Barua ya wazi kwa Sheikh Walid
Assalaamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakaatuh,
Sheikh Walid, kwanza napenda kukufikishia pole zangu za dhati kwa mitihani na changamoto ambazo umekutana nazo katika kipindi hiki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akupe subira, nguvu na hekima katika kukabiliana na kila jambo.
Katika maisha ya waumini, mitihani ni sehemu ya safari. Mwenyezi Mungu amesema: “Hakika pamoja na uzito kuna wepesi.” (Surat Ash-Sharh 94:5-6). Pia tunakumbuka visa vya Mitume wa Mwenyezi Mungu ambao walipitia majaribu makubwa. Nabii Yusuf (A.S) alisingiziwa na kuvumilia kifungo, Nabii Ayyub (A.S) alivumilia maradhi na matatizo, na Mtume Muhammad (S.A.W) alikabiliana na tuhuma, kejeli na upinzani kutoka kwa watu wake. Lakini subira yao ilipelekea Mwenyezi Mungu kuwapa heshima na ushindi.
Sheikh, mimi binafsi ni mmoja wa Waislamu wanaokufuatilia kwa karibu. Nimekuwa nikisikiliza na kufaidika na khutuba zako katika Msikiti wa Kichangani Magomeni. Wewe ni miongoni mwa masheikh ambao nimekuwa nikikuheshimu na kujifunza mengi kupitia mawaidha yako.
Kwa sababu hiyo, jambo hili limenigusa sana. Ninaumia na nasikitika kuona jina lako likiwa katika mjadala huu unaoendelea ndani ya jamii. Ni jambo linalowahuzunisha wengi wanaokupenda na kukuheshimu.
Tunafahamu kuwa katika Uislamu wakati mwingine ukimya huwa ni hekima, hasa unapolenga kuzuia fitina na kulinda amani. Lakini pia, pale ambapo mtu anaona ameonewa, amesingiziwa au kuna jambo lisilo na ukweli, kutoa ufafanuzi kwa hekima kunaweza kusaidia kulinda heshima na kuondoa mashaka.
Kumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu sakata linalohusishwa na mwanamke mmoja. Kama jambo hilo halina ukweli, wengi wanaona ni vyema usikie sauti ya waumini wanaokuamini na utoe ufafanuzi ili jamii ijue ukweli wa jambo hili.
Sheikh Walid, wewe ni mmoja wa masheikh wanaopendwa na kuheshimiwa Tanzania. Watu wengi wamekuwa wakisikiliza nasaha zako na kukuona kama mfano wa uongozi wa dini. Ndiyo maana tunakuomba, kama utaona inafaa, uzungumze kwa utulivu, hekima na kwa kuzingatia misingi ya dini.
Mwenyezi Mungu akulinde dhidi ya mitihani, akupe subira, na akuongoze katika kila hatua.
Wassalaamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakaatuh.