Barua ya wazi kwa Mhe. Waziri wa nchi ofisi ya raisi (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa

Barua ya wazi kwa Mhe. Waziri wa nchi ofisi ya raisi (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa

Rightman

Member
Joined
Apr 30, 2015
Posts
15
Reaction score
7
YAH: MADAI MBALIMBALI YAKIWEMO POSHO YA KUJIKIMU WATUMISHI AJIRA MPYA, MALIPO YA LIKIZO NA MALIPO YA SAFARI ZA KIKAZI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA

Mhe Waziri wa TAMISEMI, kumekuwa na changamoto na usumbufu mkubwa sana juu ya stahiki mbalimbali za watumishi katika Halmashauri ya Ngara iliyopo katika Mkoa wa Kagera.

Watumishi wengi wamekuwa wahanga wa kwenda likizo bila kulipwa stahiki zao na kumekuwa na usumbufu mkubwa sana katika kuzifuatilia, pia watumishi wengi katika Halmashauri hiyo wanasafiri kikazi ndani au nje ya Mkoa bila malipo, Watumishi wanaamua kujikopa wakijua stahiki zao za kujikimu zitalipwa wakiwa safarini au wakirudi kutoka safari ila usumbufu unakuwa mwingi sana kuzipata kitu kinacholeta wasiwasi endapo siku nyingine atatakiwa kusafiri tena kikazi.

Aidha ni karibu mwaka mmoja kufikia sasa baadhi ya watumishi wa Ajira mpya mpaka sasa mfano Idara ya Kilimo na Mifugo, Idara ya Maendeleo Jamii n.k wameendelea kuwa wahanga wa kutolipwa fedha zao za kujikimu kinyume na maelekezo uliyoyatoa. Fedha za uendeshaji wa Idara (OC) zinatoka ila wakuu wa Idara na Vitengo wanazielekeza katika vipaumbele vyao na kujiandikia posho bila kujali maslai ya watumishi walio chini yao, ilhali ya jitihada mbalimbali za watumishi wanaodai kukumbushia madai yao ila hayasikilizwi na hakuna jitihada chanya zinazooneshwa na viongozi wao kuzitekeleza.

Kwa sasa Halmashauri hiyo imeendelea kupokea watumishi wapya ambao bila juhudi basi wataendelea kuwa wahanga wa kutolipwa stahiki zao zaidi ya miaka kama viongozi wa Halmashauri hawatobadilika. Hivyo kupitia barua hii ya wazi kwako Mh. Waziri tunakuomba ukemee mapungufu hayo katika Halmashauri hiyo na Halmashauri nyingine zitakazobainika.
 
Back
Top Bottom