Barua ya wazi kwa Zitto Kabwe: Jitoe kwenye Kamati ya Msajili wa Vyama vya Siasa, hana nia njema

Barua ya wazi kwa Zitto Kabwe: Jitoe kwenye Kamati ya Msajili wa Vyama vya Siasa, hana nia njema

Kuna watu wamesusia mchakato kimwili tu ila akili imegoma kususia ndio sababu hawaachi kufuatilia kila kinachoendelea
 
Zitto na timu yake wapuuzwe.

Jitihada mbadala za kudai katiba mpya yenye maslahi kwa wananchi zishike kasi zaidi.

Vibaraka, opportunists, na wenzao tukutane mbele ya safari panapo Majaliwa tukiwa na katiba na tume sahihi.
 
Tukienda na akili hizi za KICHADEMA CHADEMA hatuwezi kufanikisha jambo lolote! Kuzira zira kila jambo, HAPANA!
Kila jambo lazima liwe na mahali pa kuanzia na lack of these skills inawagharimu sana CHADEMA!
Zitto Kabwe piga kazi na hiyo time ya Jaji Mutungi ni nzuri!
Tunasubiri mapendekezo yenu ambayo mtatoa kwa ajili ya kupelekwa kwenye mkutano wa TCD!
Tatizo tuna watu wajuaji ambao "HAWAJUI HAWAJUI".
 
Ndugu Zitto Kabwe, Kiongozi wa chama cha ACT

Pole na majukumu ya kazi zako. Nakuandikia hii barua ili mimi na wewe tuweze kureason, na kuchukua hatua sahihi ya kisiasa inayoendelea nchini kwa manufaa ya usitawi wa demokrasia nchini.

Mheshimiwa, Zitto
Mimi binafsi ni miongoni mwa watu waliokupa benefit of doubt, pale chama chako na wewe mlipoamua kushiriki kikao cha msajili katika kile walichotuaminisha kuwa ni kutafuta muafaka wa kisiasa nchini. Na nilikuunga mkono kuhudhuria kwa sababu zifuatazo:

1. Wewe ni kiongozi wa TCD, Tanzania center for democracy, kwa hiyo ingekuwa ajabu majority ya wanachama wako wawe interested kuhudhuria halafu wewe mwenyekiti wao usiende

2. Pili ACT ni chama chenye maamuzi yake yatokayo vikaoni, kama chama kimeamua kinashiriki, basi kiongozi wake atake asitake itabidi atii msimamo wa chama

3. Kutofautiana katika falsafa za namna ya kutafuta solution, ni jambo la kawaida. Kwamba baadhi wanaweza kuamini katika disengagement na wengine wakaamini katika engagement.

Kutokana na nukta hizo juu, binafsi niliiona nia yako njema na niliunga mkono ushiriki wako.

Ila sasa, baada ya Msajili kutengeneza timu yake hii ya kuchakata maazimio, binafsi ninaona yafuatayo:

1. Msajili hana nia njema
Timu ya Msajili imejaa watu ambao kwa misimamo yao, mienendo yao ni watu ambao misimamo yao ni ya kuunga mkono mitizamo CCM na serikali za CCM.

Majority ya timu ile ya msajili, hawajawahi kukemea hata mara moja uvunjwaji wa demokrasia nchini. Infact wapo watu on record, wakitoa kauli huko nyuma za kudogosha hitajio la kikatiba la kutoa haki za kisiasa kwa vyama zilizoko kikatiba. Je kuna maajabu gani unadhani yatapatikana kwa kujiengage na watu wenye msimamo wa dhahiri wa kutopenda demokrasia?

2. Kiongozi wa BAKWATA na padri wanafanya nini ndani ya kamati?
Hii nchi haina dini rasmi, leo hii Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam anafanya nini kwenye kutafuta solutions za kisiasa za nchi yetu?.
Ukiachilia mbali hoja hiyo, Sheikh wa mkoa wa Dar misimamo yake inajulikana wazi toka wakati wa Magufuli, siku zote hajawahi kuwa mtu wa haki kwa makundi yote ya kijamii nchini. Siku zote amecaucus na serikali za CCM, na kauli zake za kuipa moral cover serikali hata inapominya haki.

Ukiwa na jicho la udadisi utaona msajili anataka kutumia viongozi hawa wa dini kama cover ya kutafuta kuaminika mbele ya umma, maana anajua watanzania wengi wanaheshimu dini, kwa hiyo anataka kuwatumia hswa kama greese ya kulainisha mambo yake.

3. Zitto wanataka kukutumia kujustify nia yao ovu ya kuminya demokrasia nchini.
Watawala wamegundua kutumia mabavu kuminya demokrasia ni unsustainable, sasa wanataka compliance ya vyama vya kisiasa kupitia vyama hivyo kwa kujua au kutojua ili vijikaange kwa mafuta yake yenyewe. Mheshimiwa Zitto, while wewe binafsi unaweza kuwa na NIA NJEMA, but inaonyesha wazi kuwa SERIKALI haina Nia njema kulinda demokrasia. Na ushahidi wa ukosefu wa nia njema ni Uundwaji wa Timu kama hii iliyokaa kilaghailaghai!. Sasa Ndugu Zitto jiulize, unataka kubariki mchezo huu?

4. Haki za msingi za kikatiba ni non negotiatable
Ni common sense kudiscuss vitu ambavyo bado havipo kikatiba kwa. mfano madai ya katiba mpya n. k. Lakini zile haki ambazo tayari ziko kikatiba na kisheria zinaundiwa Task Force ili iweje? - Huoni kwamba, hata kitendo chenyewe cha kukaa mezani, kujadili hilo suala ni matusi makubwa kwa wananchi?

Ndugu Zitto
Huenda wewe una nia njema, lakini imedhihirika serikali ya CCM inacheza game, haina nia njema. Sasa ni jukumu lako hilo kuliona na kufanya maamuzi. Ama ulegitimize nia ovu na mkakati ovu wa chama cha Mapinduzi, au uachane na huu. mchezo mbaya na hatari wa kujustify uminywaji wa demokrasia nchini.
Chadema waliuona huu mtego wakaukwepa, huyu genius zito anafeli wapi?
 
Tukienda na akili hizi cha KICHADEMA CHADEMA hatuwezi kufanikisha jambo lolote! Kuzira zira kila jambo, HAPANA!
Kila jambo lazima liwe na mahali pa kuanzia na lack of these skills inawagharimu sana CHADEMA!
Zitto Kabwe piga kazi na hiyo time ya Jaji Mutungi ni nzuri!
Tunasubiri mapendekezo yenu ambayo mtatoa kwa ajili ya kupelekwa kwenye mkutano wa TCD!
Tatizo tuna watu wajuaji ambao "HAWAJUI HAWAJUI".
Sasa twende na akili za majambazi ccm??

Tume huru halafu wajumbe woote wa ccm? Hivi nyie mkiwa huko ccm akilozote huwa mnawekez wapi?

Jaji Mtungi anapoteza muda wake na kujitekenya anacheka mwenyewe
 
Kuna watu wamesusia mchakato kimwili tu ila akili imegoma kususia ndio sababu hawaachi kufuatilia kila kinachoendelea

Una kiwango duni hivi cha ufikiri!? Tulipowasusia makaburu wa Afrika kusini tuliacha kufuatilia nyendo zao? Hatufuatilii kikao chao, tunafuatilia impact ya kikao chao kwenye mustakabali wa demokrasia ya nchi yetu.
 
Lakini kauli yake moja ambayo nimewahi kumwamini na alisema ukweli ni hii " usimwamini mwanasiasa yeyote"

Hapo hapo rafiki yangu mwingine akaniambia "politics is worse than prostitution"
" usimwamini mwanasiasa yeyote"

"politics is worse than prostitution"
😎
 
Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam aliwahi kumwambia Magufuli kuwa ni zaidi ya Yesu na Muhammad!

 
Dr Shoo na Sheikh Issa Ponda Issa wanakubalika kwa misimamo yao ya haki
Sheikh wa Dar ki ukweli hakubaliki kabisa na waislam...Zitto anajuwa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
H
Sasa twende na akili za majambazi ccm??

Tume huru halafu wajumbe woote wa ccm? Hivi nyie mkiwa huko ccm akilozote huwa mnawekez wapi?

Jaji Mtungi anapoteza muda wake na kujitekenya anacheka mwenyewe
Hiyo siyo tume huru ya uchaguzi bali ni kikosi kazi ( kamati) ya kupitia na kutoa mapendekezo ya kupelekwa TCD ili kujadiliwa na vyama vya siasa!
CHADEMA imejaza washabiki wajinga wajinga kweli! Katika siasa hamtafanikisha chochote kwa akili duni hizi!
 
Back
Top Bottom