Barua ya wazi kwa Mbowe & CHADEMA: Kajipangeni Upya

Mbona hata katiba iliyopo Ina mazuri mengi ukiondoa ku I favor ccm madarakani ila changamoto ya hii nchi yetu Bado umaskini na sip katiba. Katiba inaweza kuwa nzuri bila mipango ya kukuza uchumi na umaskini hatutavuka sehemu. Kenya Wana katiba nzuri ila umaskini uko palepale
 
Hoja yao ni katiba mpya wanachotaka na wametoa mapendekezo ya kukaa meza ya mazungumzo kwani kuna ubaya gani kukaa pamoja kusikilizana mama akae nao watoke nanmsimamo hata kama mchakato utasicheleza wataweka roadmap uanze lini?
 
Kama wao sio UMMA Kuamini kwao haiatasaidia chochote .Kwa nini msiwapuuze tu?
Kwa sababu Chadema wanaamini wao ndio UMMA makundi mengine sio UMMA ndio maana wanadai Rais anatakiwa atekeleze matakwa ya UMMA (i.e. CHADEMA)[emoji23][emoji23]
 
Reactions: BAK
Kwa nini mnaizungumzia Chadema tu na sio ACT, TLP, NCCR au CUF ?

Kwasababu Chadema hawajui walitakalo kazi kudandia dandia tuu mambo , wanataka demokrasia lakini wao katika chama hawaongozwi kwa demokrasia, mfano halisi ni jinsi Mwenyekiti wa kudumu alivyokikalia chama kama vile hakuna wengine wa kuongoza.
 
Sawa , mkuu lakini kama nchi nafikiri kitendo cha kukifavor chama ambacho kinashika dola siyo kitu kizuri na nafikiri huchangia kwa asilimia nyingi katika kuleta ustawi wa nchi .

Kama chama dola kinapata favor nyingi hivyo nchi inakuwa na hatar ya kutopiga hatua katika maeneo mengi kwani chama kilicho ndo hupanga sera za maendeleo na mambo mengine. Na walio katika hicho chama ndo husimamia hizo sera , kwa kua favor ipo upande wao hata wasipo fanya kwa tija hamna linalo wagusa zaidi hufanya mambo kwa manufaa yao na ndiyo asili ya wanadamu tunapokuwa na privilege flani.

Hivyo bado kuna haja ya msingi saana ya kuwa na katiba mpya yenye mambo mengi katika maeneo mengi ya kiutawara, kisheria , kibinadamu na kiuchumi.
 
Hata Mungu mwenyew alipoona katiba yake ya agano la kale ina upungufu alibadilisha akaleta katiba mpya chini ya agano jipya na Yesu Kristo yenye misingi ya upendo, amani, utu , msamaha na ushirika. KamaMungu aliweza kubadilisha katiba sisi tunaogopa nini, ni swala la kukutana na kuweka roadmap
 
Naunga mkono hoja
 
Nakubaliana na wewe tena by 100% kuwa Mdude alionewa na naweza kukutafutia threads zangu humu JF nilizo paza sauti kuwa Mdude must be freed. Ila kwa sasa Mdude anaitaji likizo ya kuji rehabilitate mentally.

Kuhusu style ya CDM kuwa ni Static haibadiliki kadri ya Kiongozi aliyepo ndipo yanapoanza matatizo. CDM walim face Magufuli kwa jinsi ile ile waliyo mface Kikwette na matokeo waliyaona. Hayakuwa mazuri kwao. Kufa kwa Magufuli siyo ushindi kwa CDM, bado CCM iko vile.

Angalieni wananchi wanataka nini ambacho Serikali haiwapi ndicho mukifanye agenda yenu. Hivi kuna study/ research yeyote iliyofanyika na CHADEMA au chombo chochote na kuonyesha kuwa wananchi wanataka KATIBA kwa sasa?
 
UPUUZI MTUPU!!! Wewe ni nani nchi hii hadi UJIKWEZE kiasi hiki!? Miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi lakini bado tuna katiba ya chama kimoja!? Hili hulioni!!!!

 
Eti Rais ametupa uhuru tuutumie vizuri, Kumbe kuna watu hawajitambui mpaka sasa. Dah hatari sana
 
Reactions: BAK
Naunga mkono hoja
 
Sababu zilizotolewa na raisi zina mashiko, ndio kwanza ameingia madarakani ana vipa umbele vyengine. Na wakati huo huo yuko katikati ya covid crisis (janga la kiafya).

Ukitazama maneno ya raisi hajasema kama hatoshughulikia suala la katiba. Amesema watu wavute subra, nadhani anastahili kupewa muda kidogo. Binafsi mambo aliyoyafanya kwenye kusimamia haki na watu wasio na hatia kutolewa magerezani naunga mkono hoja apewe muda kidogo (kama mwaka ivi).

Janga la covid inshallah liko njiani kuisha.Kwenye nchi ambazo zinachanja na watu wake sio wabishi nadhani mwisho wa mwaka huu asilimia kubwa itakuwa ishachanjwa na watu washarudi kwenye hali za kawaida. Hivi naandika mataifa mengi yashaondoa utaratibu kama wa kuvaa barako, imebakia 1.5m ambayo huenda mwishoni ikaondoka pia na kurudi kwenye full turbo charge.
 
Wachukue hatua kwa post yako ambayo haioni udhalimu, dhuluma, wizi na ufisadi wa maccm kwa miaka 60 ya kuwepo madarakani katika nchi yenye utajiri mkubwa wa rasilimali lakini haina chochote kile cha kujivunia!? Hebu tia akili kichwani acha KUKURUPUKA na kuandika upumbavu!

Ni ushauri tu, siyo lazima ufuatwe. Ila wenye Kusoma between the lines wataelewa na kuchukua hatua
 
Hakuna watu waoga kuingia mtaani kama Watanzania. Alijaribu Mange Kimambi mwaka 2017/18 kuhamasisha maandamano kupitia Instagram hakuna hata mtu mmoja aliingia mtaani.

Baada ya uchaguzi wa 2020 ambao MAGUFULI aliuiba wote kupitia NEC na Polisi, Tundu Lissu aliitisha maandamano hakuna mtu alikwenda.

Urais ni Taasisi na siyo hivyo unavyochukulia wewe. Huyu unayemuona ni mwepesi kuliko MAGUFULI maamuzi yake yanaweza yakawa mabaya kuliko MAGUFULI.
 
Uko sahihi sana kinatakiwa Chadema kijitayarishe chama kinahitaji nini?vipaumbele vya chama na muono wa chama kwa miaka mitano ijayo.

Kuna upungufu mkubwa kwenye top leadership na mpaka uwe ndani ndio unafahamu upungufu. Chama siku zote hakiwezi kupata matokeo sahihi kama hakito tayarisha reli ambayo uongozi wote wa chama watapita hapo.
Na sio kweli kuwa Chadema ni chama cha wasomi, kwa kuwa hakitumii usomi kupata matokeo. Wasomi wanaonekana wanachelewesha matokeo, kumbe ni kinyume chake.

Mapito ya chama na uongozi ya miaka mitano iliyopita inatosha sana kuamsha ari ya mapambano kimkakati na kisomi. Majungu na mawazo ya kimtaa yanachukua nafasi kubwa kinyume na inavyotakiwa.
Sio muda mrefu tutaelewa mapungufu ya kiuongozi na kisera na yatakuwa bayana.
NCHI INAHITAJI CHAMA IMARA CHA UPINZANI CHENYE MIPANGILIO WA KUTOA MAJIBU YA KESHO KISIASA NA KIUCHUMI, LEO SIO YETU UPINZANI, TUNAHITAJI KUJIPANGA KWANZA .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…