Motowntzjpm
Senior Member
- Jun 16, 2023
- 134
- 203
Tanzania na Uwekezaji
Barua ya wazi kwa Mhe Kitila Mkumbo, Waziri wa Ofisi ya Rais Uwekezaji na Mipango
Mhe Kitila,
Hongera kwa uteuzi wako kuongoza Wizara hii muhimu.
Umepata ubatizo wa moto na sio mafuta kufuatia “ishu” ya uwekezaji kwenye Bandari na Seikali ya Dubai.
Nionavyo malumbano na mijadala inayoendelea imetupa mwanya na fursa ya kujifunza ikiwa tutakuwa tayari kwa ajili ya maswala mazima ya Uwekezaji endelevu ambayo Tanzania tunahitaji kwa maendeleo endelevu ya taifa letu.
Ninazo hoja kumi ambazo kwa mawazo yangu tunapaswa kuyanzingatia na kuyafanyia kazi.
01
Kilichobainika, ipo haja kubwa ya kuelimisha watanzania kwamba swala la uwekezaji haukwepeki. Uliiweka vizuri pale Mbeya kwamba serikali itaendelea kutoa huduma za jamii na vile vile kusimamia maswala ya ulinzi na usalama.
Inayoambatana na namba 02 utajiri wote wa rasilmali zetu tulizozikuta tutafaidika tu ikiwa tutafanya kazi. Mito, milima, dhahabu, almasi , gesi asilia na Tanzanite hazitogeuza watanzania wote matajiri bila sote kufanya kazi. Bahati mbaya baadhi ya viongozi wanaendekeza dhana hili potofu.
02
Watanzania wengi wanaimani potofu kuhusu uwekezaji . Imani hii imechangiwa kwa maoni yangu na historia la kijamaa ambayo iliaminisha watu kwamba akiondoka mkoloni tutalamba asali na kunywa maziwa . Swala la kazi lilitamkwa lakini halikuendelea kupewa umuhimu yake matokeo yako wengi wanadhani kuna maisha mazuri bila kazi.
Namba 03
Kuendelea kuendekeza propaganda inahatarisha muungano Jumuiya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika. Hii pia ni changamoto kwenye uwekezaji kwa kuwa kila tukiwa na changamoto ya ndani tunatafuta mchawi nchi jirani. Kwenye hili la bandari waliomshauri Raisi wamemuingiza chaka kwamba Kenya wameenda Dubai kwa kuwa tunalumbana wakati la kwa ilikuwa 2019.
04
Siasa za umajumuhi wa Afrika zilikuwa na umuhimu wake na umuhimu huo bado upo.Lakini, tunahubiri maziwa na kunywa mvivyo. Haiwezekani sisi tunaohubiri umajujumuhi wa Afrika kila kukicha tunahubiri hiki au kile kinachohusu Afrika Mashariki au Afrika ambacho hatukubaliani nacho kisa utanzania wetu.
05
Ni bayana kwamba Muungano unamatatizo makubwa. Muungano ungetusaidia kuongoza muungano wa Afrika lakini kama minunguniko na sauti nyingi ya mgongano tunazosikia ni ishara ni bora sasa tukajadilia kwa lengo la kutatua matatizo.
06
Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba alitamka bungeni kwenye hotuba yake ya Bajeti 2023-2024 kwamba watanzania hususani watendaji wanakautaratibu wa kukatisha wawekezaji tamaa. Yule ana hela , ataweza nini hili eneo linahitaji elimu kubwa kwa kuwa wananchi wenyewe nao tuko vivyo hivyo.
07
Tumefukuza Citi water Neo Technologies na kadhalika. Matamshi yako hayo ni hatari kwa uwekezaji. Ukweli ni kwamba kila mkataba sharti uwe na vipengele vya kuondokana na mkataba huo.Tulichokiana kwenye mgorogoro wa Feisal Toto na Yanga ndivyo ilivyo kwenye mikataba yote. Kila upande unaweza kuamua kujiondoa kwa sababu zake ikiwemo kutoridhikia au kujiondoa kwa kununua mkataba.
Tusiwaaminishe watanzania kwamba tulifukuza na kwamba tutafukuza kwakuwa hili lina athari mbili.
Kwa Watanzania kwenye kila uwekezaji tutakuwa tunataka wafukuzwe kila tukikwazika na jambo. Kwa utaratibu huo hakuna uwekezaji unaoweza kudumu
Kwa wawekezaji hofu ya uwekezaji utapanda na itachukua muda mrefu kufuta hiyo hofu.
Tujitahidi kujuza watanzania kwamba kila mkataba una utaratibu na upande wowote ule Jamhuri au mwekezaji asio ridhika anajiondoa au anaomba mkataba uvunjike. Ukiukwaji wa taratibu unavunja mkata automatically na jamhuri hukiuka mingi mikataba tusidanganyane.
08
Uzawa/Utanzania usichanganywe na utendaji uliotukuka. Tusitumie utanzania kama chka la uovu kwenye maeneo ambayo kinachohitajika ni utendaji uliotukuka. Mitandao ya kijamii imejaa malalamiko kuhusu utendaji kwenye sekata ya afya na elimu na malalamiko hayo yanahusu utendaji wa watanzania wenzetu. Mabasi yaendayo kasi na kwingineko kote tumeharibu wenyewe. Panapohitajika tuenzi utendaji ulio tukuka.
09
Uwekezaji ni ubia kati ya SJT na sekta binafsi. Mfano kwenye gesi asilia serikali inayo gesi. Sekta binafsi inaleta rasilmali fedha, rasilmali technolojia na watu wenye weledi. Kama ulivyosema serikali inahitaji sekta binafsi kwa kuwa haina vitu hivyo sekata binafsi inavyo.
Inatulazimu kuingi mikata inayoheshimu na kulinda maslahi ya pande zote na sio kuaminisha watanzania sisi tunauwezo wa kufukuza wawekezaji holela holela.
10
La mwisho sio kwa umuhimu sharti turuhusu mahakama yetu iheshimike kama muhimili ili kukiwa na jambo la utafutaji wa haki wawekezaji wawe na Imani na Mahakam zetu. Sasa hivi mifano ni mingi ya kesi za utafutaji haki zinazopelekwa kwenye Mahakam ya nchi zingine kwa kuwa ya kwetu haviaminiwi hali ambayo tumechachia sisi wenyewe kwa kauli na kutoheshimu maamuzi ya mahakama.
Wakuu wa wilaya na mikoa kutoa matamko ya ovyo hawana nafasi kwenye uwekezaji. Hakuna mkataba unaoruhusu mwekezaji kuwekwa lock up kisa mradi umechelewa . Usuluhishi ndio njia pekee.
Tujirekebishe na tuipe taifa heshima yake

Upvote
1