Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
- Thread starter
- #21
Asante sana mkuu kwa pendekezo muhimu sana katika taifa letu. Ni kweli kabisa bila kumumunya maneno na kupepesa macho mipango miji ndio msingi wa maendeleo yoyote endelevu ya taifa lolote duniani.Wafanye mipango miji kwanza, miji imekaa kiswahili swahili. Hakuna barabara za kutosha, kubwa na feeder roads kwenye miji yetu yote, Nyumba zimejengwa ovyo ovyo bila utaratibu, unazalisha slums nyingi, miji michafu, hakuna sewage system, miji imekosa vyoo vya public, watu wanajisaidia vichakani, kwenye mito na wamefanya bahari kuwa vyoo vyao, nchi ni chafu mno. Rekebisheni hayo kwanza kabla ya kuunda magari. Bado nchi ipo savage katika level ya chini sana ya maendeleo.
Na swala hili la maendeleo ya miji yetu lipo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na Wizara hii ndio inaweza kushughulikia changamoto hizi zote za makazi kwa kushirikiana na mamlaka za serikali za mitaa.
Kiukweli changamoto kama upungufu wa barabara za kutosha, feeder roads, utaratibu wa ujenzi wa nyumba, na mifumo ya usafi kama vile vyoo vya umma na mfumo wa maji taka zinahitaji suluhisho la haraka sana ili tuweze kwendana na kasi ya maendeleo ya sekta zingine.
Lakini wakati tunashughulikia hayo yote ya makazi na barabara, Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaweza kuendelea kutengeneza mazingira wezeshi ya kuleta wawekezaji wa viwanda vya mabasi na daladala na uzalishaji ukaanza, huku miji ikiandaliwa kuwa na miundombinu bora na safi.