Barua ya Wazi kwa Baba Mtakatifu Papa Leo XIV (Kwa Kiswahili)

​

Baba Mtakatifu,
Ninaandika kwa dharura kutoka Tanzania, nchi ambayo historia yake imesimama kama mfano wa kuvutia wa mshikamano wa kidini. Zaidi ya miongo sita, Wakristo na Waislamu wameishi kama ndugu, wakiwa si tu watu wa imani bali Watanzania. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwanzilishi wa Taifa letu na mkatoliki mwaminifu, ndiye aliyepanda mbegu za uvumilivu huu. Aliongoza si kama Rais wa Kikatoliki, bali kama Rais wa Watanzania wote, na imani yake ilimfundisha kuheshimu wote.

Baada yake, Ali Hassan Mwinyi, Mwislamu, aliongoza taifa na amani iliendelea. Kisha Benjamin William Mkapa, Mkristo Katoliki, naye akafuatiwa na Jakaya Mrisho Kikwete, Mwislamu. Baadaye John Pombe Magufuli, tena Mkatoliki. Na sasa kwa mara ya kwanza tunao Rais mwanamke Mwislamu, Dk. Samia Suluhu Hassan. Kupitia mizunguko hii yote, Tanzania ilibaki kuwa kielelezo cha taifa linaloweza kubadilisha marais wa dini tofauti bila migawanyiko ya kidini.

Baba Mtakatifu, leo urithi huu unavunjwa — na si na magaidi kutoka nje, bali na Kanisa lenyewe kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Badala ya mimbari kuwa mahali pa wokovu, zimegeuzwa majukwaa ya kisiasa. Jumapili baada ya Jumapili, mahubiri hayazungumzii tena Injili, bali yanashambulia serikali. Hayatamki tena upendo wa Kristo, bali “udhaifu” wa Rais Samia. Wamekwenda mbali hadi kudai kuwa hafai kuongoza, hastahili muhula wa pili, na hawezi kuendesha taifa. Meza ya Ekaristi imegeuzwa kuwa madhabahu ya upinzani.

Kati ya sauti kali zaidi ni ya Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu wa TEC, ambaye sauti yake imekuwa kama kipaza sauti cha upinzani. Alipodaiwa kushambuliwa ndani ya makao makuu ya TEC yaliyolindwa vikali, taifa liliingiwa na mshangao. Lakini wengi wananong’ona kuwa tukio lile lilitengenezwa ili kuonyesha serikali kama mtesi na Kanisa kama mwathirika. Iwe kweli au la, lilimpa fursa mpya ya kumshambulia Rais. Hata hivyo, kinachouma ni kwamba wakati John Magufuli, Mkatoliki mwaminifu, alipokuwa Rais — enzi ambazo zilijulikana kwa ukali na woga — maaskofu walinyamaza. Hakuna aliyedai hafai, hakuna aliyehubiri kwa ukali huu.

Kwa nini sasa? Kwa nini tu wakati kiongozi ni mwanamke Mwislamu?

Na mashambulizi hayakuishia kwa Rais Samia pekee. Wamegeuza mishale yao kwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, wakimshutumu kwa “kutojitoa” kwa sababu anahudhuria shughuli rasmi pamoja na Rais. Lakini huu ni upotoshaji. Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iko wazi kabisa: marais na makamu wa rais wastaafu lazima wawe wajumbe wa Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu. Nyerere aliwahi, Mwinyi aliwahi, Mkapa aliwahi, na Kikwete naye yupo kwa wajibu. Hivyo kumshambulia yeye ni kudhalilisha si mtu binafsi tu, bali taasisi za kitaifa.

Baba Mtakatifu, hiki si tena ukosoaji wa kawaida. Hii ni vita isiyotangazwa. Ikiendelea, itaharibu urithi wa mshikamano ambao Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata Magufuli waliulinda. Maaskofu wanapohubiri chuki mara kwa mara, hawapandi imani bali wanamwaga mafuta juu ya nyasi kavu.

Kwa uhalisia, wanachofanya si unabii bali uchokozi. Sio mwongozo bali ni siasa. Na pale ambapo viongozi wa Kanisa wanageuka kuwa wanasiasa, wasitarajie Kanisa libaki na heshima yake ya kiroho; litabaki na vumbi la siasa.

Baba Mtakatifu, ninakuomba uingilie kati. Ni wewe peke yako mwenye mamlaka ya kumuita Askofu Mkuu Damian Denis Dallu wa Songea, aliyemkosea adabu Rais Mstaafu na kumfokea kama mtu wa mitaani bila staha wala diplomasia, maskini ya Mungu akiwa hajui Kikwete yupo vile kikatiba na sio kwa matakwa yake binafsi. Soma kiambatanisho Askofu Dallu wa huko Songea. No research no right to speak!! Haikutegemewa mtu anayejulikana ni wa Mungu kuwa na chuki ya kutoka povu mdomoni kwa sababu ya binadamu mwenzako. Inatisha kuwa na mtu wa kanisa kama wewe...

Pia usiwaache kina Padri Kitima, na uongozi mzima wa TEC na kuwaadabisha na mawaraka yao ya kila kukicha kana kwamba Ukatoliki ndio dini pekee duniani. Wakumbushe kuwa wito wao ni wa milele, si wa uchaguzi. Wakumbushe kuwa waliwekwa wakfu si kwa ajili ya kupiga kampeni, bali kwa ajili ya kuhubiri Injili na kuhubiri amani.

Kukaa kimya sasa kutatafsirika kama kukubaliana. Kuchelewa kuchukua hatua kutahesabiwa kama kushirikiana. Na historia itaandika kuwa katika enzi zako, Kanisa Katoliki Tanzania liliacha injili na kukumbatia siasa, likaacha umoja na kusambaza mgawanyiko.

Baba Mtakatifu, Save Our Souls. Tanzania inalia.

Kwa heshima kuu, lakini pia kwa ujasiri wa kukataa ukimya unaozalisha dhuluma,

Tarishi Hauwawi
Dar es Salaam, Tanzania
Papa anatawala Vatikani na wala siyo Tanzania
 
Mwambie Pia Baba Askofu Kuwa
*Raisi Muislam Anataka Amnyonge Mpinzani Wake TUNDU LISSU.
*Mwambie Wapinzani Wanauwawa Kila Kona Ya Nchi Na Rais Anajibu 'kifo Ni Kifo' Tu
*Mwambie Pia Waya Za INEC,NIDA Na CCM Zinasomana.
*mkumbushe Kuwa Kuna Askofu Wake Alipigwa Lungu Zito.
Hapo Nitakuona Una Akili Timamu.
Hii ndio jamiiforums niipendayo inaondoa stress.
 
Nikutajie jina la sinema hii?? Huna hata haya
We kweli boya message ya kwanza umesema sent and delivered nadhani hukuelewa msg hii ya pili unajidai kulijua hiyo filamu baada ya katibu tawala wa mkoa x kukutumia hayo maelezo inbox Kwa taarifa yako ujinga wenu tunaujua ila tunauhifadhi Kwa muda sahihi.
 
​

Baba Mtakatifu,
Ninaandika kwa dharura kutoka Tanzania, nchi ambayo historia yake imesimama kama mfano wa kuvutia wa mshikamano wa kidini. Zaidi ya miongo sita, Wakristo na Waislamu wameishi kama ndugu, wakiwa si tu watu wa imani bali Watanzania. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwanzilishi wa Taifa letu na mkatoliki mwaminifu, ndiye aliyepanda mbegu za uvumilivu huu. Aliongoza si kama Rais wa Kikatoliki, bali kama Rais wa Watanzania wote, na imani yake ilimfundisha kuheshimu wote.

Baada yake, Ali Hassan Mwinyi, Mwislamu, aliongoza taifa na amani iliendelea. Kisha Benjamin William Mkapa, Mkristo Katoliki, naye akafuatiwa na Jakaya Mrisho Kikwete, Mwislamu. Baadaye John Pombe Magufuli, tena Mkatoliki. Na sasa kwa mara ya kwanza tunao Rais mwanamke Mwislamu, Dk. Samia Suluhu Hassan. Kupitia mizunguko hii yote, Tanzania ilibaki kuwa kielelezo cha taifa linaloweza kubadilisha marais wa dini tofauti bila migawanyiko ya kidini.

Baba Mtakatifu, leo urithi huu unavunjwa — na si na magaidi kutoka nje, bali na Kanisa lenyewe kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Badala ya mimbari kuwa mahali pa wokovu, zimegeuzwa majukwaa ya kisiasa. Jumapili baada ya Jumapili, mahubiri hayazungumzii tena Injili, bali yanashambulia serikali. Hayatamki tena upendo wa Kristo, bali “udhaifu” wa Rais Samia. Wamekwenda mbali hadi kudai kuwa hafai kuongoza, hastahili muhula wa pili, na hawezi kuendesha taifa. Meza ya Ekaristi imegeuzwa kuwa madhabahu ya upinzani.

Kati ya sauti kali zaidi ni ya Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu wa TEC, ambaye sauti yake imekuwa kama kipaza sauti cha upinzani. Alipodaiwa kushambuliwa ndani ya makao makuu ya TEC yaliyolindwa vikali, taifa liliingiwa na mshangao. Lakini wengi wananong’ona kuwa tukio lile lilitengenezwa ili kuonyesha serikali kama mtesi na Kanisa kama mwathirika. Iwe kweli au la, lilimpa fursa mpya ya kumshambulia Rais. Hata hivyo, kinachouma ni kwamba wakati John Magufuli, Mkatoliki mwaminifu, alipokuwa Rais — enzi ambazo zilijulikana kwa ukali na woga — maaskofu walinyamaza. Hakuna aliyedai hafai, hakuna aliyehubiri kwa ukali huu.

Kwa nini sasa? Kwa nini tu wakati kiongozi ni mwanamke Mwislamu?

Na mashambulizi hayakuishia kwa Rais Samia pekee. Wamegeuza mishale yao kwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, wakimshutumu kwa “kutojitoa” kwa sababu anahudhuria shughuli rasmi pamoja na Rais. Lakini huu ni upotoshaji. Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iko wazi kabisa: marais na makamu wa rais wastaafu lazima wawe wajumbe wa Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu. Nyerere aliwahi, Mwinyi aliwahi, Mkapa aliwahi, na Kikwete naye yupo kwa wajibu. Hivyo kumshambulia yeye ni kudhalilisha si mtu binafsi tu, bali taasisi za kitaifa.

Baba Mtakatifu, hiki si tena ukosoaji wa kawaida. Hii ni vita isiyotangazwa. Ikiendelea, itaharibu urithi wa mshikamano ambao Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata Magufuli waliulinda. Maaskofu wanapohubiri chuki mara kwa mara, hawapandi imani bali wanamwaga mafuta juu ya nyasi kavu.

Kwa uhalisia, wanachofanya si unabii bali uchokozi. Sio mwongozo bali ni siasa. Na pale ambapo viongozi wa Kanisa wanageuka kuwa wanasiasa, wasitarajie Kanisa libaki na heshima yake ya kiroho; litabaki na vumbi la siasa.

Baba Mtakatifu, ninakuomba uingilie kati. Ni wewe peke yako mwenye mamlaka ya kumuita Askofu Mkuu Damian Denis Dallu wa Songea, aliyemkosea adabu Rais Mstaafu na kumfokea kama mtu wa mitaani bila staha wala diplomasia, maskini ya Mungu akiwa hajui Kikwete yupo vile kikatiba na sio kwa matakwa yake binafsi. Soma kiambatanisho Askofu Dallu wa huko Songea. No research no right to speak!! Haikutegemewa mtu anayejulikana ni wa Mungu kuwa na chuki ya kutoka povu mdomoni kwa sababu ya binadamu mwenzako. Inatisha kuwa na mtu wa kanisa kama wewe...

Pia usiwaache kina Padri Kitima, na uongozi mzima wa TEC na kuwaadabisha na mawaraka yao ya kila kukicha kana kwamba Ukatoliki ndio dini pekee duniani. Wakumbushe kuwa wito wao ni wa milele, si wa uchaguzi. Wakumbushe kuwa waliwekwa wakfu si kwa ajili ya kupiga kampeni, bali kwa ajili ya kuhubiri Injili na kuhubiri amani.

Kukaa kimya sasa kutatafsirika kama kukubaliana. Kuchelewa kuchukua hatua kutahesabiwa kama kushirikiana. Na historia itaandika kuwa katika enzi zako, Kanisa Katoliki Tanzania liliacha injili na kukumbatia siasa, likaacha umoja na kusambaza mgawanyiko.

Baba Mtakatifu, Save Our Souls. Tanzania inalia.

Kwa heshima kuu, lakini pia kwa ujasiri wa kukataa ukimya unaozalisha dhuluma,

Tarishi Hauwawi
Dar es Salaam, Tanzania
Imefika, lakini yanayoendelea Tanzania, yanajulikana. Mateso wanayopitia watanzania yanajulikana. Humo Kuna Wakristo na waislamu! Kazi ya Kanisa ni kuombea Dunia na watu wake. Kazi ya Kanisa ni kufundisha, kushauri, kuonya na kukemea mtu, watu bila kujali nafasi yake. Kiongozi wa Dini platform yake ya kuzungumza ni kwenye Mimbali au Madhabahuni. Na Kanisa Katoliki linatekeleza wajibu huo ipasavyo.

Kanisa lisiposikiliza vilio vya wengi kutokana na dhuluma za aina yoyote ile, litakuwa linakwepa majukumu na wajibu wake wa Kitume.

Kama hukunya Jana kwa sababu unazozijua wewe, Leo ukanya mavi rundo, ni haki mtu akikuuliza mbona Leo unakunya sana ilhali Jana hukunya hata mara moja?

Unapoandika mambo kama haya jitahidi usiwe umetuma vilevi vya aina yoyote ikiwemo bangi, mataputapu na makorokocho mengine.

Pia njaa, unafiki na uchawa visikufanye ujione kuwa wewe ndiye Bora na mwenye thamani kuliko wengine wote.

Vinginevyo, kijibarua hiki umekiandika kwa kutumiwa na wahuni, yakiwa ni Moja ya ya matokeo ya Ile funga ya Novena.

Poleni kwa maumivu lakini mdogo mdogo tu mwisho mtapona, Taifa litapona na watanzania watapona.
 
  • Akurupuke tu amnyonge bila sababu? Subiri mahakama ndio itaamua sio nyinyi humu mitandaoni
  • Mnauana wenyewe mnunue huruma kwa nguvu mnasingizia dola
*Nyumbu mfuata upepo huna maajabu kumsikiliza taahira
*Ulinzi wote mle Kurasini alipigwa ama kafanya usanii aonekane na ngeu?
Hoja zako zimenionesha wewe una akili mgando

Majibu Yako Yana-reflect Hauko Sawa,mtu Timamu Mwenye Busara Akirushiwa Jiwe Na Kichaa Hukimbia Asiwe Karibu Na Kichaa,so Mm Nakukimbia,Maana Nitaonekana Na Mm Niko Sawa Na Ww.
 
Sasa matusi ya nini kama mna hoja za kweli? Au unadhani wengine hawajui kutusi mtu kama wewe ambaye kwa lugha yako inaonekana mshamba wa bara na nyumbu mfuata mkumbo. ukileta matusi utatukanwa wewe hadi ukimbie. kuwa mstaarabu
Tulia hivyo hivyo mvaa makobazi wewe.
 
Ukiwa unaandika mambo Kama haya epuka kuandika uongo. Ulianza kuweka uongo hakuna atayeweza kuendelea kusoma

Tec hawajawahi kusema raisi aliyepo hatakiwi kuendelea,balihusema haki itendeke hatua zichukuljwe

Pia sio kwelikuwa walikaa kimya wakati wa magufuli
Tatizo ni kujiona nyie wasomi, werevu na wajuaji kuliko wengine wote. Hivi unadhani wasio wakatoliki hawajui kusoma katikati ya mstari. Mwongo anza na Kitima anayedanyanya kashambuliwa TEC Kurasini, tena ndani. How? Mgeni akiingia mle huwa anafungwa kamba mguuni. Sio physically lakini watu wote wanampiga jicho. Na siku hiyo ushahidi upo (omba register ya walioingia) hakukuwepo na mgeni!! Think!!!!1 NA hio hakuna wa kuendelea kusoma wewe ni nani uwasemee wengine?? Who the hell are you? au ndio katika kuendeleza kuwa dini ni katoliki tu?? Acheni ukuda nyie!!!!
 
​

Baba Mtakatifu,
Ninaandika kwa dharura kutoka Tanzania, nchi ambayo historia yake imesimama kama mfano wa kuvutia wa mshikamano wa kidini. Zaidi ya miongo sita, Wakristo na Waislamu wameishi kama ndugu, wakiwa si tu watu wa imani bali Watanzania. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwanzilishi wa Taifa letu na mkatoliki mwaminifu, ndiye aliyepanda mbegu za uvumilivu huu. Aliongoza si kama Rais wa Kikatoliki, bali kama Rais wa Watanzania wote, na imani yake ilimfundisha kuheshimu wote.

Baada yake, Ali Hassan Mwinyi, Mwislamu, aliongoza taifa na amani iliendelea. Kisha Benjamin William Mkapa, Mkristo Katoliki, naye akafuatiwa na Jakaya Mrisho Kikwete, Mwislamu. Baadaye John Pombe Magufuli, tena Mkatoliki. Na sasa kwa mara ya kwanza tunao Rais mwanamke Mwislamu, Dk. Samia Suluhu Hassan. Kupitia mizunguko hii yote, Tanzania ilibaki kuwa kielelezo cha taifa linaloweza kubadilisha marais wa dini tofauti bila migawanyiko ya kidini.

Baba Mtakatifu, leo urithi huu unavunjwa — na si na magaidi kutoka nje, bali na Kanisa lenyewe kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Badala ya mimbari kuwa mahali pa wokovu, zimegeuzwa majukwaa ya kisiasa. Jumapili baada ya Jumapili, mahubiri hayazungumzii tena Injili, bali yanashambulia serikali. Hayatamki tena upendo wa Kristo, bali “udhaifu” wa Rais Samia. Wamekwenda mbali hadi kudai kuwa hafai kuongoza, hastahili muhula wa pili, na hawezi kuendesha taifa. Meza ya Ekaristi imegeuzwa kuwa madhabahu ya upinzani.

Kati ya sauti kali zaidi ni ya Padri Charles Kitima, Katibu Mkuu wa TEC, ambaye sauti yake imekuwa kama kipaza sauti cha upinzani. Alipodaiwa kushambuliwa ndani ya makao makuu ya TEC yaliyolindwa vikali, taifa liliingiwa na mshangao. Lakini wengi wananong’ona kuwa tukio lile lilitengenezwa ili kuonyesha serikali kama mtesi na Kanisa kama mwathirika. Iwe kweli au la, lilimpa fursa mpya ya kumshambulia Rais. Hata hivyo, kinachouma ni kwamba wakati John Magufuli, Mkatoliki mwaminifu, alipokuwa Rais — enzi ambazo zilijulikana kwa ukali na woga — maaskofu walinyamaza. Hakuna aliyedai hafai, hakuna aliyehubiri kwa ukali huu.

Kwa nini sasa? Kwa nini tu wakati kiongozi ni mwanamke Mwislamu?

Na mashambulizi hayakuishia kwa Rais Samia pekee. Wamegeuza mishale yao kwa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, wakimshutumu kwa “kutojitoa” kwa sababu anahudhuria shughuli rasmi pamoja na Rais. Lakini huu ni upotoshaji. Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iko wazi kabisa: marais na makamu wa rais wastaafu lazima wawe wajumbe wa Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu. Nyerere aliwahi, Mwinyi aliwahi, Mkapa aliwahi, na Kikwete naye yupo kwa wajibu. Hivyo kumshambulia yeye ni kudhalilisha si mtu binafsi tu, bali taasisi za kitaifa.

Baba Mtakatifu, hiki si tena ukosoaji wa kawaida. Hii ni vita isiyotangazwa. Ikiendelea, itaharibu urithi wa mshikamano ambao Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata Magufuli waliulinda. Maaskofu wanapohubiri chuki mara kwa mara, hawapandi imani bali wanamwaga mafuta juu ya nyasi kavu.

Kwa uhalisia, wanachofanya si unabii bali uchokozi. Sio mwongozo bali ni siasa. Na pale ambapo viongozi wa Kanisa wanageuka kuwa wanasiasa, wasitarajie Kanisa libaki na heshima yake ya kiroho; litabaki na vumbi la siasa.

Baba Mtakatifu, ninakuomba uingilie kati. Ni wewe peke yako mwenye mamlaka ya kumuita Askofu Mkuu Damian Denis Dallu wa Songea, aliyemkosea adabu Rais Mstaafu na kumfokea kama mtu wa mitaani bila staha wala diplomasia, maskini ya Mungu akiwa hajui Kikwete yupo vile kikatiba na sio kwa matakwa yake binafsi. Soma kiambatanisho Askofu Dallu wa huko Songea. No research no right to speak!! Haikutegemewa mtu anayejulikana ni wa Mungu kuwa na chuki ya kutoka povu mdomoni kwa sababu ya binadamu mwenzako. Inatisha kuwa na mtu wa kanisa kama wewe...

Pia usiwaache kina Padri Kitima, na uongozi mzima wa TEC na kuwaadabisha na mawaraka yao ya kila kukicha kana kwamba Ukatoliki ndio dini pekee duniani. Wakumbushe kuwa wito wao ni wa milele, si wa uchaguzi. Wakumbushe kuwa waliwekwa wakfu si kwa ajili ya kupiga kampeni, bali kwa ajili ya kuhubiri Injili na kuhubiri amani.

Kukaa kimya sasa kutatafsirika kama kukubaliana. Kuchelewa kuchukua hatua kutahesabiwa kama kushirikiana. Na historia itaandika kuwa katika enzi zako, Kanisa Katoliki Tanzania liliacha injili na kukumbatia siasa, likaacha umoja na kusambaza mgawanyiko.

Baba Mtakatifu, Save Our Souls. Tanzania inalia.

Kwa heshima kuu, lakini pia kwa ujasiri wa kukataa ukimya unaozalisha dhuluma,

Tarishi Hauwawi
Dar es Salaam, Tanzania
Mbona hujaandika ni watu wangapi mmeua katika tukio la uchaguzi fake wa 29 October? Unataka kanisa alihubiri injili ipi zaidi ya hii ya kukemea ukandamizwaji wa haki ya kuishi?
 
Tatizo ni kujiona nyie wasomi, werevu na wajuaji kuliko wengine wote. Hivi unadhani wasio wakatoliki hawajui kusoma katikati ya mstari. Mwongo anza na Kitima anayedanyanya kashambuliwa TEC Kurasini, tena ndani. How? Mgeni akiingia mle huwa anafungwa kamba mguuni. Sio physically lakini watu wote wanampiga jicho. Na siku hiyo ushahidi upo (omba register ya walioingia) hakukuwepo na mgeni!! Think!!!!1 NA hio hakuna wa kuendelea kusoma wewe ni nani uwasemee wengine?? Who the hell are you? au ndio katika kuendeleza kuwa dini ni katoliki tu?? Acheni ukuda nyie!!!!
Tarishi mtetezi wa mauaji ya Watanganyika wasiokuwa na hatia kibaraka mkubwa wewe. Kanisa siku zote husimama na wanaoonewa na kudhulumiwa endeleeni na propaganda zenu mshibishe matumbo yenu lakini damu mliyomwaga itawatokea puani.
 
Back
Top Bottom