Barua ya wazi kwa Rais Samia: lose lips sink ships

Barua ya wazi kwa Rais Samia: lose lips sink ships

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Nakusalimu mheshimiwa Raisi.

Kwa unyenyekevu mkubwa sana naandika haya kama mwananchi wa kawaida ambaye anapenda kuona wewe unafanikiwa. Huu ni ushauri, hivyo unaweza ukautendea kazi au ukaupuuza vilevile.

Majuzi tarehe 18 September 2024, ulitoa hotuba nzito sana ambayo imezua gumzo siyo tu Tanzania, bali duniani kote. Wewe binafsi umekuwa gumzo la dunia au "Talk of the town". Wengi wameshangazwa huku wengine wakikushangilia kwa kuonesha msimamo mkali na uthabiti.

Mimi nitaongelea na kukichambua kile ambacho ulikisema, hasahasa kuhusu mauaji (Killings) na uhuru wa nchi kujiamulia mambo (National Sovereignty). Mengine sina utaalamu nayo na nitawaachia waswahili waendelee kuyazungumza.

Mosi, mauaji hutokea duniani kote: Nakubaliana na wewe kwa asilimia 1000% katika hili. Japo kitaalamu haikutakiwa kabisa kauli kama hii izungumzwe na mkuu wa nchi kwenye jambo nyeti kama mauaji ya yanayoendelea nchini.

Kisheria hili sisi tunaliita Tu QuoQue Fallacy ambapo unaamua kushambulia tabia binafsi ya mpinzani wako (Personal Behavior of opponent) ili kuhalalisha kile ambacho kimefanywa na wewe. Hili linaweza kuwa ni sawa kwenye mambo mengine, lakini siyo uhai wa mwanadamu. Hichi ulichokisema juzi kinakujengea taswira mbovu, kwamba unakubaliana na kinachofanyika kwako kwasababu kinafanyika na kwingineko.

Tuliosoma sheria tunafahamu kitu kimoja muhimu kwamba, kwenye mauaji ya binadamu kuna dhana ya iitwayo MURDER au HOMICIDE. Ambayo ni kutoa uhai wa binadamu mwingine kwa kukusudia. Hili hufanywa na mtu binafsi. Kama ulivyosema hili hufanyika duniani kote, hata kule Marekani linafanyika kila siku na ukatoa mfano wa Gun Violence.

Tatizo ni kwamba kisheria siyo kila mauaji ni MURDER au HOMICIDE. Mauaji mengine yanaangukia kwenye kundi la GROSS VIOLATION OF HUMAN RIGHTS na kuwa aidha GENOCIDE au CRIMES AGAINST HUMANITY. Mauaji yakishaingiza mkono wa serikali, hayawi tena MURDER or HOMICIDE kama ambavyo ulisema hapo majuzi.

Kweli nchini Marekani kuna Gun Violence, kweli nchini Tanzania kuna mauaji ya Albino na Watoto. Lakini haya ni mauaji ya kawaida ambayo hufanywa na watu binafsi ambao hushitakiwa kupitia sheria ya kanuni ya adhabu (The Penal Code) kwa kosa la mauaji ya kukusudia (Murder or Homicide) au kutokusudia (Manslaughter).

Mauaji yakifanywa tu na mkono wa serikali (State Sponsored), taswira nzima inabadilika na haiwi tena Murder or Homicide tu. Ndiyo maana mikataba yote ya kimataifa ya haki za binadamu, iwe chini ya East African Community, African Union au United Nations, raia wa nchi wanachama huwa hawashtakiani wao wenyewe kwa uvunjifu wa haki za binadamu, bali hushitaki serikali za nchi zao ambazo zimevunja haki zao.

Falsasa nzima dhidi ya hili ni kwamba Serikali ndiyo yenye dhamana na mamlaka ya kulinda raia wake pamoja na mali zao (Primary Responsibility to protect its citizen). Hivyo inapoonekana kwamba serikali hiyo yenye dhamana ya kulinda watu wake inafuatisha sera fulani ya kukandamiza raia wake basi huwezi kusema tena mauaji hayo ni kawaida. Maana serikali haiwezi kujishitaki na kujiwajibisha yenyewe, ndiyo maana makosa yanawekewa uzito duniani kote ili serikali zisijisahau na kuanza kutesa raia wake.

Hivyo makosa yote kama Murder, Kidnapping, Causing Grievous Bodily Harm yakifanywa chini ya mkono na udhamini wa serikali (State Sponsored) basi hubadilika na kuongezewa uzito wa kuwa makosa ya kimataifa ambayo huwezi kusema mbona kila siku yanatokea tu:
  • Murder/Homicide inageuka na kuangukia kwenye aidha Crimes Against Humanity, Gross Violation of Human Rights au Genocide.
  • Kidnappings/Abductions inageuka na kuwa Enforced Disappearance.
  • Rape, Defilement, yanageuka na kuwa aidha Torture, Genocide, Crimes Against Humanity au War Crime.

Muhimu kufahamu ni kwamba, kabla hatujazungumzia mauaji mengine na kutoa mifano ya nchi za watu ni vyema tungefahamu fika kwamba Gun Violence in America, hairatibiwi na serikali, lakini pia hata mauaji ya Albino hapa kwetu hatukuwahi kuituhumu serikali kwamba inahusika, kwasababu tunafahamu yalifanywa na watu binafsi ambao wengine waliwajibishwa. Hivyo yalikuwa ni mauaji ya kawaida tu (Murder/Homocide) yaliyofanywa na watanzania dhidi ya wenzao kwasababu lukuki ukiwemo ushirikina.

Pili, Tanzania haitakiwi kuingiliwa na mataifa mengine: Hili nalo nakuunga mkono kwa asilimia 1000%. Ulinifurahisha kwamba ulitumia makataba wa Vienna (Vienna Convention on Diplomatic and Consular Relations, 1961).

Jambo moja tu ambalo hukutakiwa kulisema ni kwamba mataifa mengine wasiingilie mambo yetu ilhali kwao kuna shida. Narudi palepale kwenye hoja ya kwanza, kwenye makosa ya kawaida ambayo wananchi huwafanyia wananchi wenzake (Citizen vs Citizens) ulikuwa sawa kabisa, kwasababu serikali ina haki uwezo wa kushughulikia wahalifu kwa kuwapandisha kizimbani.

Ulijikwaa pale kwenye mauaji ya marehemu Mzee Mzee Kibao na utakeji mwingine, ambao mpaka sasa kuna ushahidi kwamba uliratibiwa na watu wa mfumo hivyo ni (State Sponsored Killings and Enforced Disappearance of Persons). Hapa inakuwa ni Dola dhidi ya mwananchi wake (The State vs Citizens).

Jambo ambalo washauri wako hawakukutajia na limekuchafua kimataifa ni kwamba kwenye State Sponsored Killings/State Sponsored Violence/Genocide/Crimes Against Humanity/Gross Violations of Human Rights, dhana nzima ya State Sovereignty huwa inapoteza mashiko. Sheria za kimataifa huruhusu mataifa mengine kuzikemea, kuzikosoa na hata kuziwajibisha serikali za nchi nyingine zinazofanya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.

Mkataba wa Vienna unataka nchi isiingiliwe kwenye mambo yake halali, lakini huu mkataba ni sehemu ndogo sana kwenye dunia ya sheria za kimataifa. Huu mkataba inabidi usomwe sambamba pamoja na mikataba mingine mikubwa ya kimataifa kama The United Nations Charter 1945, The ICCPR 1966, The Banjul Charter 1986, ambayo hutaka nchi zote ziheshimu utu na haki za raia wake.

Lakini pia nchi yetu ya Tanzania tumesaini mikataba mingi ya haki za binadamu ya UN, AU na EAC ambayo inazipa haki na wajibu wa kukemea uvunjifu wa haki za binadamu unaofanyika kwingine. Ila kubwa zaidi Customary International Law, inakitu kinachoitwa Jus Cogens ambazo ndiyo Sheria Mama zisizoweza kuvunjwa na taifa lolote lile kupitia mkataba wa kimataifa (Treaty) au sheria za bunge (National Legislation) na zinatakiwa ziheshimiwe na dunia nzima.

Jus Cogens inakataza mambo kama Genocide, Torture, Slavery, Wars of Aggression na kuipa jumuiya ya kimataifa haki za kuyakemea na kuyadhibiti popote pale yatakapotokea duniani. Hivyo mabalozi walipolaani kinachofanyika nchini walikuwa sahihi, wakitekeleza wajibu wao chini ya sheria za kimataifa. Raisi Samia ungekuwa sahihi sana kama ungekosoa mauaji ambayo serikali ya Marekani inafanya dhidi ya raia wake.

Mfano ungesema serikali ya Marekani haina uhalali kwasababu imeua maelfu ya raia wasio na hatia kule Gaza kwa kuunga mkono serikali ya kibaguzi ya Kizayuni inayofanya Genocide na kesi iko mahakama ya dunia ICJ, walau ungeeleweka na sidhani kama Balozi wa USA angekuwa na ujasiri wa kuja kupangua hoja ya Gaza Genocide. Japo hili nalo lisingehalalisha kinachoendelea nchini. Walau ungesema unachukua hatua za msingi na utafanyia kazi ushauri wao kwasababu wao ni wadau wetu wakubwa wa maendeleo.

Hebu nikupe mfano mzuri kabisa: Kitengo cha Propaganda cha CCM wanarusha hotuba ya Mzee Mkapa ya mwaka 2000 alipokataa kuingiliwa na watu wa nje. Kinachonishangaza ni kwama CCM wameshindwa kufahamu kwamba Mzee Mkapa alikuwa anaongea vile katika muktadha upi, kwa malengo yapi na alimlenga nani.

Mzee Mkapa alikuwa sahihi kusema vile katika asilimia 1000%, kwasababu kwanza kabisa ule ulikuwa ni uchaguzi wa kisiasa (Political Elections) jambo ambalo kisheria nchi nyingine hazitakiwi kabisa kuingilia. Hayakuwa mauaji ya watu yale. Lakini pili, alikuwa anaongea na wasimamizi wa kimataifa wa uchaguzi (International Observers) ambao walikosoa mwenendo mzima wa uchaguzi ule ambao ulijaa vitimbwi, uhuni na fitna.

Mzee Mkapa huyohuyo mwaka 2001 baada ya mauaji ya Zanzibar yaliyofanywa na polisi wa Tanzania, hakudiliki kuwanyooshea vidole mataifa mengine walipokosoa matumizi mazito ya mabavu. Alipohojiwa kule BBC Hardtalk alisema hata yeye anakereka sana na anawaonea huruma wazanzibari ndiyo maana akapeleka polisi wapambane na wahalifu.

Mzee Mkapa huyohuyo mwaka 2001 baada ya mauaji ya Zanzibari yaliyofanywa na polisi wa Tanzania, aliamua kusikiliza na kutii ushauri wa mataifa ya nje kwa kuanzisha mazungumzo na CUF ambayo yalizaa kitu kinachoitwa MUAFAKA I kule visiwani Zanzibar. Walau alionyesha kuchukua hatau, japo alichokifanya kilikuwa kibaya na yeye akakiri kwenye kitabu chake kwamba yale mauaji yulikuwa ni doa kubwa kwenye utawala wake.

Mwisho kabisa: Dhana nzima ya State Sovereignty ina maana sana endapo itatumiwa pale kwenye mambo ya msingi na muhimu, siyo kutumika kama kichaka cha serikali kufanya uhalifu na uvunjifu wa haki za binadamu.

Mikataba ya kimataifa na sheria zitakuwa upande wako endapo utasema kuhusu State Sovereignty kwenye mambo ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Mfano, hatutaki masuala ya ushoga, hatutaki kuchaguliwa marafiki, hatulazimishwi kuruhusu kila uwekezaji au masuala ya utungaji wa sheria za bunge nk.

Lakini kisheria mambo kama Torture, Enforced Disappearance of Persons, Extermination, Genocide au Crimes Against Humanity yakiwa yanafanyika kwenye nchi na serikali yake, basi fahamu fika nchi yoyote ile ndani ya jumuiya ya kimataifa inaruhusiwa kuingilia au kukemea udhalimu huo kupitia kanuni ya RP (The Right to Protect) ambayo hiyohiyo ilitumiwa na Mzee Nyerere kuvamia Uganda, Shelisheli, Komoro, Msumbiji na Afrika Kusini.

NB: Pia kumbuka, haya makosa ni ya kimataifa (International Crimes). Makosa kama haya mara zote hufanywa na serikali au vikundi vya kijeshi dhidi ya raia wa nchi fulani. Njia pekee ambayo jumuiya ya kimataifa inaweza kuziwajibisha serikali kandamizi au vikundi vya kijeshi ni kulazimisha uwajibikaji aidha kupitia kushitakiwa kwenye mahakama za kimataifa (Kumbuka Uhuru na Rutto), kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kutengwa (Kumbuka Afrika Kusini), Kupiga marufuku safari za wanasiasa (Kumbuka Paul Makonda) au kuunga mkono makundi ya kisiasa ndani ya nchi ili yakutoe kimabavu (Jambo la hatari zaidi)
 
Nadhani pana watu wanampa taarifa zisizo sahihi kabisa kwa manufaa yao Viongozi wakubwa muda mwingine wanakua wapo Tanzania ila hakuna kitu anajua kuhusu Tanzania kwa sababu ya wahuni wachache wanaopeleka taarifa zisizo sahihi kwenye Mamlaka za juu kwa manufaa yao na hao...
 
Kisheria hili sisi tunaliita Tu QuoQue Fallacy ambapo unaamua kushambulia tabia binafsi ya mpinzani wako (Personal Behavior of opponent) ili kuhalalisha kile ambacho kimefanywa na wewe. Hili linaweza kuwa ni sawa kwenye mambo mengine, lakini siyo uhai wa mwanadamu. Hichi ulichokisema juzi kinakujengea taswira mbovu, kwamba unakubaliana na kinachofanyika kwako kwasababu kinafanyika na kwingineko.
ID za zamani hadi zimeibuka.....ngona tusome kwa utulivu.
 
Jambo ambalo washauri wako hawakukutajia na limekuchafua kimataifa ni kwamba kwenye State Sponsored Killings/State Sponsored Violence/Genocide/Crimes Against Humanity/Gross Violations of Human Rights, dhana nzima ya State Sovereignty huwa inapoteza mashiko. Sheria za kimataifa huruhusu mataifa mengine kuzikemea, kuzikosoa na hata kuziwajibisha serikali za nchi nyingine zinazofanya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu
Sovereignity kama sovereignity
kurwa jilala
 
Nakusalimu mheshimiwa Raisi.

Kwa unyenyekevu mkubwa sana naandika haya kama mwananchi wa kawaida ambaye anapenda kuona wewe unafanikiwa. Huu ni ushauri, hivyo unaweza ukautendea kazi au ukaupuuza vilevile.

Majuzi tarehe 18 September 2024, ulitoa hotuba nzito sana ambayo imezua gumzo siyo tu Tanzania, bali duniani kote. Wewe binafsi umekuwa gumzo la dunia au "Talk of the town". Wengi wameshangazwa huku wengine wakikushangilia kwa kuonesha msimamo mkali na uthabiti.

Mimi nitaongelea na kukichambua kile ambacho ulikisema, hasahasa kuhusu mauaji na uhuru wa nchi kujiamulia mambo (National Sovereignty). Mengine sina utaalamu nayo na nitawaachia waswahili waendelee kuyazungumza.

Mosi, mauaji hutokea duniani kote: Nakubaliana na wewe kwa asilimia 1000% katika hili. Japo kitaalamu haikutakiwa kabisa kauli kama hii izungumzwe na mkuu wa nchi kwenye jambo nyeti kama mauaji ya yanayoendelea nchini.

Kisheria hili sisi tunaliita Tu QuoQue Fallacy ambapo unaamua kushambulia tabia binafsi ya mpinzani wako (Personal Behavior of opponent) ili kuhalalisha kile ambacho kimefanywa na wewe. Hili linaweza kuwa ni sawa kwenye mambo mengine, lakini siyo uhai wa mwanadamu. Hichi ulichokisema juzi kinakujengea taswira mbovu, kwamba unakubaliana na kinachofanyika kwako kwasababu kinafanyika na kwingineko.

Tuliosoma sheria tunafahamu kitu kimoja muhimu kwamba, kwenye mauaji ya binadamu kuna dhana ya iitwayo MURDER au HOMICIDE. Ambayo ni kutoa uhai wa binadamu mwingine kwa kukusudia. Hili hufanywa na mtu binafsi. Kama ulivyosema hili hufanyika duniani kote, hata kule Marekani linafanyika kila siku na ukatoa mfano wa Gun Violence.

Tatizo ni kwamba kisheria siyo kila mauaji ni MURDER au HOMICIDE. Mauaji mengine yanaangukia kwenye kundi la GROSS VIOLATION OF HUMAN RIGHTS na kuwa aidha GENOCIDE au CRIME AGAINST HUMANITY. Mauaji yakishaingiza mkono wa serikali, hayawi tena MURDER or HOMICIDE kama ambavyo ulisema hapo majuzi.

Kweli nchini Marekani kuna Gun Violence, kweli nchini Tanzania kuna mauaji ya Albino na Watoto. Lakini haya ni mauaji ya kawaida ambayo hufanywa na watu binafsi ambao hushitakiwa kupitia sheria ya kanuni ya adhabu (The Penal Code) kwa kosa la mauaji ya kukusudia (Murder or Homicide).

Mauaji yakifanywa tu na mkono wa serikali (State Sponsored), taswira nzima inabadilika na haiwi tena Murder or Homicide tu. Ndiyo maana mikataba yote ya kimataifa ya haki za binadamu, iwe chini ya East African Community, African Union au United Nations, raia wa nchi wanachama huwa hawashtakiani wao wenyewe kwa uvunjifu wa haki za binadamu, bali hushitaki serikali za nchi zao ambazo zimevunja haki zao.

Falsasa nzima dhidi ya hili ni kwamba Serikali ndiyo yenye dhamana na mamlaka ya kulinda raia wake pamoja na mali zao (Primary Responsibility to protect its citizen). Hivyo inapoonekana kwamba serikali hiyo yenye dhamana ya kulinda watu wake inafuatisha sera fulani ya kukandamiza raia wake basi huwezi kusema tena mauaji hayo ni kawaida. Maana serikali haiwezi kujishitaki na kujiwajibisha yenyewe, ndiyo maana makosa yanawekewa uzito duniani kote ili serikali zisijisahau na kuanza kutesa raia wake.

Hivyo makosa yote kama Murder, Kidnapping, Causing Grievous Bodily Harm yakifanywa chini ya mkono na udhamini wa serikali (State Sponsored) basi hubadilika na kuongezewa uzito wa kuwa makosa ya kimataifa ambayo huwezi kusema mbona kila siku yanatokea tu:
  • Murder/Homicide inageuka na kuangukia kwenye aidha Crimes Against Humanity, Gross Violation of Human Rights au Genocide.
  • Kidnappings/Abductions inageuka na kuwa Enforced Disappearance.

Muhimu kufahamu ni kwamba, kabla hatujazungumzia mauaji mengine na kutoa mifano ya nchi za watu ni vyema tungefahamu fika kwamba Gun Violence in America, hairatibiwi na serikali, lakini pia hata mauaji ya Albino hapa kwetu hatukuwahi kuituhumu serikali kwamba inahusika, kwasababu tunafahamu yalifanywa na watu binafsi ambao wengine waliwajibishwa. Hivyo yalikuwa ni mauaji ya kawaida tu (Murder/Homocide) yaliyofanywa na watanzania dhidi ya wenzao kwasababu lukuki ukiwemo ushirikina.

Pili, Tanzania haitakiwi kuingiliwa na mataifa mengine: Hili nalo nakuunga mkono kwa asilimia 1000%. Ulinifurahisha kwamba ulitumia makataba wa Vienna (Vienna Convention on Diplomatic and Consular Relations, 1961).

Jambo moja tu ambalo hukutakiwa kulisema ni kwamba mataifa mengine wasiingilie mambo yetu ilhali kwao kuna shida. Narudi palepale kwenye hoja ya kwanza, kwenye makosa ya kawaida ambayo wananchi huwafanyia wananchi wenzake (Citizen vs Citizens) ulikuwa sawa kabisa, kwasababu serikali ina haki uwezo wa kushughulikiwa wahalifu kwa kuwapandisha kizimbani.

Ulijikwaa pale kwenye mauaji ya marehemu Mzee Mzee Kibao na utakeji mwingine, ambao mpaka sasa kuna ushahidi kwamba uliratibiwa na watu wa mfumo hivyo ni (State Sponsored Killings and Enforced Disappearance of Persons). Hapa inakuwa ni Nchi dhidi ya mwananchi (The State vs Citizens).

Jambo ambalo washauri wako hawakukutajia na limekuchafua kimataifa ni kwamba kwenye State Sponsored Killings/State Sponsored Violence/Genocide/Crimes Against Humanity/Gross Violations of Human Rights, dhana nzima ya State Sovereignty huwa inapoteza mashiko. Sheria za kimataifa huruhusu mataifa mengine kuzikemea, kuzikosoa na hata kuziwajibisha serikali za nchi nyingine zinazofanya uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.

Hata mkataba wa Vienna unataka nchi isiingiliwe kwenye mambo yake halali tu, siyo masuala mazima ya uvunjifu wa haki za binadamu. Hebu nikupe mfano mzuri kabisa: Kitengo cha Propaganda cha CCM wanarusha hotuba ya Mzee Mkapa ya mwaka 2000 alipokataa kuingiliwa na watu wa nje.

Mzee Mkapa alikuwa sahihi kusema vile, kwasababu kwanza kabisa ule ulikuwa ni uchaguzi wa kisiasa (Political Elections) na siyo mauaji ya watu. Lakini pili, alikuwa anaongea na wasimamizi wa kimataifa wa uchaguzi (International Observers) ambao walikosoa mwenendo mzima wa uchaguzi ule.

Mzee Mkapa huyohuyo mwaka 2001 baada ya muaji ya Zanzibar yaliyofanywa na polisi wa Tanzania, hakudiliki kuwanyooshea vidole mataifa mengine walipokosoa matumizi mazito ya mabavu. Kule BBC Hardtalk alisema hata yeye anakereka sana lakini alikuwa anapambana na uhalifu.

Mwisho kabisa: Dhana nzima ya State Sovereignty ina maana sana endapo itatumiwa pale kwenye mambo ya msingi na muhimu. Mikataba ya kimataifa na sheria zitakuwa upande wako. Lakini kisheria mambo kama Extermination, Genocide au Crimes Against Humanity yakiwa yanafanyika kwenye nchi yoyote ile jumuiya ya kimataifa inaruhusiwa kuingilia kupitia kanuni ya RP (The Right to Protect) ambayo hiyohiyo ilitumiwa na Mzee Nyerere kuvamia Uganda, Shelisheli, Komoro, Msumbiji na Afrika Kusini.
Uchambuzi mufti wa kizalendo uso matusi,dharau, kebehi wala bezo yaani madini tupu.
 
Lakini kisheria mambo kama Extermination, Genocide au Crimes Against Humanity yakiwa yanafanyika kwenye nchi yoyote ile jumuiya ya kimataifa inaruhusiwa kuingilia kupitia kanuni ya RP (The Right to Protect) ambayo hiyohiyo ilitumiwa na Mzee Nyerere kuvamia Uganda, Shelisheli, Komoro, Msumbiji na Afrika Kusini.
Asante sana Mkuu umetutoa tongo tongo.

Kumbe mambo yako hivi.
 
Back
Top Bottom