Barua ya wazi Kwa wanawake: Usiolewe na mwanaume mpumbavu na mwoga!

Barua ya wazi Kwa wanawake: Usiolewe na mwanaume mpumbavu na mwoga!

Hii ndo kazi ya limbwata ukisha kulaaa unaropoka hovyo!!!...... kweli nina mjighorofa wangu eti mwanamke aondoke tu eti kisa leo nimelewa nimekojoa bafuni??? Mweee!! sasa huyo Mungu alisema tuvumiliane kwa taabu na raha wewe leo uni kimbie sababu za tabia zangu?? kweli??

halafu nyie mapolisi haya makanisa yenu haya yasiyo rasmi yaani ya Mahabusu yanawapoteza kweli......na tena huko kambini kwenu ni kufanyiana tuuuu warembo wenu!!...sasa wewe ngoja siku yakukute hapo kambini ndo utajua utamu wa risasi.

ukajipige risasi Lindoni ndo utajua mwanamke siyo mwenzio, make nyie hamnywagi sumu!! ni kujichapa tu shaba ya kooni!! na hapa ndo umejiroga kabisaaa!! ukipona basi wewe ni ke'' siyo kwa chuki hizi!! kwani me ni Malaika???? siyo! we subiri

km wewe ni mwanaume hii dhambi itakutafuna soon!!! hatudhihakiwi sisi!...ujinga wa mwanaume ni hekima kwa mwanamke!! umeuza uanaume!! wewe!! kajiunge Beijing,

sasa nimeamini wazi una kampasuko hapo kati kajikague!..... km sivyo unazo mbili!! km unabisha weka picha hapa utuondoe wasiwasi.......... hata mademu wanakushangaa ''huyu vepe? '' uongo wadada?


Duuuh!!

Kweli maisha magumu.

Pole Sana Mkuu
 
USIOLEWE NA MWANAUME MPUMBAVU NA MWOGA!

Kwa Mkono wa RObert Heriel.

Leo nitakaanga wapumbavu wote na waoga bila kupepesa. Iwe ni Mimi mwenyewe, wewe au Yule. Andiko hili halitamkwepa mwanaume yeyote Mpumbavu na mwoga bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na umri wake.
Kiazi mmoja[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Maisha yasingekuwa magumu usingetoa maoni yenye ishara zote kuwa unasongwa na kuzingirwa.


Kila la Kheri Mkuu.

Mungu akakuonekanie
Ni kweli Mkuu uko sahihi , nilizingirwa , nazingirwa na nitazidi kuzingirwa, n kusongwa napenda mno kuzingirwa halafu napangua kiuanaume, kifupi Siogopi kuzingirwa! ndo maana nasema ''wewe muoga kwa sababu unaogopa kusongwa na kuzingirwa''

sisi huku ndo zetu! kusongwa na kuzingirwa yaani tukiona vepe wako kimyaaa!! sisi wanaume tunalianzisha wenyewe songo mbingo!! sasa juu yenu msuke au mnyoe!! ..... km lilee la Makaburu wa kusini unaona mchonga alivo lianzisha maksudi tu,

tuliona ujinga huu tukalipiga maksudi ! ...halafu tukakataa misaada yao!!... tukaogea magwanji maksudi tu!! ...si unaona walivo tuheshimu?? .. kwa hiyo mkuu ndo zetu hujakosea uko mulemule umetamka mwenyee! sie ndo damu iyoiyo!

Umenisifia sana kidume mie naamini ''Ugumu wa maisha ndo kipimo cha akili'' sasa weye unapata kiulainii tu tutakupimaje?? basi lazima kuna anaekutafutia?? yupo mtu km mie anae penda, kusongwa na kuzingirwa ndo anaekupa! furaha na jeuri !

Hongera kwa kutafutiwa!!...yani kwa kauli zile!! nilijua tu uko ivo! ..... Mungu Mwenyewe alizingirwa na kusongwa na shetani na akapangua faster na mie ni mfano wake!!

Huyo mungu wako mwambie kabisa kuwa staki anionekanie kwa sababu nitampa kibano cha mbwa mwizi, muoga! akizidisha kiherehere nampiga makofi simkawizi!! atakusimulia tu!! '' ire makitu nyarusare siyo'kabisaaaa'....... upo hapo baba mkuru!!!
 
Huu Uzi ni kwaajili ya waliooa na wenye mpango wa kuoa kwahio Mimi Single for life haunihusu.
 
Mwanaume yeyote asiyemjali mke wake ni Mpumbavu.
Hawa alizurula Bustanini peke yake!! hatimaye akakutana na nyoka akajaribiwa!! akamplekea tunda Mumewe nae akala pia!! kwa muktadha huo Babu wa mababu zako ni mpumbavu???

unajua weee!! dogo tubu hii laana!! itakusumbua sana, km unabisha subiri..... utaota naniliu lazima tu!
 
USIOLEWE NA MWANAUME MPUMBAVU NA MWOGA!

Kwa Mkono wa RObert Heriel.

Leo nitakaanga wapumbavu wote na waoga bila kupepesa. Iwe ni Mimi mwenyewe, wewe au Yule. Andiko hili halitamkwepa mwanaume yeyote Mpumbavu na mwoga bila kujali nafasi yake, hadhi yake, na umri wake.

Aidha andiko hili natanguliza tahadhari ikiwa moyo wako ni mwepesi hautavumilia maonyo haya ni Bora uishie kusoma hapahapa. Endapo utakaidi ukaendelea kusoma basi nisihesabike wala nisipewe lawama Kwa madhara yatakayokupata.

Niite Taikon wa Fasihi, mkaangaji.

Mwanaume yeyote asiyemjali mke wake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyejali familia yake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyefanya kazi ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote asiyeweza kujitetea jamii yake ni mshenzi na Mpumbavu.
Mwanaume yeyote anayedhalilisha wanawake ni Mpumbavu.
Mwanaume yeyote anayeharibu watoto wa wenzake ni mshenzi na Mpumbavu tuu!

Enyi kina Dada, mabinti na wanawake wote, kamwe usiolewe na Mwanaume Mpumbavu.
Usimuendekeze Mpumbavu.
Usifikiri atabadilika, wapumbavu ni ngumu kubadilika.


Mwanaume yeyote mwenye aibu ya kufanya kazi ni Mpumbavu.
Usikubali hata akuongeleshe, akikufuata mtemee mate, akikuzingua mlete Polisi hapa tutakusaidia kukupa mawakili afikishwe mahakamani afungwe, apeleke upumbavu wake Jela huko.

Uliona wapi mwanaume akasikia aibu kufanya kazi. KAZI ndio inampa hadhi mwanaume yeyote.
Mwanaume habagui kazi ILIMRADI ni halali.
Mwanaume anayechagua kazi asikuoe IPO siku mtalala njaa.

Ogopa mwanaume aliyeiweka akili yake kwenye kazi moja. Mkimbie Kama ukoma. Huyo lazima akufanye uwe masikini dunia ingalipo.

Mwanaume mwoga usikubali akuoe.
Mwanaume mwoga hataweza kukulinda.
Kumbuka kuna woga na Heshima.
Kama Mwanaume woga anauita heshima mtemee mate kisha ukimbie, akikukimbiza akupige mlete kwetu tumfundishe adabu ili siku nyingine zimkae sawia.

Mwanaume anayedhulumiwa huyo usikubali akuoe. Huo ni mkosi katika familia yenu.
Usikubali kuolewa na Mwanaume anaemuchia Mungu. Mtakuwa Masikini, mtaonewa, watoto wako watateseka.

Usiolewe na Mwanaume asiyeweza kuwa hata na nyumba au Shamba, huyo atakuachia Mateso Duniani, atatesa watoto wako. Atawaacha watoto wako pasipo Urithi. Likikutongoza limwanaume la namna hiyo liliulize swali linashamba au kiwanja, Kama halina liulize utaishije na Mimi kama huna Shamba au kiwanja. Likikujibu bado linahangaika au mjini viwanja bei ghali liambie likuonyeshe Shamba au kiwanja huko kijijini. Halina litemee mate kisha toka nduki.
Usicheke na limwanaume lipumbavu litakutia mikosi na kukuzalisha Matoto ya hovyo hovyo.

Olewa na Mwanaume sio uolewe na mtu mwenye Cover/motherboard ya kiume alafu ndani ni jike jenzako.

Hakuna cha huruma hapa!
Usiolewe na Mwanaume anayependa kuhurumiwa hurumiwa, huyo ni mpuuzi.
Wanaohurumiwa ni watoto, wanawake na Wazee.
Ukiolewa na Mwanaume apendaye kuhurumiwa utaishi maisha ya kutia huruma mpaka unye mavi Kwa upuuzi wako.

Olewa na Mwanaume ambaye anapambana Kama Mwanaume. Akikosa mjini basi apate shambani. Akikosa shambani apate mjini. Sio limwanaume lililokosa bara na Pwani. Hilo usikubali kuolewa nalo. Ni ishara ya mwanaume Mpumbavu asiyeweza tumia akili yake vizuri

Usiolewe na Mwanaume anayekuhonga laki tano alafu halina hata kiwanja, utateseke wewe mpaka ukome. Huyo Hana akili nzuri no mwehu tuu anaweza fanya hivyo.
Labda umtumie kumchuna pesa zake ili lifilisike litie Akili.

Nasisitiza usikubali kuolewa na Mwanaume asiye na uwezo wa kuacha Urithi Kwa watoto atakaokupa. Utazaa mitoto itakayohangaika hapa Duniani mpaka ikome.

Lazima uchague mwanaume anayejua nyakati, na mazingira. Akiona mjini vitu bei ghali basi akanunue nje ya mji huko kijijini vilipo rahisi.
Sio limwanaume linalong'ang'ania kujenga mjini linakusanya pesa zisizojaa, mwisho linakosa bara na Pwani.

Usiolewe na Mwanaume anayejipenda kimwili kukushinda, yaani mtanashati kukushinda wengi uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, wengi ni wabinafsi, utashindia kanga moja Kama Sanda ya maiti, vitoto vyako vitavaa marapurapu wala Baba Yao halitajali.
Wanaume watashanashati kupitiliza wanatabia ya aidha ubinafsi au ushoga Kati ya hizo tabia lazima moja umkute nayo.

Hujawahi ona limwanaume limependeza lakini mkewe na Watoto wamevaa hovyo?? Ndio matokeo ya kuolewa na wanaume wapumbavu.

Usiolewe na Mwanaume Mlafi, na mwenye kujipenda mwenyewe. Huyo hawezi kujitoa kafara Kwa ajili ya Familia. Huyu anaweza kuwalisha Dagaa wa chukuchuku wewe na watoto lakini lenyewe linakunywa Bia na supu huko nje. Haya unayakuta yamenenepa na kukuza vitambi alafu wake zao dhoofu ilhali.


Usilivumilie! Likimbie! Hata Kama halijakufukuza ndani ya ndoa liache hapo, usiishi na Mwanaume Mpumbavu ndani ya nyumba.

Mara nyingi nawasema wanawake wapumbavu kuwa tusiwavumilie lakini leo nasi wasituvumilie.

Wewe jitu likulishe Dagaa miezi nenda Rudi aalafu lenyewe linakula nje na kunenepeana bado unalichekea.
Hakuna kulirekebisha, hiyo sio kazi yako, Kama halikurekebishwa na wazazi wake huko basi liende kanisani au msikitini huko ndio wanalipwa zaka na Sadaka Kwa kazi za namna hiyo. Hakuna kuchekeana na wapumbavu.

Mwanaume atakayekupiga bila sababu zile kubwa kubwa Kama kukutwa unataka ku-cheat, au ukiwa una-cheat, au mwanamke mwenyewe kutaka kupigwa maana wapo wanawake wanakuwaga wanawashwa washwa.

Lakini jitu limekukosea unaliambia Kwa adabu alafu linakupandia na kukupiga. Usilichekee. Piga chini. Usicheke na Mwanaume Mpumbavu.
Yaani lije limechelewa nyumbani, linanuka pombe, linatukana hovyo hovyo, ukiliuliza imekuwaje linajibu kipumbavu "hapa ni kwangu" na majibu ya mengine ya hovyo. Kisha likakojoe huko chooni au kutapika hovyo hovyo, bado likupige, loooh! Hakika ukiishi na Mwanaume WA hivyo nawe ni Mpumbavu tuu.

Kupenda upumbavu ni Dalili ya kichaa.

Mimi huwaga nawaambia Dada zangu na pia nitawausia binti zangu hayo wasiyachekee. Wasicheke na Kima, mwanaume Mpumbavu hachekewi muwashie Moto mpaka aone dunia chungu. Usimuhofie, akizingua mlete kwetu tumnyooshe kisheria.

Ewe binti usiyaogope maisha ikiwa unamikono na miguu na akili timamu. Ni Bora uishi mwenyewe kuliko kuishi na Lofa na lipumbavu likakuchosha mwili na Akili.

Mtu Kama hakuheshimu wa nini?
Mtu Kama hajiheshimu Kwa nini umheshimu?
Mwanaume sio Mungu, Ila ni mungu mdogo endapo atafanya wajibu wake Kwa hekima na akili.

Usitishwe na Motherboard yake Kama ndani yake ni Mwanamke.

Binti zangu, msitishwe na wanaume wapumbavu wasiojielewa. Bali Tishweni na wanaume wema, wenye akili na hekima, wanaojiheshimu na kuwaheshimu, wanaomheshimu Mungu. Hao wakiwaoeni hao watiini na kuwasujudia ikibidi Kwa maana HAO ni Kama mungu kwenu.

Lakini hawa Mbuzi wasiojielewe msipoteze muda nao. Msiwakawize, wawashieni moto mpaka waelewe.

Kama nilivyowaandikia na Kuwafunza ndivyo mtakavyofanya.

Mimi Baba Yenu,

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa, MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM
Kunywa soda kwa Mangi nitalipa
 
Kuna mengine umeongea sawa , kuna mengine umeongea kwa mihemuko na kudhihirisha upumbafu wako [emoji817] " kaa ujitafakari wewe mpumbavu
 
Mlivyokuwa mkidanganyana chuoni Leo hii mwenzako unamuona mpumbavu??

Nawakumbuka sana nyie watu pale chuo cha uhasibu tawi la singida mlikuwa mkilinga sanaaa.
 
hakuna mwanamme mpumbavu tambua hilo halafu kwa ufupi mwanamke bora anayetambua maana ya ndoa hawezi kufuata mali hatawewe hukuzaliwa na mali tambua hilo raha ya ndoa mtafute pamoja ilimuheshimiane mwanaume kupendeza inategemea makuzi yake siyo ukiwa mchafu ndiyo mfanya kazi, kuwbuka wale wanao pata mali za urithi ni wasumbufu sana . Sasa wewe mwanamke kaolewe na mtu wa aina hiyo uone utakavyo semwa majina yote utaitwa na hapo ndipo utakapo juwa mwanaume mwenye mali ndiyo wako au laa tafutandoa yako kwa msaada wa mungu na siyo kwa mtazamo wa binadamu .
 
hakuna mwanamme mpumbavu tambua hilo halafu kwa ufupi mwanamke bora anayetambua maana ya ndoa hawezi kufuata mali hatawewe hukuzaliwa na mali tambua hilo raha ya ndoa mtafute pamoja ilimuheshimiane mwanaume kupendeza inategemea makuzi yake siyo ukiwa mchafu ndiyo mfanya kazi, kuwbuka wale wanao pata mali za urithi ni wasumbufu sana . Sasa wewe mwanamke kaolewe na mtu wa aina hiyo uone utakavyo semwa majina yote utaitwa na hapo ndipo utakapo juwa mwanaume mwenye mali ndiyo wako au laa tafutandoa yako kwa msaada wa mungu na siyo kwa mtazamo wa binadamu .

😊😊😊
 
Back
Top Bottom