Barua ya wazi kwa Lady Jay Dee na Ruge Mutahaba!

Barua ya wazi kwa Lady Jay Dee na Ruge Mutahaba!

Hata kupangilia hoja zako hujui, unaandika as if unaandika majina ya wapiga kelele baada ya kubananishwa na mwl wa zamu, umerudia rudia maneno kama unaimba chorus, umepotezea tu watu muda na utumbo wako huu!

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
bora ungeweka audio tuisikilizi kuliko hilo bandiko lako la kigazeti gazeti
 
kwa hiyo prince unataka kama mtu alikutoa aendelee kukunyonya for the rest of your miserable life in earth? Unaleta zile za 'mimi ji babako na ndo nilikuleta duniani. Lazma usomee ualimu'. Wakati huo baba mwenyewe kachooka na shati limechanika mgongoni.

Na barua hii (nimeisoma yote hata nukta), ni ujumbe kwa jaydee na madj wa ruge (umewashtaki kwa boss wao). Haujaadress issues.

Nimemeona kitu kimoja au viwili. Kwamba hii barua imemlenga Jide wala si Ruge. Iko Biased imemkandamiza Jide lakini haikuonyesha alitakiwa kufanya nini after being fed up na unyonyaji wa Clouds, je akae kimya afe na tai shingoni?

Pili, kama si Ruge kaandika barua hii basi ni mtu wake wa karibu. It seems anataka kuonesha kuwa Jide ni mkosaji lakini indirectly kuwa kujifanya fair kwamba anamsema na Ruge.
 

Leo hii nimekaa chini na kisha kuiandika barua hii kwenu, nataka mkae chini na kuisoma pamoja, mkimaliza kuisoma najua mtajua kipi kinachotakiwa kufanyika kwenu. Kama mpo kwenye ugomvi, hebu kuweni na amani japo kwa dakika tano tu, yaani dakika tano tu za kusoma barua hii na baada ya hapo ugomvi wenu uendelee zaidi huku maneno ya barua hii yakiwa yamewaingia vichwani mwenu.

Lengo la barua hii ni kuwang’ata sana na kisha kuwapuliza, maisha yale yale kama ya panya afanyayo usiku. Ok! Nianze na nani sasa? Nianze na jay Dee au Ruge? Nianze kumng’ata nani sasa? Acha niache na Jay Dee kwani naamini sana katika msemo wa kizungu kwamba ‘Ladies first’.

Kwanza nilikuwa nimesahau dada kwamba Ruge na maswahiba zake ndio walikutoa mpaka wewe kufika hapo ulipo, juzi kati ndio alinikumbusha katika kipindi cha Breakfast. Nilimsikia akiongea, alionekana kuwa makini sana kwa kila neno ambalo alikuwa akilizungumza na mwisho wa siku nikasema kwamba wewe ulikuwa na makosa, sitaki kuzungumzia sana hilo kwani bado ;Muwamba ngoma huvutia kwake’.

Naomba nikuulize swali moja kabla sijaendelea, hivi ni kitu gani ambacho kilikupeleka mpaka kuandika kwenye mitandao ya kijamii mambo kama yale? Ulifikiri itasaidia? Ulifikiri tukijua tutamfuata Ruge na kumdiss au ulifikiria nini? Ok! Labda uliandika mambo yaliyo sahihi sana na ambayo ulifanyiwa lakini haukutakiwa kufanya jambo kama hilo. Kwa upande wangu mimi umenipa uhakika wa asilimia mia moja kwamba wasanii wa Kibongo hawana washauri na kama wanao basi hao washauri hawana akili, na kama wana akili basi hawafanyi kazi zao kwa usahihi na hata kama wanafanya basi kutokana na kutokulipwa, hawasimamii sana kazi zao juu yako.

Unavyofikiria kama wasanii wote Tanzania wangeamua kuandika mitandaoni mambo wanayofanyiwa na watu wengine unadhani nani angesalimika hapa? Si hata mimi ningeandikwa. Hivi unafikiri Rais Kikwete angeamua kuandika mambo mengine anayofanyiwa na watu nani angesalimika? Hivi ni nani ambaye alikushauri kuchukua uamuzi kama huo dada yangu? Au kama ulidhani ingesaidia nini hasa?

Au maneno ya watu watakaoonyesha sapoti ndio ulitaka kuyasikia?

Nisikilize vizuri dada yangu ambaye sijawahi hata kukaa nawe meza moja na kuongea. Ulichokifanya sio, ulichokifanya hakikustahili kufanywa na mtu kama wewe. Nilichodhani ni kwamba kama msanii mkubwa uliyekuwa kwenye gemu kwa kipindi kirefu ungekuwa mfano mzuri wa kuigwa kumbe umenidhihirishia kwamba nilikuwa nafanya makosa kufikiria hivyo.

Unajua wakati mwingine inakupasa mtu uonyeshe kwamba umekuwa katika hatua fulani ya maendeleo, hatua ambayo inaonyesha kutojali kitu chochote kile. Hivi umewahi kuwasikia mastaa wa nje wakiandika mambo wanayofanyiwa na watu ambao wamewatoa kimuziki hadharani? Wewe kwa nini umefanya hivi, hilo ni kosa kubwa sana ulilolifanya ambalo litakwenda kukugharimu sana hapo baadae, simaanishi kimuonekano, linaweza kuiharibu hata saikolojia yako baadae.
Kumbuka kwamba sipo hapa kukutea wewe au Ruge, hapana, nipo hapa kuongea kile ambacho kimenigusa mimi kama mpenzi wa muziki wako na mpenzi wa kituo cha Clouds Fm. Kama ninavyokupa hapa madongo basi hata Ruge nae nitampa hivi hivi kwani jambo lenu limeteka sana hisia za watu, limeteka sana mitandao ya kijamii Tanzania.

Umenifanya nigundue kwamba mara zote wahenga wamekuwa sahihi hasa ulipoudhihirisha msemo usemao ‘Shukrani ya punda mateke au ule sijui umfadhiri mbuzi utakula mchuzi kuliko binadamu ana maudhi’. Sisi ni binadamu dada, binadamu kama binadamu hajakamilika, kuna mapungufu ambayo tunayo kama binadamu, na pale unapoona kwamba binadamu kakosea basi jua hapo ndio ubinadamu wake umekamilika kwani bila kukosea, huko si ubinadamu bali utakuwa Uungu.

Mpaka sasa hivi sikufichi, sijaona mantiki ya wewe kuandika ishu hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kutufanya sisi kuisoma, inaonyesha kwamba washauri wako nao ni chenga tu kama walivyokuwa washauri wa Diamond kwa kuandika maongezi yake na Wema mtandaoni. Aya tufanye umekwishaandika, umepata faida gani dada? Huyo Ruge kafungwa jela? Huyo Ruge kapigwa? Watu wameacha kuiskiliza Clouds Fm au? Si unaona hakuna kilichobadilika! Basi jua kwamba kuandika kwako hakukuwa na faida yoyote ile.

Ninachokifahamu mimi dada yangu, kuna kitu ulikuwa ukikitaka sana na ndio triki ambayo imekuwa ikifanywa na wasanii wengi sana, wanapoona wanataka kutoa filamu, wanaanzisha skendo nyingi ili filamu zinunuliwe kwa sababu watakuwa kwenye chati, na mwimbaji anapotaka kutoa albamu anaanzisha skendo nyingi ili albamu inunuliwe kwa sababu anakuwa kwenye chati, sisemi kwamba inaweza kuwa hivyo, ila inawezekana kuwa ni moja ya triki, hakika umefanikiwa, uzinduzi wa albamu yako watakuja wengi, hata mimi nitakuwa mmoja wapo kwani sasa hivi skendo yako na Ruge imekuwa kichwa cha habari cha kila magazeti hapa Bongo.

Sikufichi dada, hicho ulichokifanya kimesapotiwa zaidi na watoto wa mitaani kama sisi ila kwa watu wazima, wengi wao wamekiponda. Haukutakiwa kuchukua hatua hiyo uliyochukua, ilitakiwa kukaa chini kibinadamu na kisha kuzungumza na mambo yangekwisha kabisa ila hatua uliyochukua si nzuri. Umechukua hatua hiyo kwa kudhani kwamba ungemaliza tatizo kumbe walaaaaa, halijakwisha kabisa na ndio kwanza linaendelea vile vile, ndani wiki tutasahau na maisha kuendelea kama kawaida.

Mshauri…mshauri….sidhani kama kuna mtu alikushauri kufanya jambo hili, na kama kuna mtu alikushauri, kiukweli alitaka kukupotezea mashabiki pamoja na kuonekana kwamba haufai, kama itawezekana, mtimue huyo mshauri kwani si mshauri mzuri katika kufanikisha ukitakacho. Sitaki kuongea mengi sana kwako kwani kama nitaongea sana, nina uhakika kesho utatangaza kuacha muziki kwani naweza kuongea maneno makali yenye kukatisha tama na kisha kesho ushauriwe tena na mshauri huyo na mimi uje kuniandika, sipendi hilo, sipendi uache muziki, nahitaji kuendelea kuisikia sauti yako nzuri. Kama una swali, jaribu kunicheki kwa email yangu nitakujibu personal.

Ngoja nije kwa Ruge sasa. Koh koh koh koh. Nimekohoa mara nne kuonyesha kwamba ili niongee kuhusu wewe itanipasa sauti yangu isikike vizuri sana na iweze kusikiwa na kila mtu. Ngoja nianze na tetesi kwanza. Miaka kadhaa ya nyuma nilisikia kwamba madj wako wanachukua fedha za wasanii wanaotaka kupigiwa ngoma zao ili kuzirusha hewani. Ni kweli? Kama ni kweli, basi hiyo naweza kuiita RUSHWA na serikali itatakiwa iwaandalie kamati.

Nchini Marekani, MTV ananunua nyimbo ya Kanye West na kisha kuipiga, yaani hakuna kituo kinachopita nyimbo ya msanii bure, lazima ulipie na msanii ndio anakukubalia ila hapa Tanzania mambo nayaona yanakwenda Kichina zaidi. Msanii lipa wewe ngoma yako ipigwe.

Hivi kwanza hizo tetesi ni za kweli au ni stori za sehemu za vibanda vya wauza kahawa? Kama msanii chipukizi anauza mkaa ili apate fedha ya kutoa ngoma yake na nyie kumdai tena fedha, hiyo ni dhambi, ni dhambi kubwa hata kama Baba wa taifa angekuwepo angekifungia kituo chenu kwani kwa kufanya hivyo mnapelekea muziki wa Tanzania kushuka kwa kuwa na wasanii wachache.

Juzi kati nilikusikia ukiongea bwana, sauti yako ya kipole na unyenyekevu, uliongea mambo mengi sana, wema ambao ulimfanyia Jay Dee na mwisho wa siku kuja kufanya alichokifanya. Ulikuwa sahihi kulalamika kaka kwani alichokifanya hakikuwa sahihi japo na wewe lazima nikwambie maneno mawili matatu.

Kwanza unajua kwa kile kilichotokea East Africa Redio na vituo vingine vimekuja juu zaidi? Sisemi hivyo kwa kumaanisha kwamba East Africa ipo chini, hapana, ile ipo juu miaka 800 hamuwafikii kuanzia redio hadi televisheni na ndio maana vipindi vingi vya televisheni mlikuwa mkiwaiga kama Uswazi, Planet Bongo na Friday Night Live.
Mara ya kwanza nilipomsikia dada akiongea, nilidhani una makosa, ila nilivyokusikia ukiongea, nikasema dada ana makosa. Sasa nani ana makosa hapa? Hatujui na ndio maana nikakwambia jinsi nilivyogombana na demu wangu majuzi. Kila atakayeulizwa, atavutia ngoma kwake.

Kama kweli ishu hizi za kuwabania wasanii wadogo wasipigiwe nyimbo bure linafanyika, waambie waache na waridhike na mishahara yao bhana. Au unawalipa pesa kidogo mpaka kuamua kufanya hivyo? Mambo wanayoyafanya sio mazuri kabisa kaka na ninaamini hata kama ungekuwa unafanyiwa wewe, usingeweza kukubali kabisa. Tamaa walizozileta (Kama kweli wanafanya hivyo) nazo zitakugharimu sana kama Mkurugenzi wa Clouds japokuwa gharama zake hautoweza kuziona kwa macho kipindi hiki mpaka pale ugonjwa utakapokuwa mkubwa.

Wasanii wa muvi kila siku wanalalamika kwamba Mhindi anawanyonya, watanzania wengi tunasema kwamba Mhindi ni mtu mbaya sana anayewafanya wasanii wa filamu wasiendelee. Kwa wanamuziki huku hayupo Mhindi, huku kuna mtu wweusi mwenzetu ambaye kila siku wasanii wanalalamika kwamba mnawanyonya. Kwa nini kila siku iwe Clouds? Kila msanii Clouds, jamani hata kama maneno hayo ni ya uongo, hivi itawezekana kweli wasanii wote hao wawe waongo? SIDHANI.

Inawezekana kwamba mambo haya yanafanyika bila wewe kujua chochote kile, inawezekana kwamba umejua lakini umewaacha kwa kuwaona kwamba wao ni watoto wa mjini, labda inawezekana kuwa hivyo. Kaa nao chini, zungumza nao na wajue wajibu wao kuja hapo si kuchukua fedha kwa wasanii kama wanavyofanya kwani asilimia tisini ya wasanii maisha yao ni duni, unapomwambia msanii atoe laki nne umpigie nyimbo na wakati yeye mwenyewe hela ya kurekodia aliuza magunia ya mkaa aliyoyatafuta kwa miezi sita mtakuwa mnamnyonya sana.

Punguzeni mambo yenu ya hapa na pale na mtambue kwamba sisi wote ni Watanzania ambao inatupasa kubebana na si kuleteana mambo kama hata wanayoyafanya hao madj, wanazingua ile mbaya na wanarudisha nyuma soko la muziki hapa Bongo huku wakisikika hewani wanajisifia kwamba wanainua wanamuziki bila kuzisema fedha wanazowaambia wawalipe.

Waambie wabadilike ila ishu ya wewe na Jay Dee, hata msikae chini kwa sasa, najua kila mtu ana hasira zake amani itakuwa ngumu kupatikana. Kama vipi kaeni chini baada ya hata mwaka mzima ili kila mtu awe na amani zaidi kuliko kipindi hiki ambacho kila mtu ana hasira na mwenzake.

Kwa dada, ulichokifanya cha kuandika mambo personal kwa facebook hasa ugomvi sio kizuri na kwa kaka nawe ulichokifanya cha kuwafumbia mdomo watu wako sio kizuri pia. Wote badilikeni na tuendelee kupata burudani kutoka kwenu wote. Ila tukitaka kumsikiliza mmoja mmoja, mambo yatakuwa yale yale kama mimi na demu wangu.

Ni Mimi Nyemo The Prince.- (MWANDISHI)

N:B. Japokuwa barua imeandikwa kwa mwandiko mbaya na karatasi kufutwafutwa kila wakati, naamini mmeweza kuisoma vyema kabisa.

UMETUMWA WEWE, na ndio maana ulileta post yako ya Eti wimbo wa Joto Hasira umechuja mapema. Sikujua kumbe ulianza kazi hii siku nyingi. Rudisha tu hela yao, kama Mjomba alivyorudisha nauli, waambie kazi imeshinda. Wala hueleweki huku. Jide bado yuko juu sana kote kote!
 
UMETUMWA WEWE, na ndio maana ulileta post yako ya Eti wimbo wa Joto Hasira umechuja mapema. Sikujua kumbe ulianza kazi hii siku nyingi. Rudisha tu hela yao, kama Mjomba alivyorudisha nauli, waambie kazi imeshinda. Wala hueleweki huku. Jide bado yuko juu sana kote kote!
una mawazo mazuri sana
 
Yule dada kinachomsumbua ni mapepo\ majink. Hakuna la zaidi.
 
Wanajamvi, naomba nimhoji mwandishi wa barua hii kwa mambo yafuatayo

1. Suala la Jide kusema hadharani yale aliyofanyiwa na Clouds media, limemchafua yeye kiaje?

2. Ukisema kwamba kauli za Jide kuhusu Clouds media hazina athari zozote kwenye jamii, umefanya utafiti kujua ni kwa kiasi gani jamii inawachukulia clouds media kwa sasa? Umeongea na wasanii kujua maoni yao?
3. Umezungumzia suala la ma-dj wa clouds kuomba hongo ili wacheze miziki ya wasanii, unafaham kwamba clouds media wanawanyonya wasanii hata kwa shoo ambazo huwaandalia?
4. Suala la Jide kuzungumza mabaya ya Clouds Media ni mwendelezo wa harakati za Mr. II (sugu) na vinega kupiga vita unyonyaji wa Clouds, je unafaham hilo?
5. Ni lipi jema ambalo Jide angefanya ili kuokoa sanaa yake na wasanii wengine ambao wamenyonywa kwa muda mrefu na Clouds Media (Akiwemo #Scorpio - RIP Ngwair)?

Tafadhari nijibu maswali hayo ili uwe angalau umegusa upande wa pili wa barua yako! Umezungumza sana kuhusu Jide, lakini umewatetea sana Clouds Media. Maswali yangu yamelenga kufaham uelewa wako kuhusu upande wa clouds kwenye sakata hili.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Barua huwa haziandikwi hivi, ----- tupu, sio tatzo lako mmezoea kuandika mi essay kujaza booklet
 
Sio lazima kila unachokisikia au kukiona ukichangie au kusema lolote juu yake, unaweza kukuta unajidhalilisha buure! Ona sasa unaonekana ni mtu ambaye ufahamu kiduuchu sana kama mwenyewe pia ulivyojidharau kwa kujiita mtu wa mtaani, ptuu!!!
 
Back
Top Bottom