Barua ya wazi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Barua ya wazi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwanza kabisa, nataka kutoa shukrani zangu kwa Bunge kwa kazi nzuri mnayofanya katika kusimamia masuala ya kitaifa
Hapa 👆👆👆umetuingiza chaka mkuu, ikikupendeza tengua hii kauli.....!! Nikirud kweny hoja... Nna swali kdg je hayo makampuni ya waagizaji mafuta hayana uhusiano na wenye mamlaka? Means kama kuna kiongoz au viongoz aidha walipo au waliopita kweny kampuni hizi. Cz ukisema watumie ushauri wako kama kuna kundi mule itakua ngumu cz litaleta conflict of interest!!!
 
Kila mtu kakomalia dhahabu dhahabu as thought ni rahisi sana kupata hiyo dhahabu, hivi mnajua ugumu wa kupata hiyo dhahbu nyie au mnajiongelea tu?

Kama dhahabu inauzwa nje kwa dollars kwanini wasitumie hiyo dollar kununua mafuta? Hapa changamoto ni sera mbovu zinafanya gold dealers hawarudishi pesa nyumbani sababu ya sera mbovu za uwekezaji. Mtu anauza dhahabu ya 10M USD anarudisha 1M tu, rekebisheni sera zenu ila mkitaka BOT inunue dhahabu yenyewe huku wanataka purity kubwa kwa bei subpar hii biashara itawashinda asubuhi na mapema.

Uhaba wa dollar ni tatizo worldwide sio bongo tu.

Uhaba wa mafuta ni michongo ya watu wanabana wanasubiri bei mpya, in reality hakuna uhaba wa mafuta nchini bali serikali dhaifu.
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Dodoma, Tanzania.

Kwa heshima kubwa, ninaleta pendekezo langu kuhusu njia mpya ya kushughulikia changamoto ya uhaba wa mafuta na uhaba wa dola nchini. Tatizo hili litaathiri uchumi wetu na maisha ya wananchi wetu kwa muda mrefu, na naamini pendekezo hili linaweza kuwa na manufaa makubwa kwa nchi yetu.

Kwanza kabisa, nataka kutoa shukrani zangu kwa Bunge kwa kazi nzuri mnayofanya katika kusimamia masuala ya kitaifa. Napenda pia kutoa heshima kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali yake kwa juhudi zao katika kuendeleza nchi yetu.

Tatizo la uhaba wa mafuta na uhaba wa dola ni changamoto iliyolikumba taifa letu. Changamoto hizi zinaweza kudhoofisha uchumi wetu na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wetu. Kwa kuzingatia hili, natoa pendekezo lifuatalo:

Napendekeza kuwa waagizaji wa mafuta waweze kutumia dhahabu kama njia ya malipo kununua mafuta. Pendekezo hili linaweza kutekelezwa kwa kushirikiana na taasisi na vyama vinavyohusika na sekta hii, kama vile EWURA, Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania, Wizara ya Madini, Chama cha Wanunuzi na Wauzaji Madini Tanzania (TAMIDA), PBPA, na Wizara ya Nishati.

Njia hii inaweza kufuatwa kwa hatua zifuatazo:
  • Waagizaji wa mafuta wanaweza kutumia dhahabu kama njia ya malipo kununua mafuta nje ya nchi kwenye soko la kimataifa.
  • Mafuta yakiuzwa nchini, shilingi zitakazopatikana kutokana na mauzo ya mafuta zinaweza kutumika kununua madini ya dhahabu hapa nchini.
  • Baada ya kununua dhahabu, waagizaji wa mafuta wanaweza kubadilisha dhahabu hiyo na dola kwenye soko la kimataifa.
  • Dola zilizopatikana zinaweza kutumika kununua mafuta ya petroli, dizeli, na bidhaa zingine za mafuta kutoka nje ya nchi kwenye soko la kimataifa.
Mafuta yanaweza kuingizwa nchini na kusambazwa kwa njia ya kawaida na kuuzwa kwa shilingi. Fedha zitakazopatikana zitatumika tena kununua dhahabu, ambayo itapelekwa kwenye soko la kimataifa kwa ajili ya kubadilishwa na dola ambazo zitatumika kununulia mafuta.

Kwa kufuata njia hii, waagizaji wa mafuta watakuwa na njia mbadala ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini hata katika hali ambayo nchi ina uhaba wa dola za kutosha. Njia hii pia inaweza kusaidia kukuza biashara ya madini ya dhahabu na kuongeza mapato ya nchi yetu.

Napendekeza kuwa Bunge lifanye utafiti zaidi kuhusu pendekezo hili, na ikiwa itabidi, kuanzisha majadiliano na wadau husika ili kuona uwezekano wa kutekeleza pendekezo hili kwa manufaa ya nchi yetu.

Nashukuru kwa kulisoma pendekezo hili, na natumaini kuwa tutaweza kutafuta njia za kushirikiana kuleta suluhisho kwa changamoto hizi za kiuchumi nchini mwetu.

Kwa heshima na taadhima,

Elia Wilinasi

September 06, 2023
Kwani hiyo dhahabu wanaoweza kununua waagizaji mafuta ina uzwa wapi, na pesa yake inawekwa wapi
 
Kila mtu kakomalia dhahabu dhahabu as thought ni rahisi sana kupata hiyo dhahabu, hivi mnajua ugumu wa kupata hiyo dhahbu nyie au mnajiongelea tu?

Kama dhahabu inauzwa nje kwa dollars kwanini wasitumie hiyo dollar kununua mafuta? Hapa changamoto ni sera mbovu zinafanya gold dealers hawarudishi pesa nyumbani sababu ya sera mbovu za uwekezaji. Mtu anauza dhahabu ya 10M USD anarudisha 1M tu, rekebisheni sera zenu ila mkitaka BOT inunue dhahabu yenyewe huku wanataka purity kubwa kwa bei subpar hii biashara itawashinda asubuhi na mapema.

Uhaba wa dollar ni tatizo worldwide sio bongo tu.

Uhaba wa mafuta ni michongo ya watu wanabana wanasubiri bei mpya, in reality hakuna uhaba wa mafuta nchini bali serikali dhaifu.
Bado hujaelewa sehemu vyema. Naomba nifuatilie kwa makini kwenye hii comment. Nilichoshauri ni kwamba fedha Tsh zinazotengwa na serikali kwaajili ya kuagiza mafuta zitumike kununulia dhahabu inayopatikana kwa wachimbaji hapa nchini kila tunapotaka kuagiza mafuta. Waagizaji wa mafuta wavuke ng'ambo na hiyo dhahabu waiuze huko ili wapate dolla za kununulia hayo mafuta.
 
Kwani hiyo dhahabu wanaoweza kununua waagizaji mafuta ina uzwa wapi, na pesa yake inawekwa wapi
Kitu nilichokieleza ni sawa nawewe utumie mtaji wako kununulia dhahabu kwa wachimbaji wa dhahabu hapa nchini. Dhahabu utakayoipata uende nayo U.S.A kuiuza ili upewe dollars, dollars utakazopata nunulia bidhaa za kuja kuuza Tanzania.
 
MWALIMU NYERERE ANAMALIZA KWA USHAIRI KWENYE KITABU CHAKE.

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.

Ole wake Tanzania Tusipoisaidia
Niwezalo nimelifanya kushauri na kuonya nimeonya.

tahadhali nimetoa ushauri na kuonya nimeshatoka kitini zaidi nifanye nini.

Namlilia Jaalia atumulikie njia Tanzania ailinde WAOVU wasiishinde.

Amina Tena Amina Amina Tena amina

UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.
MWALIMU JK NYERERE
 
Bado hujaelewa sehemu vyema. Naomba nifuatilie kwa makini kwenye hii comment. Nilichoshauri ni kwamba fedha Tsh zinazotengwa na serikali kwaajili ya kuagiza mafuta zitumike kununulia dhahabu inayopatikana kwa wachimbaji hapa nchini kila tunapotaka kuagiza mafuta. Waagizaji wa mafuta wavuke ng'ambo na hiyo dhahabu waiuze huko ili wapate dolla za kununulia hayo mafuta.

Mkuu, with all due respect hujui unachozungumzia. Nifuate taratibu.

Mosi, the gov doesn't print new money solely kwa dhumbuni la kununua dhahabu tu.

Pili, at the moment dhahabu inanunuliwa in TSH kwa asilimia kubwa na inauzwa nje in dollars, naamini unajua hilo. DhAhabu yote inaenda nje ndo maana gold reserve yetu ni ndogo sana, unadhani wakienda kuuza huko hizvi sasa wanauza in TSH? So unachoongea ndo kinachofanyika tayari.

Nadhani swali hapo ni kwanini wauzaji wakipata hizo dollars hawarudishi dollars bongo au kwanini hawanunulii mafuta? Jibu hapo ni moja tu, sio kila mtu anayeuza dhahabu nje anarudisha dollars nchini, wengi zinaishia huko huko sababu ya sera mbovu za uwekezaji bongo. Na wengine wanafanyia shughuli zingine sio kununua hayo mafuta, huwezi kulazimisha watu nini cha kufanyia hela yao.

Hii ishu hata Biteko wakati yupo madini alishaongelea tafuta interview yake youtube.
 
Sio barter trade boss, dhahabu zinanunuliwa Tanzania kwa shillingi na zinakwenda kuuzwa kwenye soko la kimataifa kwa dolla. Dolla zinatumika kununulia mafuta.
At what exchange rate ? Hio hio ya Dunia at any given moment ? Kwani sasa hivi ukiuza dhahabu yako huko Mafichoni unatomia dollar au pesa hii hii ya madafu ?

Naona hapa tunakuwa tunaongeza some complications na technicalities; Kwa nchi ambayo ina gas asilia nadhani ni Uzuzu kuacha kutumia CNG kwenye magari na sehemu nyingine ili kupunguza matumizi yetu ya Dollar...; Hayo mengine ni kutengenezeana fursa tu
 
Kwa hapa serikali inatakiwa kuweka mazingira wezeshi ili iwe rahisi kubadili haya magari ili yatumie CNG, na vituo vya mafuta navyo viweke eneo la kujaza hizo gesi
 
At what exchange rate ? Hio hio ya Dunia at any given moment ? Kwani sasa hivi ukiuza dhahabu yako huko Mafichoni unatomia dollar au pesa hii hii ya madafu ?

Naona hapa tunakuwa tunaongeza some complications na technicalities; Kwa nchi ambayo ina gas asilia nadhani ni Uzuzu kuacha kutumia CNG kwenye magari na sehemu nyingine ili kupunguza matumizi yetu ya Dollar...; Hayo mengine ni kutengenezeana fursa tu

Word.
 
Tatizo letu linahitaji utatuzi wa haraka. CNG ni nishati mbadala ambayo tukiitumia itaweza kutufanya tuache kutegemea mafuta toka nje ya nchi. Shida tuliyo nayo kwenye CNG miundombinu yake bado haijakamilika kutufanya tuwaeleze watanzana watumie CNG. Tanzania nzima tuna vituo viwili tu vya kujaza CNG. Lakini pia hatuna karakana za kutosha za kubadilisha magari yetu yote yatumie CNG. Vituo na karakana zote zipo Dar es Salaam vipi kuhusu mikoani. Hivyo kutatua tatizo linalohitaji utatuzi wa haraka la uhaba wa mafuta kwa kutumia njia ya nishati ya mbadala ya CNG tutasababisha matatizo kwa watanzania. Ili tutumie CNG kwenye magari tunahitaji extensive investment ya kujenga vituo vya kujaza gesi Tanzania nzima.
 
Ngoja kwanza tuache argument ya iwapo hata hio suggestion yako ni solution (lets assume it is)..., Tatizo kubwa la hii nchi ni mipango ya muda mfupi na sio kutatua mambo kwa muda mrefu (long term planning) siongelei kizazi chetu naongelea miaka na miaka ijayo who cares kama tukifunga mikanda leo hata kutumia punda kama tunatengeneza kwa future ? Nani amesema tufungie private cars; vipi tukianza na magari ya abiria, magari ya serikali na baadhi ya idara ambazo zipo chini ya Serikali moja kwa moja ? hayo ya kupata vituo vingi n.k. yatakuja yenyewe baada ya wawekezaji kuona hili suala linalipa kwao; Na gharama ambayo ingetumika kuagiza mafuta ikitumika kama ruzuku kwa hawa wafanya biashara wenye CNG plants nadhani watu automatically wataitikia wito...

Ila saying that huenda Gas sio yetu tena na ukijikuta hawa walamba asali wanapandisha bei kwa excuse yoyote ile (kikulacho ki nguoni mwako)
 
Back
Top Bottom