Barua ya wazi kwa ndugu, jamaa na watanzania kwa ujumla baada ya kupata vitisho vya kuniteka, kuniuwa na kunipoteza

Ben saa8 ilikuwaje????
Nae alikuwa anaongea hivi hivi kuwa anatishwa.
So mwache mdude achukue tahadhari.
Ndio maana nikasema huyu anajua ana wajinga wengi humu mitandaoni, ndio maana kila anapoamka anafikiria kuandika lolote akijua kuwa kuna wajinga wataungana nae.

So hebu fikiria kuwa na wew upo katika kundi la wajinga wake anaejua kuwa watakubali chochote atachoandika, au upo kwenye kundi la watu makini kama mimi ambao tunaamini mtu mwenye nia ya kukuua hawezi kukupa taarifa ya nia yake maana anajua utapopata taarifa utakuwa makini na lengo lake la kukuua litafeli.

Ben na yeye alitaka kutumia siasa uchwara kama huyu kwa kujifanya anatafutwa auawe, matokeo yake watu wengine wanatumia fursa hiyo kummaliza kwa kujua kwamba jumba bovu litawaangukia wale waliokuwa wanatajwa na marehem.

Unaweza kugombana na mtu ukamwambia kwa hasira kuwa popote nitapokuona nita deal na wewe. Wakati wewe umeongea pengine kwa hasira bila kumaanisha, lkn hapo hapo wanaweza kutokea wabaya wake na yule uliegombana nae wakatumia maneno yako kama fursa ya wao kufanya mauaji yake wakiamini kuwa kesi ya mauaji utakuangukia wewe ulieahidi ku deal nae popote utapokutana nae.

Ndiomaana wenye akili tunaamini kuwa muuaji anaekuwinda akuue huwa hakupi taarifa. Bali hukuvizia kimya kimya ili iwe rahisi kukupata na kukumaliza bila wewe mwenyew kujua kama ulikuwa unawindwa uuwawe. Nafikiri uliona mzee Kibao alivyotafutwa kimya kimya na kumalizwa kimya kimya bila yeye mwenyewe wala familia yake kuwa na taarifa yoyote.
 
Hata kwa jpm mambo yalianza hivi hivi.

Tunaamini kwa Hakika Hutakufa bali Utaishi.

Ameen
 
Kiburi cba uzima hiki ndugu yangu. Walikuwepo wababe zaidi Yenu.

Yesu Kristo ndio Mbabe Pekee Mbinguni na Duniani.

Mrudieni Bwa a wa Majeshi uziponye roho zako na kizazi chako.
 
umefanya vyema...ova
 
Kiburi cba uzima hiki ndugu yangu. Walikuwepo wababe zaidi Yenu.

Yesu Kristo ndio Mbabe Pekee Mbinguni na Duniani.

Mrudieni Bwa a wa Majeshi uziponye roho zako na kizazi chako.
Nimrudie mimi au tumrudie wote, una uhakika gani kama wewe hapo ulipo hauna dhambi?

Moyo wa mtu ni msitu nikimaanisha hakuna anaejua kilichopo ndani ya moyo wa mwenzake. Ndomaana mwaka 2008 kuna mtu aliamka asubuhi akaja na story ya Lowasa fisadi, akiamini kuwa kuna wajinga na wapumbavu kibao wataamini kile alichosema.

Na kweli kama ilivyo ada wajinga na wapumbavu huwa hawakosekani duniani, jamaa akapata kundi kubwa nyuma yake haswa kupitia chama chake. Wakaanza kumuandama mzee wa watu kwa kila anachofanya mpaka kumfanya akose raha na amani ya kuishi nchini kwake na duniani kwa ujumla ilimradi tu wao watimize lengo lao la kisiasa, aonekane hana maana na hafai kuwa kiongozi yeyote wa nchi hii.

Mungu huyu huyu unaesema hapa sio John, Hamisi wala Athumani mwaka 2015 akaamua kuwaumbua kwa kumleta Lowasa katika chama chao, ili waliotengeneza uongo ule kupitia midomo yao, waweze kumsafisha wao wenyewe na kuukanusha uongo wao kwa kupitia njia ile ile ya midomo yao. Alieleta uongo na wenzake wakakiri kuwa Lowasa hakuwa fisadi bali walitumia strategy ya kisaisa kumchafua ili kupata kundi kubwa la wajinga kama wewe nyuma yao.

Sasa wewe unaweza kufanywa mjinga na mpumbavu na wanasiasa ili kukufanya uwasaidie kufikia malengo yao, lakini mimi sipo tayari kufanywa mjinga na kukimbilia kuamini kauli zozote zinazotengenezwa na hawa wanasiasa na wanaharakati uchwara wa Tanzania. Wote ni waongo na wanatumia ujinga na upumbavu wa baadhi ya watanzania kufanikisha uongo wao.

Narudia tena, hakuna mtu anaetaka kumuua adui yake alaf akimbilie kumpa kwanza taarifa mapema, huyo atakuwa hana nia ya kumuua. Hata mwizi akitaka kukuibia huwa hakupi taarifa kuwa atakuibia, itakuwa muuaji!!

Na kweli katika sekeseke kama hili kuna wale maadui wa pembeni ambao hujitokeza kufanya mauaji au kujeruhi, wakoamini kwamba zigo la lawama litawaangukia wale waliotajwa na mleta mada hapa JF.

Endelea kufanywa mjinga ndugu yangu na wanasiasa uchwara ambao hata watoto wao hawakutambui kama wewe ni mjinga wa baba yao, mjomba wao nk.
 
Nimesoma vizuri na kuelewa andiko lako nataka niseme chochote lkn Kuna kitu kinaniambia nitofautishe akili zangu na za aliyeandika binadamu wote tuna matatizo ya kichwa lkn tunatofautiana Kwa kweli ngoja nipite.
 
Huwa huna cha kufanya ,tangu 2014 wewe ni kutukana watu hata walikuuwa sisi hatuna tulichobakisha kwenye kuonya na kushauri.

Umemtukana ana Samia leo unalialia tena na huyu Samia alijutia jela

USSR
Kuandika tu hujui sijui unafanya nini humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…