Kayombo Tips
JF-Expert Member
- Jun 19, 2020
- 461
- 574
Wakati tunapokea taarifa za uteuzi wa Uwaziri wako bwana January Makamba, watu wengi tuliamini kuwa wewe ndiye utakaye leta mageuzi makubwa sana kwenye Wizara yako. Lakini nasikitika kuona kuwa matarajio tuliyo kuwa nayo kwako yamepotea.
Ulipoteuliwa tu na kuapishwa ulionesha mwelekeo kwamba changamoto za nishati zitapungua sana badala yake changamoto hizo zimeongezeka zaidi.
Umeme umekuwa una katika mara kwa mara, bei ya gesi imezidi kuongezeka zaidi. Licha ya ahadi zako nyingi ulizotoa mara ulipoteuliwa kuwa Waziri wa Nishati ila hakuna hata ahadi moja uliyotekeleza. Zaidi sasa hivi umekuwa mtu wa kuja na matamko yanayopingana na ahadi zako ulizotoa.
Sasa hivi ukiulizwa kwanini umeme unakatika mara kwa mara unajibu kuwa tatizo ni mitambo ya zamani haikufanyiwa matengenezo kwa muda mrefu sana. Mara unajibu kuwa matatizo ya umeme kukatikakatika yataendelea kuwepo. Sasa kwa kauli zako hizi huoni kama unapata sifa ya kuwa kiongozi uliyeshindwa.
Sisi Wananchi hatutaki kusikia maneno ya kuwa umeme utaendelea kukatika mara kwa mara, tunataka kusikia majibu ya namna utakavyo ondoa tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Ulionekana kama kijana ambaye tulikuwa tunatazamia siku moja utakuwa Mkuu wa Nchi ila umeonesha kushindwa kiuongozi. Tabia yako ya kubadilisha badilisha kauli ahadi zako inaonesha kabisa hufai kuwa Mkuu Wa Nchi kwa siku za mbeleni.
Wananchi huu ni muda wa kuwa tazama kwa umakini viongozi vijana waliopewa dhamana ya kiuongozi kuona wanavyotusaliti ili kama siku moja wanatamani kushika nafasi ya juu tujue mapema hawatufai na kwamba ahadi wanazotoa siyo sahihi.