Barua ya wazi kwa waziri wa elimu mh. Mulugo

Joined
Jan 14, 2014
Posts
38
Reaction score
12
Mh; Waziri napenda kukutumia barua ya wazi kutokana na kukosa namba yako ya simu.

YAH;MIZENGWE KATIKA NAFASI ZA WATOTO WALIO FAULU NA KUTAKIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA.

Rejea kichwa cha habari hapo juu ,mimi ni Mzazi wa mtoto IRENE FRANK MICHAELI,mtoto aliye kuwa akisoma katika shule ya KIVULINI iliyopo kisesa Magu Mwanza ,mtoto huyu alifauru kwa average GRADE A, Kwa mtililiko huu,Kiswahili B,English A ,Maarifa B ,Hisabati B ,science B .Mtoto huyu alipagwa katika shule ya wasichana Tabora ,chakusikitisha juzi tulipo kwenda shuleni hapo tulikuta jina lake limeondolewa kinyemela,tukalazimika kurudi Mwanza tulipo fika Mwanza tulikwenda katika ofisi ya Afisa elimu Mkoa ,Afisa elimu mkoa alituelekeza twende kwa Afisa elimu Wilaya ya Magu ,leo asubuhi tumekwenda Magu tumekuta nafasi ya mtoto wetu imeporwa,tulipo hoji waka twambia tulete ushaidi kama alipangwa Tabora. Mh.Waziri kama unavyo jua matokeo na mahali ambapo watoto upelekwa ubandikwa kwenye kuta ama kwenye mbao za matangazo ambavyo kwanza ni kosa kisheria kubandua tangazo la serikali,pili matokeo na alocation izo zimeisha banduliwa je huu ushaidi wanao utaka niutoe wapi?.Pili kwanini wamepora nafasi ya mwanangu.Mh;Waziri nakuomba uchunguze swala hili kwani kuna watoto wengi wameisha fanyiwa hivi ,mwisho warejeshe nafasi ya mwanangu na wafahamu haki uwa aipotei yaweza cheleweswa.Nategemea utanijibu kupitia ukurasa huu ama kwa barua pepe kaijuko@yahoo.com.

Nikutakie shuguli njema
 
Tovuti ya wizara haina wanafunzi walipopangiwa, tumsaidie huo ushahidi wadau
 
POLE SANA kwa dhahama iliyo kukuta, cha kukushauri nenda wilayani ukauulizie nakala ya matokeo kwa afisa elimu wa s/msingi. Maana kama yalibandikwa basi anaweza akawa na soft copy ambayo anaweza kuigonga mhuri kuidhinisha penye jina la mwanao.
 
Tuweke kumbukumbu sawa, Mh. Mulugo ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
 
Duh,
uspostajaabu ya Musa, utayaona na Filauni.
......HUU NDO UFISADI WA SERIKALI.
 
pole sana kwa dhahama iliyo kukuta, cha kukushauri nenda wilayani ukauulizie nakala ya matokeo kwa afisa elimu wa s/msingi. Maana kama yalibandikwa basi anaweza akawa na soft copy ambayo anaweza kuigonga mhuri kuidhinisha penye jina la mwanao.

kweli mkuu
 
Pole sana ndugu yangu! ushauli nenda ufisi ya almashauli ya wilaya kule utayakuta matokeo huwa wanakuwanayo kwenye softi kopi "naamini utafanikiwa":majani7:
 
hivi ulimaliza darasa la saba ukiwa unajua kusoma na kuandika vizuri? Hufai kuwa hata mwenyekiti wa kitongoji
 
pole kaka ilinikuta 2007 walioona tangazo la matokeo waliniambia nimechaguliwa mtwara tech nikapelekwa kata nashukuru huko nilipasua
 
Pole sana mzazi. Komaa sana, na mwishowe wasije kufariji kumpangia mwanao shule za kata. Komaaa arudi Tabora girls!
 
hivi ulimaliza darasa la saba ukiwa unajua kusoma na kuandika vizuri? Hufai kuwa hata mwenyekiti wa kitongoji

Acha kumponda jamaa...toa mawazo ya kumsaidia huyu mzazi...ata ivo alichoandika mbona kinasomeka tu!
 
Mh; Waziri napenda kukutumia barua ya wazi kutokana na kukosa namba yako ya simu.

YAH;MIZENGWE KATIKA NAFASI ZA WATOTO WALIO FAULU NA KUTAKIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA.

Rejea kichwa cha habari hapo juu ,mimi ni Mzazi wa mtoto IRENE FRANK MICHAELI,mtoto aliye kuwa akisoma katika shule ya KIVULINI iliyopo kisesa Magu Mwanza ,mtoto huyu alifauru kwa average GRADE A, Kwa mtililiko huu,Kiswahili B,English A ,Maarifa B ,Hisabati B ,science B .Mtoto huyu alipagwa katika shule ya wasichana Tabora ,chakusikitisha juzi tulipo kwenda shuleni hapo tulikuta jina lake limeondolewa kinyemela,tukalazimika kurudi Mwanza tulipo fika Mwanza tulikwenda katika ofisi ya Afisa elimu Mkoa ,Afisa elimu mkoa alituelekeza twende kwa Afisa elimu Wilaya ya Magu ,leo asubuhi tumekwenda Magu tumekuta nafasi ya mtoto wetu imeporwa,tulipo hoji waka twambia tulete ushaidi kama alipangwa Tabora. Mh.Waziri kama unavyo jua matokeo na mahali ambapo watoto upelekwa ubandikwa kwenye kuta ama kwenye mbao za matangazo ambavyo kwanza ni kosa kisheria kubandua tangazo la serikali,pili matokeo na alocation izo zimeisha banduliwa je huu ushaidi wanao utaka niutoe wapi?.Pili kwanini wamepora nafasi ya mwanangu.Mh;Waziri nakuomba uchunguze swala hili kwani kuna watoto wengi wameisha fanyiwa hivi ,mwisho warejeshe nafasi ya mwanangu na wafahamu haki uwa aipotei yaweza cheleweswa.Nategemea utanijibu kupitia ukurasa huu ama kwa barua pepe kaijuko@yahoo.com.

Nikutakie shuguli njema
Wana jf, nimesikitika sana, kesho nitafuatilia kwa Kamishina wa Elimu au Idara ya Elimu ya Sekondari, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili nijue ukweli. Nitaleta majibu hapa. Nijuavyo, siku ya kutangaza matokeo huwa kuna mwakilisho wa Wizara ambaye huondoka na nakala za vitabu kuvipeleka Wizarani. Tutapata majibu hapo.
 
Back
Top Bottom