunda.

"Ukiangalia barua hiyo utaona imerejea vikao kadhaa ambavyo viliwahi kufanyika kati ya TFF na BMT" kilisema chanzo cha taarifa hiyo.

"Cha kushangaza ni kuwa TFF inaliagiza Baraza la Michezo la Taifa kufanya mabadiliko ya Sera na Sheria eti kwa sababu tayari Katiba ya TFF imeshaweka ukomo wa miaka 12 (4:4:4). Hapa kuna udhaifu mkubwa sana wa uelewa. Hii ni sababu ya kijinga".

"Ukiiangalia na kuisoma hiyo barua between the lines utaona walichofanya TFF ni kukiri kwamba walifanya mabadiliko ya Katiba yao kinyume cha Sera ya Maendeleo ya Michezo na Sheria ya BMT na wamefanya hivyo huku wakijua wanafanya makosa." kilisema chanzo hicho.

"BMT inasimamia vyama vya michezo yote, kama kila chama kitakuja na maagizo ya namna hiyo BMT itayumba. Ingawa bado haijajulikana BMT walijibu nini lakini the fact kwamba Sera na Sheria hazijawahi kubadilika tangu 1995 ni dhahiri kwamba BMT walikataa huo ujinga wa kupokea maelekezo ya kunufaisha kikundi cha watu wanaotamani kukalia madaraka kwa muda mrefu kinyume na Sheria", chanzo kilisema.

Katika barua hiyo TFF walidai kwamba kwa kuwa maelekezo ya mashirikisho ya kimataifa (bila kutaja hayo mashirikisho) ni kuweka ukomo wa madaraka wa miaka 12, wanaomba BMT ifanye mabadiliko ya Sera katika tamko namba 5.2.3 linaloweka ukomo wa madaraka wa miaka 9.

Sehemu ya barua hiyo inasomeka kama ifuatavyo, "Kwa kuzingatia mwongozo wa mashirikisho ya Kimataifa, na kutoa muda wa kutosha kwa uongozi unaochaguliwa kutekeleza mipango yake, na kwa vile tayari vipindi vya uongozi kwa TFF ni vitatu vya miaka minne minne, tunaomba Mheshimiwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo aondoe (waive) zuio hilo la Sera ili wanachama wa TFF (mikoa na vyama shiriki) na wanachama wao (wilaya) nao warekebishe Katiba zao kwa kuwa na vipindi vitatu vya uongozi vya miaka minne minne."

Ukiangalia tone ya barua hiyo ni kama vile Katibu wa TFF alikuwa anaamini mabadiliko ambayo yalishafanyika kwenye Katiba ya TFF yalishapata uhalali kwa sababu tu yalipitishwa na Msajili.

"Ambacho Katibu Mkuu wa TFF hajui ni kwamba hata kama Katiba ilipitishwa na Msajili, kama kuna Ibara inakinzana na Sheria za nchi, Ibara hiyo automatically inakuwa batili kwa sababu sheria ya nchi ina supercede Katiba za vyama vya michezo", alisema.

Wakati ambapo mchakato wa Urais wa TFF unaendelea, tayari wanasheria watano wanapinga mchakato huo wakidai muhula wa tatu kwa Rais Karia ni batili kwa kuwa Katiba ya TFF imekiuka Sheria ya nchi.

Wanasheria hao wamesema watalifikisha suala hilo mahakamani kama Baraza la Michezo la Taifa halitachukua hatua sahihi.

Katika mchakato wa Uchaguzi, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imempitisha Karia kama mgombea pekee na kuwachuja wagombea wengine wanne kwa kukosa udhamini.

Wagombea hao wamekosa udhamini baada ya Karia kukomba wadhamini 46 kati ya 47 waliopo. Katiba inahitaji kila mgombea Urais adhaminiwe na wadhamini wasiopungua watano.
 

Attachments

  • IMG-20250715-WA0095.jpg
    58.5 KB · Views: 34
Karia alishawai kumuita Michael Wambura kuwa ni Tundu Lisu wa kwenye tasinia ya soccer, kisa Michael Wambura alijitosa kwenye kinyang'anyiro cha urais wa tff kitu ambacho Karia hakukipenda.
 
Yule wakili wa TFF anayetaka alipwe bilioni 2 za kuchafuliwa, (character assassination), anaitwa nani vile?
 
Wahuni walijipanga kuwepo , mpaka Yesu au Mtume arud
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…