Barua ya wazi kwa Paul Makonda

Barua ya wazi kwa Paul Makonda

Sasa nyie na kiki zenu za kitoto tuwaeleweje?
Mashoga nao niwadamu kama ninyi.Ushoga ni ulemavu Maanayake kunawatu wamelemaa hadi sura zimeishaenda huko.
Sasa mnaitisha kampeini hili hiweje? mkiwakamata mnawafunga je mnamagereza yakutosha?

TUNAHITAJI KATIBA ITAKAYOZITAMBUA SHERIA ZA DINI
Mkuu katiba tunayo tayari inayopinga masuala hayo na ndio maana Mh Paul Makonda akaanzisha hiyo kampeni.

Iliwapasa viongozi wote na serikali kiujumla imuunge mkono
 
Anapofeli Bashite,ni Approach ya hayo matatizo, niamini waliopiga kelele wengi walimpigia kisa Approach yake.
Huwezi tetea haki kwa kuvunja haki ya Wengine..utaratibu wa kutaja majina hovyo na vitu kama hivyo ilikua ji tatizo.
Haki ya mmoja inaishia inapoanza ya mwingine.
USHOGA NI USHETANI, wala tusipepese macho.
Kabisa kabisa. Ndio maana nkasema ni approach zilizotumika katika zile kampeni ndio hazikuwa sahihi
 
Mkuu,

Pole kwa majukumu na changamoto za uongozi.

Kwanza naomba ku-declare interest: Mimi ni kijana wa kiislam ambae Nina uelewa kiasi juu ya Uislam.

Hivi karibuni ulidhamiria kufanya kampeni ya kulisafisha jiji la Dar as salaam kuhusu suala zima la watu wanaojihusisha/wanaofanya mapenzi ya jinsia moja (mashoga). Napenda nikuhakikishie kuwa, ndani ya mioyo ya Watanzania wenye busara na akili na wenye kuitakia mema nchi yao ulipata uungwaji mkono wa hali ya juu. Mimi binafsi nilikaa nikawa nakuombea kwa Mungu akupe ujasiri wa kulifanikisha suala lile.

Mkuu, nataka nikuhakikishie na kukufariji kwamba wapo watu wakubwa na wenye busara zao ambao wanajua kwamba ulikuwa sahihi kuanzisha kampeni ile, sitaki kuwazungumzia maana mimi sio msemaji wao rasmi lakini amini usiamini kwamba kuanzia Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa, Mheshimiwa Said Kubenea, Mheshimiwa Zitto Kabwe, Dk Bashir Ally, Baraza la wawakilishi la Zanzibar na kama sisi hohehahe tulikuwa pamoja na wewe.

Mkuu, suala hili lilikuwa na sura mbili na ni bahati mbaya sana kwamba umma wa wanasiasa wakalifanya ni suala la kisiasa. Wanasiasa hao walikuwa wakikuunga mkono ndani ya mioyo yao lakini kwa sababu hawakutaka kuwakasirisha ma-boss wao wakajitoa akili zao, wakajifanya hamnazo, wakakupinga au wakafurahia pale ulipopingwa hadharani.

Mkuu, katika suala hili la ushoga ujasiri wako hautosahaulika kamwe na Mimi binafsi mungu akinipa umri nitakuja kuhadithia ujasiri huu wajukuu zangu. Vile vile hatutakaa tuusahau ukasuku na unafiki wa wale waliokupinga katika hili, hatuna vya kuwafanya tunawatazama tu ila kiukweli thamani yao kwetu imeshuka.

Mkuu, kwa vile msingi mkubwa wa barua hii ni suala hili la ushoga, naomba tuishie katika suala hili japo zipo kampeni zako nyengine nyingi tu ambazo binafsi nilizikubali sana ila sikukubali njia ulizotumia kwenye kampeni hizo. Kampeni ya madawa ya kulevya, kampeni ya kutetea wanawake/ watoto waliotelekezwa na nyenginezo zilikuwa ni kampeni zenye nia njema lakini njia zilizotumika kufanya kampeni hizo nadhani hazikuwa sahihi. Kama hivyo ndivyo, basi nadhani ipo haja ukaangalia upya timu ya washauri wako.

Najua watatokea watakaonipinga, kunikebehi na kunitukana lakini Mwenyezi Mungu mtukufu kwenye kitabu chake cha qur an anasema " wala msichanganye haki na batili, mkaificha haki na hali mnajua (Qur an 2:42)" na Mimi nimeamua kukukumbusha na kukupongeza juu ya msimamo wako uliouchukua juu ya suala hili.

Mkuu, hata kama nchi hii haina dini, na msingi wa taratibu na kanuni za maisha ya Watanzania ni katiba zao, basi sihitaji kukukumbusha kuwa hiyo katiba ambayo wale waliokupinga "WALIAPA" kuilinda na kuitetea basi inakataa mambo ya ushoga ndani ya nchi hii ambayo mmoja wa waasisi wake alitangazwa kuwa "MTAKATIFU".

Kuna mengi ya kusema lakini kwa Leo naomba niishie hapa ili nikaribishe matusi na kejeli za wale wote wanaotetea ushoga.

Relief Mirzska.
siku moja akiungwa mkono na wenye nguvu hizi harakati zake basi moja kwa moja watu watamuelewa zaidi huyu bwana
 
Back
Top Bottom