A
Anonymous
Guest
Mheshimiwa Rais,
Awali ya yote, tunakupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya katika kuijenga nchi yetu, hususan katika kuboresha sekta ya afya. Sisi kama watumishi na wadau wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), tumeona ni wajibu wetu kukuandikia taarifa hii kwa uzalendo na kwa maslahi mapana ya taasisi yetu.
Nia yetu si chuki dhidi ya mtu yeyote, bali ni kunusuru kilele cha huduma za afya nchini (Muhimbili) ambacho kwa sasa kinakabiliwa na changamoto kubwa za kiutawala na kiutendaji.
Mheshimiwa Rais, tunaomba kuwasilisha hoja zifuatazo kwa hatua na uchunguzi:
Kukiukwa kwa Kanuni za Utumishi: Taratibu za uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu na kati hazizingatiwi kwa mujibu wa Kanuni za Wafanyakazi (2023). Viongozi wengi wamekaimu nafasi kwa muda mrefu kinyume na taratibu, huku wengine wakiteuliwa kwa upendeleo wa kirafiki.
Kutoshirikisha Wasaidizi: Uongozi umejijengea tabia ya kutopokea ushauri kutoka kwa Wakurugenzi wasaidizi na wataalamu, jambo linalopelekea miradi na manunuzi mengi kukwama mezani kwa mkurugenzi kwa miezi kadhaa.
Gharama za Juu: Gharama za matibabu kwa sasa zimepanda kiasi cha kuzidi hospitali binafsi za daraja la juu, hali inayowaumiza wananchi wanyonge.
Ucheleweshaji wa Huduma: Vipimo vya msingi (kama maabara na X-ray) vinachukua hadi siku mbili kupata majibu, hali inayozorotesha huduma ikilinganishwa na taasisi jirani (MOI, JKCI na Ocean Road).
Upasuaji: Foleni za upasuaji ni ndefu kutokana na usimamizi mbovu, huku vitendea kazi na dawa vikosekana wodini licha ya serikali kutoa fedha.
Miradi ya Ukarabati: Miradi kama ule wa Jengo la "Sabasaba" (lililotumia takriban TZS milioni 650 kwa ukarabati mdogo) na miradi mingine ya ununuzi wa samani (furniture) inatia shaka.
Mfumo wa Malipo (Control Numbers): Kuna malalamiko kuwa mfumo wa malipo ulidanganywa wakati mmoja kutoonyesha majina ya wagonjwa, hali iliyotoa mwanya wa uvujaji wa mapato.
Usimamizi wa Fedha za Msamaha: Fedha zilizoletwa na serikali (takriban bilioni 2) kusaidia wagonjwa wasiojiweza katika upandikizaji figo na usikivu zinatuhumiwa kutotumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
Kukosekana kwa Posho: Watumishi hawalipwi posho mpya zilizoidhinishwa na Serikali, huku kisingizio kikiwa ni hospitali kutokuwa na fedha wakati matumizi kwenye miradi ya ujenzi yakiwa makubwa.
Upendeleo: Kuna watumishi wachache (wanaojiita "machawa") wanaopata fursa na malipo ya ziada kinyume na wengine.
1. Uchunguzi wa Kiidara (Forensic Audit): Vyombo vya uchunguzi (PCCB, CAG, na PPRA) vifanye ukaguzi wa miradi yote ya ukarabati na manunuzi iliyofanyika katika miaka mitatu iliyopita.
2. Mapitio ya Uongozi: Kufanya mabadiliko ya uongozi ili kuingiza watu wenye weledi na uzoefu wa kuongoza taasisi kubwa kama Muhimbili.
3. Uchunguzi wa Mikataba: Mikataba ya ardhi (kama kule Vikuruti) na ile ya wauzaji dawa (suppliers) ichunguzwe ili kubaini kama kuna harufu ya rushwa.
Mheshimiwa Rais, Muhimbili ni roho ya sekta ya afya nchini. Isipookolewa sasa, miundombinu na utaalamu mkubwa uliowekezwa na serikali yako utapotea. Tunaamini katika nia yako njema na tunaomba vyombo vyako vifanye kazi kurejesha hadhi ya Hospitali hii.
Wako watiifu,
Watumishi Watiifu na Wazalendo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Awali ya yote, tunakupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya katika kuijenga nchi yetu, hususan katika kuboresha sekta ya afya. Sisi kama watumishi na wadau wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), tumeona ni wajibu wetu kukuandikia taarifa hii kwa uzalendo na kwa maslahi mapana ya taasisi yetu.
Nia yetu si chuki dhidi ya mtu yeyote, bali ni kunusuru kilele cha huduma za afya nchini (Muhimbili) ambacho kwa sasa kinakabiliwa na changamoto kubwa za kiutawala na kiutendaji.
Mheshimiwa Rais, tunaomba kuwasilisha hoja zifuatazo kwa hatua na uchunguzi:
1. Changamoto za Uongozi na Utawala
Uongozi wa sasa chini ya Mkurugenzi Mtendaji umekumbwa na changamoto ya kitaaluma na kiutendaji. Maamuzi mengi yanategemea hisia (emotional management) badala ya taaluma (professionalism). Kuna malalamiko makubwa juu ya:Kukiukwa kwa Kanuni za Utumishi: Taratibu za uteuzi wa viongozi wa ngazi za juu na kati hazizingatiwi kwa mujibu wa Kanuni za Wafanyakazi (2023). Viongozi wengi wamekaimu nafasi kwa muda mrefu kinyume na taratibu, huku wengine wakiteuliwa kwa upendeleo wa kirafiki.
Kutoshirikisha Wasaidizi: Uongozi umejijengea tabia ya kutopokea ushauri kutoka kwa Wakurugenzi wasaidizi na wataalamu, jambo linalopelekea miradi na manunuzi mengi kukwama mezani kwa mkurugenzi kwa miezi kadhaa.
2. Kuzorota kwa Huduma za Matibabu na Gharama Kubwa
Muhimbili imekuwa kimbilio la wenye uwezo wa kifedha pekee, kinyume na dhana ya Hospitali ya Taifa.Gharama za Juu: Gharama za matibabu kwa sasa zimepanda kiasi cha kuzidi hospitali binafsi za daraja la juu, hali inayowaumiza wananchi wanyonge.
Ucheleweshaji wa Huduma: Vipimo vya msingi (kama maabara na X-ray) vinachukua hadi siku mbili kupata majibu, hali inayozorotesha huduma ikilinganishwa na taasisi jirani (MOI, JKCI na Ocean Road).
Upasuaji: Foleni za upasuaji ni ndefu kutokana na usimamizi mbovu, huku vitendea kazi na dawa vikosekana wodini licha ya serikali kutoa fedha.
3. Matumizi Mabaya ya Fedha na Tuhuma za Rushwa
Kuna viashiria vya ubadhirifu wa fedha za umma kupitia miradi ya ukarabati na manunuzi:Miradi ya Ukarabati: Miradi kama ule wa Jengo la "Sabasaba" (lililotumia takriban TZS milioni 650 kwa ukarabati mdogo) na miradi mingine ya ununuzi wa samani (furniture) inatia shaka.
Mfumo wa Malipo (Control Numbers): Kuna malalamiko kuwa mfumo wa malipo ulidanganywa wakati mmoja kutoonyesha majina ya wagonjwa, hali iliyotoa mwanya wa uvujaji wa mapato.
Usimamizi wa Fedha za Msamaha: Fedha zilizoletwa na serikali (takriban bilioni 2) kusaidia wagonjwa wasiojiweza katika upandikizaji figo na usikivu zinatuhumiwa kutotumika kwa malengo yaliyokusudiwa.
4. Hali ya Watumishi na Maslahi
Moyo wa kazi miongoni mwa watumishi umeshuka kwa kiwango cha juu:Kukosekana kwa Posho: Watumishi hawalipwi posho mpya zilizoidhinishwa na Serikali, huku kisingizio kikiwa ni hospitali kutokuwa na fedha wakati matumizi kwenye miradi ya ujenzi yakiwa makubwa.
Upendeleo: Kuna watumishi wachache (wanaojiita "machawa") wanaopata fursa na malipo ya ziada kinyume na wengine.
5. Uhusiano wa Muhimbili na Mloganzila
Mloganzila imekomaa na ina mifumo imara ya utawala. Tunashauri iachiwe ijitegemee kurejesha ufanisi. Kwa sasa Mloganzila inatumiwa kama kichaka cha kupata rasilimali zinazopelekwa Main Campus bila tija ya wazi kwa Mloganzila yenyewe.6. Mapendekezo yetu
Mheshimiwa Rais, kwa unyenyekevu mkubwa tunaomba:1. Uchunguzi wa Kiidara (Forensic Audit): Vyombo vya uchunguzi (PCCB, CAG, na PPRA) vifanye ukaguzi wa miradi yote ya ukarabati na manunuzi iliyofanyika katika miaka mitatu iliyopita.