Barua ya wazi kwa Boniface Mwamposa

Barua ya wazi kwa Boniface Mwamposa

Kwako mtumishi wa Mungu, nakuomba Tafadhali sana usipuuze andiko langu, hili ni andiko la Mungu mwenyewe.
Wewe hakika ni mtumishi wa Mungu,ni kweli kabisa Mungu alikuita ili ufanye kazi yake,wanaokudharau na kukusimanga ni wa kuonea sana huruma,kwa sababu mimi nina ushahidi wa zaidi ya 100 %,kuwa kweli wewe ni mtumishi wa Mungu.
Niende kwenye hoja ya mada yangu kwako.
Mungu anapokuita shetani huwa anafanya vikao kuzimu ili aharibu kazi ya Mungu,na shetani ana mbinu zaidi ya milioni moja za kuangusha watumishi wa Mungu.
Wewe Mwamposa, shetani anahangaika ili aharibu kazi ya Mungu aliyokupa uifanye ,alichokifanya shetani kwako ni kuwaleta watawala wa Tanzania kuanzia Rais hadi wakuu wa mikoa watengeneze ukaribu kwako kwa maslahi yao ya kisiasa.
Walipojua maelfu ya watanzania wanakufuata ili waombewe basi wakaona ni bora waanze kukutumia ili wapate mtaji wa kisiasa.
Yaani uwashawishi watu waichague CCM, Mwamposa achana kabisa na harakati za kisiasa zitakuharibia kazi ya Mungu.
Siyo vibaya wewe kuwaheshimu viongozi wa serikali, lakini habari za siasa kwa chama chochote achana nazo, wewe piga injili na ufungue watu waliofungwa na shetani.
Narudia tena, Mwamposa achana na siasa ,fanya kazi ya Mungu aliyokuitia,muige mzee Mwakasege ,huyu mzee huwezi kumsikia ulimi wake ukiongelea siasa kwa namna yotote ile.
Narudia tena, Mwamposa achana kabisa na siasa,iko siku utaitwa Ikulu (kama alivyowahi kuitwa Gwajima) na utapewa jimbo la kugombea ubunge,hapo ndo itakuwa anguko lako kamili kwenye kazi ya Mungu na utabaki historia.
Shetani hajachoka kukufuatilia ili akuangushe, kwa sababu umeharibu kazi nyingi mno za shetani shetani kwa hiyo ana kisasi kikubwa mno na wewe.
Hiyo madhabahu unayoongoza siyo ya kwako ni ya Mungu,Mungu amekuamini wewe kuisimamia tu,ndo maana inaitwa madhabahu ya Mungu, siyo madhabahu ya Mwamposa,kwa hiyo acha kuichafua madhabahu ya Mungu kwa kukaa unaifanyia kampeni CCM .
Mungu ana watu wemgi mno, anaweza kuinua mwingine kufanya kazi yake endapo utaendelea kumkera.
Watu wanaenda kusali na kupokea uponyaji siyo kusikiliza kampeni za CCM kwenye madhabahu ya Mungu.
Mwamposa achana kabisa na siasa fanya kazi ya Mungu.
ALIYE KARIBU NA MWAMPOSA AMPELEKEE HUU UJUMBE.
Kumbuka aliwahi kusababisha vifo huko Moshi, japo polisi walitumia mbwembwe nyingi kumkamata lakini walimuachia na jambo lake likaisha kama vile hakuna waliofariki.
 
Mwanzo wa andiko lako umesema hili andiko ni la Mwenyezi Mungu cha kushangaza mwisho unasema aliyekaribu na Mwamposa ampelekee huu ujumbe!! Pia ndani ya andiko lako limejaa mambo ya siasa tu kwani Mungu hataki siasa!! Pia vipi Askofu Mwamakula anayehubiri siasa kupitia Chadema?
Mungu ni mwanasiasa wa kwanza ndio maana akina Daudi, Musa, Elia na kina Yusufu na Daniel Abednego na Meshaki walikuwa wanasiasa japo wa upinzani
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Mwanzo wa andiko lako umesema hili andiko ni la Mwenyezi Mungu cha kushangaza mwisho unasema aliyekaribu na Mwamposa ampelekee huu ujumbe!! Pia ndani ya andiko lako limejaa mambo ya siasa tu kwani Mungu hataki siasa!! Pia vipi Askofu Mwamakula anayehubiri siasa kupitia Chadema?
Na mbunge wa Kawe naye kupitia Chadema!
 
A

Alikuibia nini mkuu? na au alikutapeli nini? Hebu Tuambie
Kudanganya watu eti anaponya, which is not true. Anwadanganya watu wajinga masikini. Ni wizi kwa njia ya udangannyifu. Kosa la Jinai na Mungu hawezi kuwa naye maana ni uongo. Mwambie aende Muhimbili aponye wagonjwa.....
 
Kwako mtumishi wa Mungu, nakuomba Tafadhali sana usipuuze andiko langu, hili ni andiko la Mungu mwenyewe.
Wewe hakika ni mtumishi wa Mungu,ni kweli kabisa Mungu alikuita ili ufanye kazi yake,wanaokudharau na kukusimanga ni wa kuonea sana huruma,kwa sababu mimi nina ushahidi wa zaidi ya 100 %,kuwa kweli wewe ni mtumishi wa Mungu.
Niende kwenye hoja ya mada yangu kwako.
Mungu anapokuita shetani huwa anafanya vikao kuzimu ili aharibu kazi ya Mungu,na shetani ana mbinu zaidi ya milioni moja za kuangusha watumishi wa Mungu.
Wewe Mwamposa, shetani anahangaika ili aharibu kazi ya Mungu aliyokupa uifanye ,alichokifanya shetani kwako ni kuwaleta watawala wa Tanzania kuanzia Rais hadi wakuu wa mikoa watengeneze ukaribu kwako kwa maslahi yao ya kisiasa.
Walipojua maelfu ya watanzania wanakufuata ili waombewe basi wakaona ni bora waanze kukutumia ili wapate mtaji wa kisiasa.
Yaani uwashawishi watu waichague CCM, Mwamposa achana kabisa na harakati za kisiasa zitakuharibia kazi ya Mungu.
Siyo vibaya wewe kuwaheshimu viongozi wa serikali, lakini habari za siasa kwa chama chochote achana nazo, wewe piga injili na ufungue watu waliofungwa na shetani.
Narudia tena, Mwamposa achana na siasa ,fanya kazi ya Mungu aliyokuitia,muige mzee Mwakasege ,huyu mzee huwezi kumsikia ulimi wake ukiongelea siasa kwa namna yotote ile.
Narudia tena, Mwamposa achana kabisa na siasa,iko siku utaitwa Ikulu (kama alivyowahi kuitwa Gwajima) na utapewa jimbo la kugombea ubunge,hapo ndo itakuwa anguko lako kamili kwenye kazi ya Mungu na utabaki historia.
Shetani hajachoka kukufuatilia ili akuangushe, kwa sababu umeharibu kazi nyingi mno za shetani shetani kwa hiyo ana kisasi kikubwa mno na wewe.
Hiyo madhabahu unayoongoza siyo ya kwako ni ya Mungu,Mungu amekuamini wewe kuisimamia tu,ndo maana inaitwa madhabahu ya Mungu, siyo madhabahu ya Mwamposa,kwa hiyo acha kuichafua madhabahu ya Mungu kwa kukaa unaifanyia kampeni CCM .
Mungu ana watu wemgi mno, anaweza kuinua mwingine kufanya kazi yake endapo utaendelea kumkera.
Watu wanaenda kusali na kupokea uponyaji siyo kusikiliza kampeni za CCM kwenye madhabahu ya Mungu.
Mwamposa achana kabisa na siasa fanya kazi ya Mungu.
ALIYE KARIBU NA MWAMPOSA AMPELEKEE HUU UJUMBE.
Mtumishi wa Mungu yupi?
 
umesema Mwamposa ni mtumishi wa Mungu?

Mtumishi wa Mungu amewekwa ili awarejeshe watu kwa Mungu, atakemea maovu yanapotokea, ataonya pale penye kuonya, sasa mtumishi amekomaa kuipamba serikal kuwapamba viongozi na watawala hata pale anaona mambo yanaenda tofauti na inavyotakiwa
 
Tatizo akinyimwa kibali cha kufanya hiyo kazi, zile nguvu za miujiza huwa zinapotea; angalia waliomtangulia.
Mwisho wa siku utajiuliza zile nguvu ni za mungu au ni za nani? muhimu kula na kipofu tu.​
 
Huyo ni mtumishi wa sheytwani , mdanganyifu na ni mfanyabiashara haramu wa mafuta na maji ya upako
 
Back
Top Bottom