Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
YAH: Upendeleo wa wazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika uchaguzi mkuu huu na kutumika kuwanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa
Ndugu Mwenyekiti,
wakati Taifa lingali likiendelea na mchakato wa uchaguzi kuelekea katika tarehe yenyewe ya tukio la kupiga kura tarehe 28 October 2020, kwa bahati mbaya kumekuwepo na matendo ambayo yanaashiria kuwa tume yako haiko fair, na wala haizingatii sheria za nchi, na hapa nitaeleza machache:
1. Mkurugenzi wako ameonyesha mahaba na mapenzi ya dhahiri kwa chama tawala kinyume cha maadili ya kazi yake na NEC haijamkemea
Kwa mfano, mkurugenzi wa NEC badala ya kusimamia shughuli za NEC yeye amejiingiza katika malumbano ya kisiasa kwa kunadi ilani mbadala ambazo pengine ni kinyume cha Ilani za vyama kadhaa vinavyoshiriki uchaguzi, ameonekana akipiga vijembe sera za vyama vingine katika issue kama za madini na hivyo kujenga taswira mbele ya umma kuwa vyama hivyo vinataka kutapanya utajiri kwa wageni na hivyo Mkurugenzi huyo kuitumia NEC kupitisha ajenda zake za kisiasa ambazo tunajua kuwa ni kada mtiifu na mwaminifu sana wa CCM. Hili jambo siyo sawa na nakuomba wewe kama mwenyekiti wa Tume ukemee hili na ulitolee ufafanuzi ili kurudisha imani ya wananchi kwa tume.
Ndugu Mwenyekiti, kama kweli mkurugenzi wa NEC anaamini kweli kuwa watanzania wanahitaji maji na vitu mbalimbali alivyovitaja, kwa nini basi Yeye au NEC haijatoa tamko kuhusu mgombea wa CCM ndugu Magufuli aliyetishia wazi kabisa kuwanyima wananchi maji iwapo watatumia uhuru wao wa kikatiba kuchagua wamtakaye hata kama mtu huyo siyo wa mrengo autakao Magufuli? - Mahera yuko wapi kukemea hili yeye si ndo alisema watanzania wanataka maji?
2. Kitendo cha Mkurugenzi wa NEC ndugu Mahera kutangaza rasmi kuanza kupiga wagombea urais mabomu ni kinyume cha sheria na ni kitendo cha uchochezi na kinaweza kupelekea kuvurugika kwa amani na kuharibu uchaguzi
Kisheria NEC haina mamlaka za kuamuru watu wapigwe mabomu, kazi ya NEC ni kusimamia uchaguzi. Na kwa mujibu wa sheria, Kuna chombo cha kudeal na masuala yote ya maadili ya uchaguzi iwapo mgombea anayavunja, na miongoni mwa taratibu zilizowekwa kisheria ni walalamikaji ikiwemo Wagombea, Serikali, Msajili wa vyama au hata Tume yenyewe kuandika barua rasmi ya malamiko juu ya mwenendo wa mgombea fulani na kisha masuala hayo kutolewa maamuzi. Siyo jukumu la polisi kujichukulia sheria mkononi na kuanza kuenforce "maadili" ya uchaguzi bila masuala hayo kwanza kulalamikiwa rasmi, maana tukifanya hayo tutaenda kupiga wananchi mabomu bure na kuumiza wananchi huku tukivunja sheria. Nakuomba wewe Mwenyekiti wa NEC umtake mkurugenzi atii sheria bila shuruti maana siyo yeye, wala NEC wala jeshi la polisi walio juu ya sheria.
3. Mgombea wa CCM ndugu Magufuli anaendesha kampeni za ubaguzi, kugawa watu na kublackmail wananchi
Ndugu Mwenyekiti, Katiba ya nchi imewapa wananchi haki ya kuvhagua na kuchaguliwa, na imepiga marufuku ubaguzi kwenye kuhudumia wananchi. Leo hii mgombea wa CCM badala ya kunadi sera, yeye anawatisha wananchi kuwa atawabagua wakitumia haki yao ya kikatiba. Wakati haya yanafanyika, tume inaona, inasikia na pia nayo ina mamlaka za kufuata utaratibu maalum wa kukemea mwenendo wa wagombea, lakini tume imekuwa ikiandama wapinzani tu hususan mheshimiwa Tundu Lissu huku ikimuacha Magufuli akitoa matamshi ya kuwagawa wananchi na kutishia kuvuruga umoja, amani na mshikamano wa kitaifa. Hili jambo siyo sawa na NEC ijisahihishe na imuite ndugu Magufuli kwenye kamati au mamlaka za maadili ahojiwe na apewe karipio kali.
4. NEC inavumilia uvunjifu wa sheria unaofanywa na Kassim Majaliwa
Sheria ya NEC inasema, chombo chenye mamlaka ya kupanga ratiba za kampeni ni NEC, na Tumeona NEC ikitoa ratiba za wagombea urais, ratiba zenye kueleza vituo vya wagombea urais na mgombea mwenza, Lakini NEC haikutoa Ratiba kwa mtu yeyote mwingine kwenye ngazi hizo akiwemo hata waziri mkuu, Nashangaa Waziri Mkuu anazunguuka nchi nzima kupiga kampeni za urais kwa niaba ya Magufuli kinyume cha ratiba za NEC lakini cha ajabu NEC yenyewe haimuonyi wala kumkataza uvunjifu wa wazi wa sheria za nchi.
Ndugu Mwenyekiti nakuomba umkemeee kwa nguvu zote ndugu Majaliwa, aache uvunjifu huu wa sheria la sivyo sheria ichukue mkondo dhidi yake maana anavuruga uchaguzi.
5. Tume haikemei Jeshi la Polisi kuonea wapinzani
Tumeona majuzi, Msafara wa mheshimiwa Lissu na msafara mwingine wa mgombea mwenza wake ukipigwa mabomu kwa hoja za kufanya kampeni katika vituo visivyo rasmi, Wakati huohuo mhombea mwenza wa CCM na Mgombea urais wa CCM wamekuwa wakifanya kampeni njiani lakini hawajapigwa mabomu, na sheria ya uchaguzi inataka vyombo vya dola visiwe na upendeleo au kuhujumu mchakato wa uchaguzi kwa kukipendelea chama fulani.
Ndugu Mwenyekiti, NEC yako haijalikemea jeshi la polisi kwa kufanya kazi kwa upendeleo dhahiri dhidi ya wagombea wa upinzani, kuendelea na utaratibu huu ni kutufanya sisi wananchi tukose imani na chombo chako
Nakuomba kama mwananchi mwenye kulipenda taifa lake, Chombo chako cha NEC kiwe fair, na kisimamie sheria na kiwachukulie hatua kali za kinidhamu watumishi wake wenye kuacha kufanya kazi kwa maadilinya viapo vyao na kuanza kuonyesha ukada na upendeleo wa dhahiri kwa chama cha mrengo fulani kama tulivyoona hivi karibuni Mkurugenzi wa NEC ndugu Mahera anavyofanya.
6. Kutopitia kwa haraka rufaa za wagombea ubunge na udiwani na wengine kuwaengua bila sababu za msingi
Ndugu Mwenyekiti, katika haki za msingi ambazo katiba imetoa kwa wananchi ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa, leo hii ni mwezi mmoja wa kampeni umeshapita, tume inaenda kwa mwendo wa kinyonga kwenye kupitia rufaa za wagombea wa udiwani na ubunge, Na wengine tume imewaengua bila hoja za msingi kabisa katika kinachoonekana dhahiri kukipendelea chama cha Mapinduzi, hii ni aibu kubwa mno kwa tume ambayo imesheheni watu wa sheria, Ndugu Mwenyekiti najiuliza kwa nini tume isiilinde haki hii ya kuchagua na kuchaguliwa ya wananchi kwa wivu mkubwa?, Yaani tume inaridhika kuona maelfu ya wananchi wanakosa haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa sababu ya vitu vidogovidogo kama "typo", Scrivener's errors na vitu ambavyo kimsingi hasa havibatilishi uhalali wa kisheria wa document?, Ndugu mwenyekiti nina wasiwasi Makada wa CCM wameiteka NEC, na nakuomba utumie influence yako hii kuzuia mchezo huu wa kuwanyima wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haki yao kuu ya kikatiba. Hii haki inabidi ilindwe kwa nguvu zote, Haimake sense hata kidogo eti chombo kilichopewa jukumu hili kikatiba chenyewe ndiyo kiwe chombo namba moja kushiriki kuwanyima wananchi haki hii. Hii haiko sawasawa!
Wako katika ujenzi wa Taifa