tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Mnaoshabikia ushindi wa Kenyatta, huku mkijua kwamba nchi ya Kenya ipo ndani ya EAC, sijui mnategemea nini? Fahamu kwamba Kenyatta ana kesi ya kujibu ICC na mataifa ya magharibi yalishatangaza kumpa kisogo endapo atashinda urais wa Kenya. Na pia mnapaswa kutambua kwamba ushindi wa Kenyatta umetokana na siasa za ukabila.
Kabila la wakikuyu ndilo kubwa kushinda yote nchini kenya, wakifuatiwa na makabila lukuki ya wakalenjin. Ushindi wa Kenyatta (kwa kutumia kete ya ukabila) ulionekana tangu zamani walipoungana na Ruto kutengeneza kundi moja la Jubilee. Ni wale wasojua ukweli kuhusu siasa za ukabila na ukanda za Kenya ndio wangeweza kudhani kwamba Odinga angeshinda.
Hata hivyo, Agwambo ameonesha ukomavu kwa kushinda kura kutoka karibu maeneo yote ya nchi bila kutegemea ukabila. Inabidi tukubali matokeo kama yalivyo kwani wakenya ndivyo walivyoamua lakini huu uamuzi wao utawa-cost. Watanyimwa misaada na wazungu hadi watakula majani! Kama wameshindwa kusoma alama za nyakati na badala yake wameamua kumuingiza mtuhumiwa ikulu, itakula kwao! Kibaya zaidi ni pale Kenyatta na Ruto watapohukumiwa kufungwa maisha au kunyongwa na ICC! Nchi itabaki bila rais wala makamo wake!
Kwa wale msofahamu vema siasa za Kenya, hebu ona kilichommmaliza odinga ni hiki hapa. Angalia idadi ya wapiga kura wa CENTRAL na RIFT VALLEY:
Region Voter Registration
Central
2,190,477
Coast
1,164,083
Eastern
1,988,475
Nairobi
1,778,903
North Eastern
451,865
Nyanza
1,954,756
Rift Valley
3,373,853
Western
1,434,987
Ni wazi kwamba Ruto ndiye alikuwa kete ya ushindi wa urais kwani mkoa wake wa wakalenjin (Rift Valley) una wapiga kura wa kumwaga. Na karibu nusu ya wapiga kura wametokea Rift valley na Central (the strongholds of the Ocamo two!). Kwa mtaji huu, hata kama Ruto angeamua kujiunga na Martha Karua, lazima Karua angetinga ikulu. Na sio Karua tu, hata angeamua kuungana na Peter Keneth, lazima tu angeshinda urais maana kinachoangaliwa hapo ni UKABILA tu wala sio SERA za mgombea au chama chake!
Wapiga kura ni wachache sana katika maeneo ambayo Odinga anaungwa mkono. Lakini hata hivyo Agwambo amejitahidi sana. Agwambo kubali matokeo muijenge Kenya yenu.
Viva Agwambo!
Haya na nyie watanzania mlokuwa mnashabikia siasa za Kenya (ambazo hazina faida yoyote kwenu), rudisha akili zenu nchini kwenu mkashughulikie matatizo yaliyoigukbika nchi yenu. Bado tatizo la kufeli kwa wanafunzi halijapata ufumbuzi. Pamoja na hili, kuna matatizo lukuki yanayolighubika taifa lenu kama vile majaribio ya kuuwawa kwa wandishi wa habari, Dr Ulimboka, nk. Yote haya ukichanganya na matatizo sugu ya UFISADI, yanatosha kuwafanya kila siku muwe mnatafakari kuhusu mstakabali wa taifa lenu. Sio kuacha kwenu kunaungua, mnakimbilia kwenda kushabikia ugomvi wa jirani usiowahusu. Rudisheni akili zenu nyumbani, nchi yenu ya kifisadi inataeketea! Tafakari, chukua hatua!