kimpango
JF-Expert Member
- Apr 24, 2011
- 600
- 717
Mheshimiwa katibu hatuna namna ya kukufikia zaidi ya njia hii tupokee
27th Julai 2020
KWA
KATIBU MKUU (CCM )TAIFA
NAKALA KWA
MWENYEKITI WA CCM TAIFA ,
KATIBU WA CCM MKOA WA PWANI,
KATIBU WA CCM WILAYA YA KISARAWE,
KATIBU WA CCM KATA YA KILUVYA
Yah: MALALAMIKO KUHUSU UCHAGUZI WA KURA ZA MAONI UDIWANI KATIKA KATA YA KILUVYA- WILAYA YA KISARAWE (CCM)
Mheshimiwa Katibu Mkuu,
Kwanza kabisa pole majukumu na msiba mkuu uliokikuta chama chetu na Taifa kwa ujumla kwa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu na Mwenyekiti wa Taifa wa tatu wa chama chetu pendwa CCM, Hayati Benjamin William Mkapa. Mwenyezi Mungu amrehemu. Mheshimiwa tunaandika haya nikiwa mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa kata ya Kiluvya wilaya ya kisarawe waliokuwa wanaruhusiwa kupiga kura za maoni kuhusu wagombea udiwani kwa mujibu wa kanuni za chama uliofanyika jana tarehe 25 Mwezi Julai 2020.
Mheshimiwa, kwa umoja wetu kama wanachama na Watanzania wazalendo tulikwisha adhimia kuirudisha kata yetu kutoka upinzani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2015 na CHADEMA kupitia aliyekuwa mgombea wao na baadaye Diwani wetu bwana Aidan Kitare.
Mheshimiwa nakiri kusema kilichosababisha wakati ule chadema ishinde ni makundi ndani ya CCM na kuwepo na wasaliti wa wazi waliomsaidia Bwana Kitare kushinda kwa sababu ya Uongozi kumkumbatia na kumvusha mgombea aliyekuwa hakubaliki japo si CHADEMA wala Bw. Kitare hakuwa chaguo la wengi.
Mheshimiwa wakati tumejipanga na kurudisha umoja wetu na kujipanga na uchaguzi mkuu kurudisha kata kwa ushindi wa asilimia zote . Kuna njama za wazi zilizofanywa na Viongozi wetu wa Chama akiwemo mwenyekiti kutuhujumu kwa kuvuruga uchaguzi kwa maslahi yao binafsi
Kwanza tarehe 28 juni 2020 Bwana Kitale alitangazwa kujivua uanachama wa Chadema na kurudi CCM (hilo sio tatizo) tatizo ni mwenyekiti NA KATIBU wetu (wa kata)alivyoanza kumpigia kampeni kwa kupigia simu wajumbe (mimi nikiwepo) na kuwatembelea hasa usiku akiwaomba wamsamehe na kumpigia kura akichukua fomu kwa kuwa ni maagizo ya uongozi wa CCM Mkoa Na Wilaya pamoja na mbunge Mh. Jafo lakini hii haikuwa na nguvu baada ya uongozi wa juu kusimama na kusema hakuna Mtu aliyetumwa japo madhara yake yalishasambaa kwa wajumbe wengi ambao pia wako vijijini mbali na vyombo vya Habari kama magazeti, tv na redio.
Pili, watia nia wa udiwani ambao wengine tunawafahamu walipotoka kwenye kikao chao cha kwanza walisema wanasikitika Mwenyekiti wa Kata na Katibu wake wamewatamkia kuwa wao (viongozi wanamjua mshindi ingawa kuna watia nia wengi) hili ni Dhahiri hata wakipigiwa simu (watia nia wote 29 )wataeleza hivyo. Pia Dhahiri shahiri najulishwa ndani ya kikao hicho Mwenyekiti wa CCM kata aliwaambia watia nia kuwa anayejisikia kumpa katibu wa kata nauli ana safari ya Wilayani ampe yawezekana atafikiriwa kwenye tatu bora ..wachache walimpa hadharani
Tatu, kulikuwa na viashiria vingi vya rushwa kwa mtiania aliyeongoza kura za maoni kwa kutembea hadi usiku wa manane kuomba kura ikiwemo kusafirisha baadhi ya wajumbe na kukaa nao baa Pamoja na vitendo vya kusherehekea ushindi pamoja na viongozi tajwa hapo juu usiku wa tarehe 25th Julai 2025 katika katika baa 2 tofauti.
Nne, Kanuni za Chama na Katiba ya nchi ilikiukwa siku ya upigaji kura
Mheshimiwa Katibu Mkuu Tunaushukuru uongozi wa Mwenyekiti Taifa na Viongozi wote waandamizi kwa kutaka kura za haki na za wazi kuondoa minong’ono hili limesaidia ingawa huku kwetu(Kata ya Kiluvya -Wilaya ya Kisarawe imekuwa ndivyo sivyo. Kwa sababu zifuatazo ambazo ndio msingi wa MALALAMIKO haya.
Haki ya wapiga kura na wapigiwa kura hazikulindwa
Mheshimiwa ni haki ya kikatiba kuwa mtanzania mwenye umri uaofaa ana haki ya kupiga na kupiggiwa kura, ni uamuzi wa juu kuwa wagombea wote waliochukua na kurudisha fomu wapigiwe kura lakini huku kwetu haikuwa hivyo kwani baadhi ya majina ya WAGOMBEA hayakuonekana kabisa ingawa wagombea walikuwepo wakalalamika likafumbiwa macho.
Pia, wagombea wengine waliokuwa wanaonekana ni tishio kwa mgombea aliyekuwa akibebwa na viongozi majina yao yalikosewa yote matatu kwa mfano mtu aliyeitwa Tabu Abdallah Msigani aandikwe Malitabu abdul Mchigani. Hivyo kufanya wapiga kura tukose haki kwa kudhani kuwa wagombea tuliowaamini hawapo
Mheshimiwa hii inaweza kuoneshwa Dhahiri ukiomba karatasi ya kura (ziilizoondoka na Kiongozi wa wilaya ) aliyesimamia uchaguzi na fomu yoyote ya mgombea ya kuomba kuwania nafasi tajwa mfano ya mgombea Ayoub Mwaikwila Mgombea huyu hakujitoa lakini jina aliloandika kwenye fomu ya kuomba uongozi na jina lililokuwepo kwenye karatasi ya kura ni tofauti ila ila aliambiwa ajinadi kwa namba5 watabadilisha kwenye karatasi za kura lakini haikufanyika.
Pia, mgombea Allen Alfred Mollell jina lake halikuwepo ingawa aliambiwa kuwa eti jina lake limekosewa ila Ajinadi kwa namba moja kwenye jina lingine lililokuwa limeamdikwa Alin Alphonce Mouew na viongozi wa uchaguzi wakaahidi watabadilisha ila haikuwa hivyo ingawa wagombea hawakujua kwani wengi wao si wapiga kura hii imetufanya sisi tukose haki yetu ya msingi ya kupiga kura vkwa wagombea wanaofaa zaidi pia waadilifu kwa chama.
Pia wajumbe wengi ambao hawakuwa na sifa waliruhusiwa kinyume na kanuni na taratibu za chama, wengine walikaimishwa kwakuwa wenye nafasi hizo hawapo au wamesafiri ila wakakaimishwa nafasi tajwa kwa haraka asubuhi ya kupiga kura (hata tulipohoji walikuwa hawajui nafasi wanazokaimu)
Pia Baadhi ya Wagombea hawakidhi sifa za kisheria kuwa Madiwani kwa kutokuwa wakazi wa eneo la kata yetu kwa muda huu (Kwa nafasi ya Udiwani) mfano Bw Aidan Kitare baada ya kuchaguliwa 2015 akiwa anaishi kwa wazazi wake alihamia Kigamboni pia kuna mama mmoja ni wazi si mkazi wa Kiluvya ni mkazi wa Segerea (Wapinzani wanasubiri watu wa aina hii wapitishwe waweke mapingamizi.
Mheshimiwa haya na mengine yasipozingatiwa yanaweza kukigawa tena chama maana yataleta mpasuko kwa kuwa lengo la uongozi wa juu kumpata mtu anayepita kwa haki,pia anayekubalika ndani na nje ya ccm na anayeuzika halipo Kwenye Kata Yetu Ya kiluvya.
Mheshimiwa Tumeandika humu tukiamini chama chetu kinafuatilia kila kitu kinachoweza kukichafua chama ili kutoharibu sifa nzuri sana iliyowekwa na uongozi wa chama taifa zima Chini ya Uongozi wa Mwenyekiti Wetu wa Taifa Dr. John Joseph Magufuli.
KIUFUPI WATIA NIA WENGI MAJINA YAO YALIKOSEWA KWA SABABU KUU MBILI
Namba za wagombea nilizonazo kwa ajili ya reference ya yaliyojiri ni ifuatavyo
Aidan Kitare ---0784 642 383
Raphael Gasper --0683 217 447
Mushobozi Gosbert Ndyamka -- 0713 413 360
Ayoub Mwaikwila -- 0652 752 010
Allen Mollel -- 0713 971 399
Beatrice mwakasala -- 0672424 035
Katibu msaidizi wa CCM kata -- 0712 038 992
Viongozi wa jumuia ya vijana
Mr David -- 065505171
Mr. Elias --0673689855
Pole na samahani kwa andiko refu na kushindwa kufata mtiririko wa ngazi nza kiuongozi kwa wasiwasi kuhusu usalama wetu kwa kusema ukweli huu kwani baadhi ya viongozi ndio washutumiwa.
Tuanaamini kero hizi zitafuatiliwa na kurekebishwa kwa maagizo na ufuatiliaji wako uliotukuka
Asante
Wako wanachama watiifu kutoka matawi mbalimbali kata ya Kiluvya, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

- Kuwachanganya wapiga kura hasa wazee na vijana wa vijijini kwa kuwa wengi wao hawajui kusoma na kuandika hivyo kukariri majina ya mwisho ya mgombea
- Kuandika majina tofa uti ili wagombea ambao majina yao yamekoseawa akiongoza kura za maoni yule viongozi waliokuwa wakimtaka akate rufaa kuwa aliyeshinda hakugombea