Barua ya wafanyabiashara mkoa wa Arusha dhidi ya Mtumishi wa TRA anayekula rushwa wazi

Barua ya wafanyabiashara mkoa wa Arusha dhidi ya Mtumishi wa TRA anayekula rushwa wazi

Mwan mpambanaji

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2008
Posts
482
Reaction score
131
Wanabodi salaam

Hii ni barua ya wafanyabiashara mkoa wa Arusha wakilalamika bwana mmoja, huyu jamaa bado yupo enzi zile za pontio plato za kutishia watu ili ajipatie fedha, anakufanyia upepelezi feki ili iwe rahisi kukufanya utoe fedha

Taarifa za uhakika huyu bwana ana ukwasi mkubwa na amejenga shule moja huko Moshono/Mwanama inaitwa Luomo school.

Mbaya zaidi amefanya kazi kituo kimoja kwa miaka 15, ni wazi kuna wakubwa ambao wananufaika na huyu bwana.

Tunaomba Mamlaka ichukue hatua za kisheria dhidi yake!

Wafanyabiashara tunaomba huruma ya Mh Rais Samia Suluhu

===

WAFANYABIASHARA/ARUSHA
13.5.2021.​

ATT: ALPHAYO J. KIDATA
KAMISHNA MKUU
MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA
S.L.P 11491
DAR ES SALAAM.

YAH:MALALAMIKO DHIDI YA MTUMISHI WA TRA/ARUSHA BW. LOSHIE LAIZER.

Somo hilo hapo juu lahusika.

Sisi wafanyabiashara wakubwa katika Mkoa wa Arusha tunapenda kuchukua fursa hii kukupongeza kwa moyo wa dhati kwa kuteuliwa kwako na tena na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mheshimiwa SAMIA SULUHU HASSAN kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Tunaamini kuwa uteuzi huu uliofanywa na Mheshimiwa Rais Wetu mpendwa uunaoonyesha imani kubwa juu yako kuwa utarekebisha na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wanaounda kundi linaloongoza katika ukusanyaji wa mapato ya nchini.

Kwa msingi huo tunaamini kwamba utasikiliza malalamiko na kilio chetu kuhusu baadhi ya watumishi ndani ya Mamlaka (TRA) ambao wamekuwa mwiba kwa wafanyabiashara kwa kubambikizia makadirio makubwa ya kodi yasiyozingatia sheria za nchi hivyo kutengeneza mianya ya kupokea rushwa kutoka kwa wafanyabiashara.

Mheshimiwa Kamishna,

Tunaomba kuchukua nafasi kuwasilisha kwako malalamiko yetu kuhusu mtumishi wa TRA Arusha Bw.Loshie Laizer wa kitengo cha uchunguzi/upelelezi kuwa amekuwa na tabia ya kuwanyanyasa wafanyabiashara hasa wakubwa kwa kubambikia makadirio ya malimbikizo ya kodi baada “kuchungulia” akaunti zao binafsi katika mabenki na pia akaunti za biashara wanazomiliki.

Mtumishi huyo amekuwa akitumia njia za vitisho dhidi ya wafanyabiashara kuwa endapo hata kubaliana na matokeo ya uchunguzi “feki” kuwa anadaiwa malimbikizo makubwa ya kodi basi ataagiza mamlaka nyingine za kiserikali kumfungulia mfanyabiashara husika kesi ya uhujumu uchumi au ya utakasishaji fedha (ML).

Kutokana na vitisho hivyo wafanyabiashara wengi wameingia katika mtego wa mtumishi huyo wa kutoa chochote (rushwa) ili kuepuka usumbufu na pia kuogopa kufunguliwa kesi hasa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Mheshimiwa Kamishna,
Taarifa zinaonyesha kuwa mtumishi huyo amekuwa akifanya kazi katika eneo moja (Mkoa wa Arusha) kwa zaidi ya miaka 15 jambao ambalo si la kawaida kwa watumishi umma hivyo kuzua maswali yasiyo na majibu kwa wadau na wafanyabiashara.Kuna madai kuwa kila mamlaka ilipojaribu kumhamisha mtumishi huyo alitumia njia mbalimbali kuzuia umahisho huo.

Kuna madai kuwa mtumishi huyo ana ukwasi mkubwa kwa kumiliki mali kadhaa kama nyummba za kupanga mashamba na hisa katika baadhi ya biashara kubwa mjini Arusha ikiwemo shule ya LOAMO iliyopo eneo la Olorien katika Jiji la Arusha ambayo ni moja katika ya shule kubwa mjini Arusha.

Mheshimiwa Kamishna tunaomba uchunguzi huru na wa haki ufanyike dhidi ya mtumishi huyo ili kuwaondoelea adha,manyanyaso, na hofu wanayopata wafanyabiashara wa Mkoa wa Arusha na tunaamini kuwa kilio chetu kitafanyiwa kazi.

Tunatangauliza shukrani zetu.
Omar SS.
Kwa niaba ya wafanyabiashara
Arusha.
 
Attachments

Kodi inakusanywa kwa maelewano,nakushauri usome barua uelewe msingi wa malalamiko
Barua imekaa kimajungu tu cjaona ishu yoyote aliyofanya, labda mnashindwa kuelewa Tanzania ina rate kubwa sana za kodi.corporate 30percent,Vat 18,withholding 10 au 15, na makodi mengine kibao.wafanyabiashara mnashindwa kuelewa mchawi wenu ni sheria kandamizi za kodi na sio wakusanya kodi.
 
Ukiona wafanyabiashara wanaelewana na wakusanya kodi mjue kama taifa mnapigwa.
Inawezekana ni kweli na inawezekana sio kweli. TRA kuna watu wanaofanya kazi kama wako kwenye vihamba vyao. Wanatumia ujanja ujanja kusumbua watu ili wapate rushwa.

Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..wapo wema. Ila kuna watu wengi tu hawastahili kufanya kazi ndani ya institution ile. Ni very corrupt.
 
Awamu ya Mama Samia ukiwa mtumishi wa umma ujue muda wowote wananchi wanachoma kibanda, wakikuweka kwenye kikaango tu ujue umeumia.

Watumishi wa umma badilikeni na msifikiri mpo juu ya sheria, hii sio awamu ya Chief Magufuli aliekua na DOUBLE STANDARD kwenye kutumbua.
 
Barua imekaa kimajungu tu cjaona ishu yoyote aliyofanya,labda mnashindwa kuelewa Tanzania ina rate kubwa sana za kodi.corporate 30percent,Vat 18,withholding 10 au 15,na makodi mengine kibao.wafanyabiashara mnashindwa kuelewa mchawi wenu ni sheria kandamizi za kodi na sio wakusanya kodi.
Basi ziwekwe vizuri ili watu wapate kulalamika vyema. Lakini mbona ni yeye tu na si wengine?

Nawaza tu.
 
Awamu ya Mama Samia ukiwa mtumishi wa umma ujue muda wowote wananchi wanachoma kibanda, wakikuweka kwenye kikaango tu ujue umeumia.

Watumishi wa umma badilikeni na msifikiri mpo juu ya sheria, hii sio awamu ya Chief Magufuli aliekua na DOUBLE STANDARD kwenye kutumbua.
Acha uongo wewe! Subiri matokeo ya tume inayochunguza BOT, maana bado ipo kwenye upembuzi,
 
Barua imekaa kimajungu tu cjaona ishu yoyote aliyofanya,labda mnashindwa kuelewa Tanzania ina rate kubwa sana za kodi.corporate 30percent,Vat 18,withholding 10 au 15,na makodi mengine kibao.wafanyabiashara mnashindwa kuelewa mchawi wenu ni sheria kandamizi za kodi na sio wakusanya kodi.
Africa kodi ni tools ya kuwafanya watu wawe masikini ili watawaliwe
 
Awamu ya Mama Samia ukiwa mtumishi wa umma ujue muda wowote wananchi wanachoma kibanda, wakikuweka kwenye kikaango tu ujue umeumia.

Watumishi wa umma badilikeni na msifikiri mpo juu ya sheria, hii sio awamu ya Chief Magufuli aliekua na DOUBLE STANDARD kwenye kutumbua.
Mbona wezi wa mwendazake kawalinda kawapa teuzi wengine.ccm wote ni walewale
 
Barua imekaa kimajungu tu cjaona ishu yoyote aliyofanya,labda mnashindwa kuelewa Tanzania ina rate kubwa sana za kodi.corporate 30percent,Vat 18,withholding 10 au 15,na makodi mengine kibao.wafanyabiashara mnashindwa kuelewa mchawi wenu ni sheria kandamizi za kodi na sio wakusanya kodi.
Mchawi ni huo utitiri wa kodi, Tanzania inatambulika ulimwenguni, kwa kodi nyingi zinazojirudia na kandamizi.
Bunge ndilo hilo!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Back
Top Bottom