Barua ya Wazi kwa Rais Samia: Umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vya ARV nchini

Barua ya Wazi kwa Rais Samia: Umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vya ARV nchini

OFISI YA RAIS,
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
DR. SAMIA SULUHU HASSAN,

YAH: UMUHIMU WA KUANZISHA NA KUENDELEZA VIWANDA VYA KUZALISHA DAWA ZA KUPUNGUZA MAKALI YA VIRUSI VYA UKIMWI (ARVs) NCHINI

Mheshimiwa Rais,

Kwa heshima na taadhima za hali ya juu, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati kwa uongozi wako thabiti, wenye maono, na uliojaa dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo Watanzania. Katika kipindi cha uongozi wako, tumeshuhudia mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali, hususan afya, miundombinu, elimu, na uchumi wa nchi yetu. Jitihada zako za kuimarisha huduma za afya kwa kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba, kuboresha hospitali, na kuimarisha mifumo ya bima ya afya ni ishara ya uongozi wenye dira na mapenzi kwa wananchi. Kwa moyo wa dhati, nakushukuru na kukupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya kwa taifa letu.

Kwa heshima na taadhima, napenda kuwasilisha maoni kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kuendeleza viwanda vya kuzalisha dawa za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi (ARVs) hapa nchini, ili kuimarisha sekta ya afya na kupunguza utegemezi wa dawa kutoka nje.

Kuanzisha na kuendeleza viwanda vya ndani vya kuzalisha ARVs kutahakikisha upatikanaji wa dawa hizi kwa urahisi, kupunguza gharama za matibabu, na kuimarisha uhuru wa Tanzania katika sekta ya afya. Uzalishaji wa ndani wa ARVs utafungua fursa kwa tafiti mpya za kisayansi zinazolenga kuboresha ubora wa dawa hizi kulingana na mahitaji ya Watanzania.

Pia, Tanzania itapata udhibiti wa uzalishaji wa dawa zake, kupunguza utegemezi wa misaada ya kimataifa ambayo mara nyingine huja na masharti. Ili kufanikisha hili, Serikali inaweza kushirikiana na wawekezaji wa ndani na nje katika kuanzisha na kuimarisha viwanda vya kuzalisha ARVs kwa kuhakikisha vinaendeshwa kwa ufanisi na ubora wa kimataifa.

Kuanzisha na kuendeleza viwanda vya kuzalisha ARVs ni hatua muhimu kwa maendeleo ya sekta ya afya na uchumi wa Tanzania. Kupitia uwekezaji katika uzalishaji wa dawa hizi, nchi yetu itaweza kupambana na changamoto ya UKIMWI kwa ufanisi zaidi, kupunguza gharama za uagizaji wa dawa kutoka nje, na kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania.

Mheshimiwa Rais, kwa kutambua juhudi zako za kuimarisha sekta ya afya na uchumi wa nchi, naomba Serikali, sekta binafsi, na wadau wa afya washirikiane kuhakikisha kwamba viwanda vya kuzalisha ARVs si tu vinaanzishwa bali vinaendelezwa kwa ufanisi na tija kwa manufaa ya taifa. Tuna imani kuwa chini ya uongozi wako thabiti, hatua hii itawezekana na kuleta matokeo chanya kwa ustawi wa Watanzania.

Kwa heshima na taadhima,
Ahsante
Hii tumeshaanza kuchonga toothpicks au bado tunaagiza China?
 
yaani sisi vidampa ndio unataka tuingilie biashara za watu..kuna magonjwa wanene wa dunia wamefanya ni biashara kubwa ya kuuza madawa mojawapo ni hiyo ARV ni moja ya biashara kubwa inayowaingizia mabilioni ya dola..kama huamini ajaribu mtu yoyote kujitokeza hadharani kuwa anatibu ukimwi na ikawa kweli watu wanapona..ndio utaona kitakachomkuta..hayo magonjwa ni fursa ya kupiga hela usicheze anga za wahuni wanaofanya biashara ya madawa kupitia hayo maradhi.. ni zaidi ya hatari na kujitafutia balaa wakikugundua.!
 
yaani sisi vidampa ndio unataka tuingilie biashara za watu..kuna magonjwa wanene wa dunia wamefanya ni biashara kubwa ya kuuza madawa mojawapo ni hiyo ARV ni moja ya biashara kubwa inayowaingizia mabilioni ya dola..kama huamini ajaribu mtu yoyote kujitokeza hadharani kuwa anatibu ukimwi na ikawa kweli watu wanapona..ndio utaona kitakachomkuta..hayo magonjwa ni fursa ya kupiga hela usicheze anga za wahuni wanaofanya biashara ya madawa kupitia hayo maradhi.. ni zaidi ya hatari na kujitafutia balaa wakikugundua.!
Viwanda vipo na kuna mikataba ilisha sainiwa tayari.
 
Naomba panado ya kenya

Naomba metakeflin ya Italy

hivi viatu vimetokea moshi? Hapana naomba ivyo made in china

made in Tanzania?.aah hizi ztakua hazina ubora

Ndo tuproduce ARVs? Na watu wenyew wa CTC walivovurugwa
Viwanda vipo
 
Back
Top Bottom