Barua ya wazi kwa Mbowe & CHADEMA: Kajipangeni Upya

Utapanuka moyo kisa Chadema kunywa maji mengi
 
Badala ya kutushawishi kwa sera nzuri wanalilia katiba, kwa hiyo wao tukiwapa nchi kipaumbele chao ni katiba mpya, mambo ya ustawi wa nchi tutapambana wenyewe.
Hawa watu hawana agenda ya kukomboa raia wao katiba tu, hivi tutawapaje nchi wameacha matatizo yanayo wagusa wananchi direct.
 
Mkuu kwa bangi wanazovuta -sijui kama watakusikiliza
 
Mithali 26:4. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye.

Tuishie hapo
 

Ndugu, kuna kitu kinaitwa "majira ya nyakati"

Nakupa neno moja hili:

Mama Samia Suluhu Hassan ndiye Rais wa kwanza Mwanamke Tanzania lakini ndiye atakuwa Rais wa mwisho toka CCM kutawala/kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huyu ndiye anatengeneza lango la kutokea na kupotea kwa Chama Cha Mapinduzi - CCM..

Asomaye na afahamu...
 
Wakipewa uhuru wanautumia vibaya, wakibwana mbavu wanalialia...
 
Sioni tatizo Chama kingine kutawala Tanzania kwa vile vyama vyote vinatambuliwa kwa mujibu wa Katiba ya JMT ya mwaka 1977 toleo la 1000 na Sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 1992 . Hata CCM hawana HATIMILIKI ya kutawala milele.
 
Hakuna mtu amewahi kuishinda dola. Hivi anavyosema hawabembelezi maana yake anamtishia Rais?? Nina amini kwa hulka ya Rais atakutana nao kama alivyoahidi lakini siyo kwa mashinikizo ya kijinga kama hayo ya Mbowe.
 
Now unataka kuwafundisha Chadema kulegeza sauti wakiwa wanadai haki zao, kwanini huu muda mnaotumia kuhangaika na Chadema msiutumie kuwaamsha watawala waliolala usingizi wanakandamiza haki za raia ili hao Chadema wasiendelee kupoteza muda kuwakera kwa namna wanavyodai haki zao?

Mnatakiwa ku deal na chanzo cha tatizo sio njia inayotumiwa kutatua tatizo, wake up.
 
Na Kuna study gani imefanywa kuonesha wananchi hawataki katiba mpya kwa sasa??
 
Asante kwa mawazo chanya. Busara inahitajika sana kuliko HARAKATI. Wananchi wanamuelewa Rais Samia sana kuliko hicho ambacho CDM wanataka kusema ni cha muhimu kuliko kupanga uchumi
Nchi hii isha ingia uchumi wa Kati huo uchumi ambao Mama anataka kujenga ni uchumi gani?
 
Na Kuna study gani imefanywa kuonesha wananchi hawataki katiba mpya kwa sasa??
Nimeuliza swali kuwa "iko wapi study/ research inayoonyesha kuwa wananchi wanataka Katiba Mpya?"

Wewe Kinkunti El Perdedo unastahili kunijibu na siyo kuniuliza swali mimi muulizaji. Hivi kweli wewe ulifaulu NECTA?
 
Kana kwamba haitoshi mama ameshasema anakubari kukosolewa ila iwe kwa staha sio matusi na zarau akiona kweri kakosea atatoka hadharani na kuomba radhi. Mdude nani hata atukane jukwaani ni anyamaziwe tu
 
CDM wamezingua huu ndio ukweli, acheni matusi, mwambieni huyo chairman awe na busara, hamna mtz atamuelewa, na huyo kichaa aliyetoka jela awe mpole, kuna njia nyingi tu za kudai katiba
 

Mkuu pana mambo ya msingi kuyaona kuweza kuelewa hali ya uwanja ilivyo:



Picha hiyo inajieleza wazi.

Pana nia na mwendelezo wa kumfarakanisha Mama na yeyote (hasa Chadema) kwa lolote hata kama ni la kijinga. Uzi huu una husika:


Hata chokochoko za kumfarakanisha Mama kwenye bandari ya bagamoyo ziko kwenye mlolongo huo huo.

Mama kazungukwa na wahafidhina wa CCM kama unavyowaona wengine humu mitandaoni. Hawa ni wanufaika wa katiba iliyopo. Zao ni kukaanga mbuyu tu kwa heri au kwa shari (zikiwamo hata kuishauri Chadema). Ali mradi tu zao kukaanga mbuyu:


Kwa dhamira ya wahafidhina hao Chadema hata wafanyeje hawatakaa kukutana mezani na mama kwa mazungumzo yoyote bila ya msukumo wao wenyewe tena wa dhati kweli kweli.

Itambulike kuwa wahafidhina hawa na CCM ni wahanga wa katiba mpya. Hawana cha kupata bali vya kupoteza. Ni vipi bado waridhie hayo kwa namna yoyote?

Asilaumiwe Mbowe wala CHADEMA, kaniki ni rangi yake!

Cc: BAK Extrovert Pascal Mayalla Missile of the Nation jingalao Idugunde
 
Kwa nini mnaizungumzia Chadema tu na sio ACT, TLP, NCCR au CUF ?


Mkuu ngoma iko hapo. Zaidi sana:


Haipo nia njema ya maridhiano bali mifarakano.
 
Ushauri mzuri sana uliwapa, ila wakaupuuza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…