KING ASSENGA
JF-Expert Member
- Oct 8, 2016
- 928
- 1,478
Salaam na heshima kwako mheshimiwa Boniface Jacobo Mayor mstaafu na Mwenyekiti wa Kanda ya pwani chama Cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Kiongozi kabla ya kusema niliyowiwa kuyasema naomba kutambua unao washauri wengi sana wenye vyeo na nafasi kubwa kuliko Mimi ila naomba unipe dakika chache tu kusoma barua hii.
Kiongozi kabla ya uchaguzi mkuu wa chama ulikuwa mtu muhimu sana katika chama na nikiri huo umuhimu wako upo , pengo lako tunaliona ndio maana nimewiwa kuandika barua hii ya wazi kwako .
Kiongozi Kuna matukio mengi sana yametokea nchini ambayo sio kawaida tukose tweet mbili tatu kuyahusu na kuna matukio mengi sana ya kichama ambayo hatukuoni wala kuona mchango wako kwa sasa
Kiongozi naomba nikukumbushe tukio la wewe kurudisha fomu ya kugombea uenyekiti Kanda ya pwani. Wanachama wengi tulikusindikiza kurudisha fomu wengine hata hutufahamu na usisahau hatukukusindikiza kwa sababu ya ukaribu wako na Mbowe tambua hili Kuna wengi tu walipendezwa na Lissu wakati wa uchaguzi na walikuwa wengi tu huenda zaidi ya wafuasi wa mbowe waliokusindikiza . Hivyo tambua tunaokuamini hatukuamini kwasababu yoyote zaidi ya kuwa mwanachama wa chadema na mwenye uwezo mkubwa katika harakati za chama .
Tunatambua umeumia sana kutokana na demokrasia ilivyoamua ila fikiria vizuri sidhani kama mheshimiwa Mbowe anafurahia ukimya wako . Tafadhali ni muda wa kurudi sasa. Tusamehe tuliotoa maneno makali wakati wa uchaguzi wa chama nikiwemo umeniblock kabisa. Uchaguzi umekwisha . Ushapumzika vya kutosha . Pengo lako linakusubiri ulizibe Tafadhali lizibe tusonge mbele.
Nisikuchoshe kwa barua ndefu. Tafadhali rudi kama awali maisha yaendelee
Mwanachama mtiifu wa CHADEMA
Na mwanaharakati wa haki
Assenga
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025