Barua ya wazi kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba

Barua ya wazi kwa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba

Akimaliza kuota atakuja kutuambia vizuri
Mazuzu yasiyosoma habari utayajua tu. Majitu majinga, upumbavu umewajaa.

Wenye Akili na weledi wanawacheka jinsi mlivyo vichwa maji.

NB:Kama hujasoma habari yote kwanini una comment?
 
Kwahiyo unataka mechi nzima simba ndo wawe na mpira??

Unaleta hisia kwenye game, utajiua shauri yako
SOMA kwa kuelewa.

Halafu Jaribu kuuelewa mpira. Utaelewa mantiki ya kilichoongelewa.

Tutoe tahadhari mapema,kabla ubingwa haujaenda Halafu tutafute mchawi.
 
Ukikua utaacha ujinga
Kati yangu na wewe Nan mjinga. Tena WEWE ndiyo mpumbavu unaesoma page Moja na huambulii kitu.

Hahahaaaa mazuzu mko wengi Sana asee. Pole mkuu kwa ujinga!

SOMA Tena mpaka mwisho halaf utajiona mjinga!
 
Ulikuwa ume "hibernate"?
Hahahaaaa FRIEND OF DP WORLD. NAKUSALIMU KWA JINA LA DUBAI!

Aliye hibernate Ni mm au Ni ww.Sababu km umesoma mpaka mwisho usingevaa mask ya kuziba macho.

Kwasababu wewe Ni rafiki nitakuelewesha. Hiyo Ni post toka maktaba.

Pale mwisho kwenye NB. Nimeeleza Kwamba Ni post ambayo niliihifadhi na sikupunguza Wala kuongeza neno. Nimeipost km ilivyo.

Na si post yangu.nimeacha na jina la mwandishi km lilivyo.
 
Kuhusu kutojituma uwanjani simba wanao sana huu utamaduni na uto wameliona hili,tukikutana nao unaona kabisa juhudi wanayofanya,tuna wachezaji mafaza ambao uchezaji wao si kashkashi.
 
Angalia mechi kubwa km ile yajuzi ngao ya jamii. Yanga wako nje ya 18 Simba wanakaba kwa macho. Mipira ya juu tuliiwini kiasi gani. Angalia uto wanavyojituma. Wanacheza JIHAD. Nb: Mechi yaSimba na Dodoma Jiji , ukweli MCHUNGU , wangekuwa Ni Gongowazi wangeshinda hata goli 8. Mashambuli ya mpinzani 80% lazima yafike langoni mwa Simba. Na wako huru kupiga Kristi nk
Kuna kila dalili kwamba hukujipanga kuanzisha uzi
 
BARUA YA WAZI KWA MTENDAJI MKUU WA KLABU YA SIMBA

Kwako Barbara Gonzalez
Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba.

Kwa heshima kubwa nakuandikia barua hii nikiwa na uchungu na masikitiko makubwa sana kutokana na makosa yanayojirudiarudia kwa wachezaji wa Simba wanapokuwa uwanjani.

Nianze kwa kuuliza swali;- Hivi Klabu ya Simba haina mtaalam wa kuchambua mechi na kuchambua utendaji wa wachezaji yaani Match and Player Performance Analyst? Kama yupo mbona hazionekani athari chanya( Positive Impact) kwa wachezaji mmoja mmoja na timu kwa ujumla?

Ukiziangalia mechi nyingi zilizochezwa na Klabu ya Simba, utagundua kuna maradhi ambayo yapo kwa wachezaji wa Simba, ambayo ni maradhi ya muda mrefu sana yanaweza yakawa sugu yasipotafutiwa ufumbuzi wa kudumu.

Maradhi ambayo wanayo wachezaji wa Klabu ya Simba ni UKOSEFU WA MOYO WA KUIPAMBANIA/KUIPIGANIA TIMU (LACK OF FIGHTING SPIRIT FOR THE TEAM). Wachezaji wetu wakiwa uwanjani hawajitoi 100% kwa ajili ya timu kupata matokeo ya ushindi ingawa wanacheza vizuri. Unajua unaweza ukacheza vizuri na usipate matokeo ya ushindi kwa kuwa haupambani kwa ajili ya kushinda. Kila mchezaji katika nafasi yake anacheza kutimiza WAJIBU wake kwenye hiyo nafasi, lakini ifahamike kuwa katika kutimiza WAJIBU kunatakiwa kuwa na kitu cha ziada kwa mtu anayetimiza huo WAJIBU ili aweza kutimiza WAJIBU kwa kwa muda sahihi, kwa ufanisi na kwa uhakika.

MIFANO HALISI;-
Mfano wa kwanza:
Pitia mechi kadhaa za Simba za ndani na nje kisha angalia kwa umakini wachezaji wanapokosa goli, wengi wao hawaoneshi kuumizwa kwa kupoteza hiyo nafasi ya kufunga ni kama vile wanaamini watafunga tu.

Mfano wa pili:
Pitia mechi kadhaa za Simba za ndani na nje kisha angalia kwa umakini wachezaji wanapokuwa mmoja dhidi ya mmoja (ONE VS ONE) katika kuwania mpira wa mguuni na opponet wake, mara nyingi wachezaji wa Simba wanapoteza mpira na kumuacha mchezaji pinzani (OPPONET) kutembea na mpira huku anamsindikiza tu kwa macho.

Mfano wa Tatu:
Pitia mechi kadhaa za Simba za ndani na nje kisha angalia kwa umakini wachezaji wa Simba wanapokuwa wanawania mipira ya juu dhidi ya mpinzani wake, mara nyingi wachezaji wa Simba wanapoteza na mpinzani anafanikiwa kuucheza.

Halikadhalika, uchezaji wa timu ya Simba unaruhusu sana wachezaji wa timu pinzani kuwa huru katika kufanya maamuzi sahihi wanapokuwa na mpira. Wanaruhusu mchezaji wa timu pinzani kukokota mpira akisindikizwa tu na mchezaji wa Simba. Wanasubiria opponet mwenye mpira aidha afanye makosa miguuni mwake aua apige pasi yenye makosa. Hii ni mbaya sana maana inasababisha mashambulizi yasiyo ya lazima na kumfanya mpinzani awe huru kupanga mashambulizi mara kwa mara.

Ni ukweli usiopingika, Timu ya Simba ina wachezaji wazuri sana na imefanya usajili mzuri sana, tena imesajili wachezaji wenye kasi sana lakini kasi yao haionekani. Hii ni kutokana na MFUMO unaotumika na makocha wengi wa Simba.

USHAURI
Wachezaji wa Simba wanahitaji mtaalamu anayeweza kuwatengeneza kisaikologia ili wawe na ari na roho ya kuipambania timu(Fighting Spirit for the team). Wanahitaji mtu ambaye anauwezo wa kuipitia mechi iliyokwishachezwa na kuzungumza na wachezaji maeneo wanayotakiwa kuyafanyia marekebisho kwa pamoja na kwa mmoja mmoja(Collectively and individually). Hivyo Klabu haina budi kufanyia kazi eneo Hilo.

SIMBA NGUVU MOJA

Edwin RZK
Mdau wa Maendeleo ya Soka
TANZANIA


Nb: Hii post niliihifadhi. Sijaongeza Wala kupunguza herufi
Mm Ni utopolo makini ila mtendaji mkuu wa sc Ni iman kajura

Huyu wa Sasa umemtoa wapi bwana mkuu
 
Back
Top Bottom