Barua ya wazi kwako IGP wetu Simon Sirro

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
525
Reaction score
2,950
Pole na majukumu mazito IGP Sirro kwa kutufanya angalau kuwa salama katika nchi yetu hadi sasa.

Mimi ni mtanzania ambaye tumewahi onana mara mbili tuu,mara ya kwanza ni ITV malumbano ya hoja ukiwa kamanda Kanda maalumu ya Dar,tukijadili uuzwaji wa visu,mishale barabarani (silaha),mara ya pili tulionana Nkurumah-UDSM ulipo kuja kuongea na wanafunzi hasa wale kutoka "law enforcement" (UDSOL).

Nilikupa taarifa juu ya RPC wa mwanza Kipindi hiko alipo nitishia kunishtaki kwa kuwaumbua polisi walio kula rushwa na kuficha ficha kesi katika kituo cha Nyamagana.Na nina shukuru Deputy IGP alilifanyia kazi.

Nadhani umenikumbuka kidogo.

*IGP Sirro*,tunajua jukumu lenu kubwa ni kuhakikisha tuna amani ya kutosha nchini kwetu.Na hayo hufanyika kwa kutulinda na kuzuia viashiria vyote vya uvunjifu wa amani.

*IGP Sirro*,tukumbuke usawa na haki yaani (Justice and equality ) ni matunda ya amani , viashiria vikuu vya uvunjifu wa amani hutokea pale usawa na haki kuanza kufifia.Haki na usawa huimarisha Amani.Kulinda na kuhubiri Amani bila kuangazia haki na usawa ni kazi bure.

*IGP Sirro* nakupa mfano,nchi ya china kuna mfumo tofauti sana na wetu ,china huwezi kutenganisha shughuli za serikali na chama,au waajiri wa serikali na chama. Kuna wafanya kazi wanaolipwa na serikali huku wakifanya kazi ya chama na serikali , hutambulika kama (The Apparatchiki) hivyo mfumo wa china ni *Fused party state Apparatus* .Nitofauti kabisa na mifumo yetu Tanzania.

*IGP Sirro*,Tanzania hapa kuna mfumo wa vyama vingi ,hivyo hatuna mfumo wa *Fused party state Apparatus* ,ndio maana ukisoma ibara ya 147 (3) ya katiba yetu inakatataza kabisa *Member of security forces to join to any political party* inakataza police kujiunga na chama chochote isipokuwa ibara ya 5 kupiga kura tuu.

*IGP Sirro* ,Ibara hiyo ni pana imeficha maneno mengi sana,ina kataza police hata kuwa affliated (kuhusishwa) na chama fulani.

*IGP Sirro* Tumeshudia police wakikataza mikutano kwa kusema ni katazo la Mh. Rais hakuna mikutano hadi uchaguzi kinyume na sheria zetu,wengine wakikamatwa .Huku chama tawala kikifanya mikutano popote na muda wowote.

*IGP Sirro* Tumeshudia Polisi wakionekana mbele wakilinda Maandamano ya chama tawala na yale ya kupongeza, huku watu au vyama vingine vikikatazwa Maandamano yaliyopo kwa mujibu wa katiba.

*IGP Sirro* tumeshudia Polisi wakiingia katika mikutano ya chama tawala na kuimba nyimbo za kusifia chama tawala wazi wazi .

*IGP Sirro* Tumeshuhudia Polisi ikiwa mstari wa mbele kuwinda na kukamata wakosoaji wa serikali mara nyingi sana.

*IGP Sirro* Tumeshudia matukio ya uvunjivu wa haki za binadamu dhidi ya Raia wa Watanzania ,ila hadi Sasa hakuna uchunguzi wowote na kila jambo ,Jeshi hubeba kisiasa na kulidogodesha hatimaye kufukiwa hata muda mwingine kutoka kauli za kukinzana katika tukio moja.

*lGP Sirro ,Je unajua athari ya haya ?*

*IGP Sirro* Ipo hivi , moja ya report ya machafuko ya Kenya 2008 inaitwa *Ballots to Bullets report* na ile ya *Kenya National task force on police reforms* iliyokuwa chini ya
WAKI- Commission reports au CIPEV (commission of inquiry into post election) ikiongozwa na Judge Philip Waki .

Ilisema hivi *Many Kenyan have little faith in police to act in a professional , impartial,and timely manner ,this reality only encourages the vigilantes to take the law into their own hands*

Ilisema wananchi walipoteza imani na police katika kufanya kazi kwa taaluma zao ,hivyo wakajichukulia sheria mkononi.

*IGP Sirro* Hili ndilo linalosubiriwa Tanzania IGP kama hatua stahiki hazitachukuliwa.Raia wakiendelea kuona hakuna haki na usawa hata kwa vyombo vyao vinavyo aminiwa (Jeshi la police), vyombo hivi kuendelea kuonesha upendeleo wa wazi wazi .

*IGP Sirro* Hakika kuna siku wananchi watasukumwa na hasira,hisia za kuchoka na watachukua hatua na maamuzi yao binafsi bila kujali athari.(Acting out)

Binadamu ni mvumilivu wa muda na mpole(rational being),kuna kipindi hufikia mwisho wa uvumilivu na huweza fanya chochote bila kujali athari yake Segmund Freud anaita hii ni *psychological Defense mechanisms* (Act out ) atafanya tukio analoona ni (jema) good will dhidi ya mfumo au ukatili ,ubaguzi na uvunjifu wa haki bila kujali athari ili atoke katika suppression anayoipata yeye hata wengine (Segmund huita hii *Altruism* ).

*IGP Sirro* Tanzania jeshi letu linaingizwa sana katika siasa kipindi hiki *Politicization of police * ,jambo hili linaweza kuleta athari kubwa baadaye ,hasa pale wananchi au wanachama wa vyama vingine wataamua kujilinda na kuonesha kuchoka dhidi ya ubaguzi na manyanyaso wanayofanyiwa tofauti na chama tawala.

Hakika IGP hii itakuwa hatua mbaya sana.

*IGP Sirro* Kenya walilitambua hilo kwani *Waki Report* ilisema hivi *polisi walikuwa wakitumika na watawala hivyo kupelekea kuto aminiwa tena na Raia ,Raia wakaanza chukua sheria mkononi*, Hii ilipelekea mageuzi makubwa (reforms) katika jeshi la polisi ili kuepuka jeshi kuingiliwa na wanasiasa na hata kuepuka machafuko mengine.

Mabadiliko (Reforms)kadhaa yalifanywa. Upande wa polisi vyombo 3 viliundwa.

*IGP Sirro*, kwanza ,kuliundwa Independent Police commission (act of 2011)(mwenyekiti ni jaji ,na mafisa wastafu ngazi ya juu jeshi la polisi,na wengine), majukumu kuajiri polisi na hata IGP huteuliwa na Rais kwa kufuata mapendekezo ya commission hii,pia kuchunga ni dhamu ya police.

Pili,Baraza la Taifa la police

*IGP Sirro* kuliundwa Mamlaka huru ya kuchunga na kudhibiti mienendo na matendo ya polisi (Independent policing oversight Authority ) Act 2011. Mamlaka hii ipo huru mwenyekiti ni Jaji, viongozi wa haki za binadamu, viongozi wa dini, viongozi wa utawala wa umma. Huangalia mienendo ya polisi wana mamlaka ya kuchunguza malalamiko,kutoa mapendekezo kwa police na kulazimisha utekelezaji wa mapendekezo hata kwa kwenda Mahakamani,kukataa kutekeleza mapendekezo yao ni kosa la jinai (criminal offence).

*IGP Sirro* ,ukiangalia mifumo hii ya Kenya na yetu unaona kabisa ,sisi bado tupo nyuma sana ,lakini hata kama mifumo yetu haipo imara bado wewe kama IGP una nafasi kubwa kutumia mamlaka yako kuwawajibisha police wote wanachochea ubaguzi,upendeleo katika utekelezaji wa majukumu yao.

*IGP Sirro* unao wajibu wa kuagiza upelelezi imara wa matendo yote ya uvunjivu wa haki za binadamu,pia kujitenga na maagizo yote ya kisiasa yanayoingilia taaluma yenu.

Najua, *IGP Sirro* uliteuliwa na Rais na ni Rais anayeweza kukutengua muda wowote ( ibara 148 (a) 2 ,hivyo labda unaweza kuwa na hofu ya kuondoka katika nafasi yako hivyo ukafumbia macho matendo yasio ya kibinadamu au ubaguzi katika siasa,hata kutumika kuvunja misingi ya Demokrasia.

*IGP Sirro* ,Ukizidi kufumba macho tujue tuna fuga bomu chumbani siku litaripuka madhara yake yatakuwa makubwa.

*IGP Sirro* Binadamu ambao ndio Raia, anaye wajua ni Mungu tuu,na anaowaweza ni Mungu.Siku wakichoka haya hatutaamini macho yetu.

IGP Sirro, Tafadhali angalia tena , Mienendo ya Jeshi letu kujua tatilipo ,ondoa Jeshi Mikononi mwa wanasiasa ,Ni dharau kubwa jeshi letu kuweka taaluma pembeni.

Mwisho , *IGP Sirro* ukisoma ibara ya 147 ,148 hata Ile sheria ya POLICE FORCE AND AUXILIARY SERVICES

Naona tunatumia sana Neno "POLICE FORCE" kwanini tusitumii neno *service* *Tanzania police service* inaweza kusaidia wanaolitumia jeshi letu vibaya na kisiasa, wataona aibu kwa Kuona neno *service* (huduma) sababu nyinyi mnatoa huduma ya ulinzi na amani na usalama wa Raia ,mambo ya Force ni ya kikoloni ,Kenya tayari 2009 neno Force walibadili sasa hivi ni *KENYA POLICE SERVICE*

Shukran sana.

Nisikuchoshe sana ,jioni njema.


Abdul Nondo.

abdulnondo10@gmail.com
 
Ujumbe murua kwa Chief of National Police

Mi nasema wapigwe tu, awashughulikie kweli kweli
 
Umemkumbusha vizuri ila umesahau kumwomba aondoe alama ya polisi wetu yenye jembe na nyundo ambayo ni alama ya chama cha siasa.
 
Mkuu Abdul Nondo, kwanza naunga mkono hoja, pili umenigusa sana ulipomtaja Sigmund Freud na Altruism.

Tukija kwenye hili suala la uvumilivu una mwisho, kwa vile wewe Abdul bado ni kijana mdogo, unaamini katika theories mnazofundishwa shuleni na vyuoni kuwa binadamu ni mvumilivu na uvumilivu una mwisho. Hizo ni theories tuu na ziko applicable huko kwingine, lakini sisi Watanzania ni very special people or tuseme we are unique, Watanzania ni wavumilivu sana na siku zote, huwa tunavumilia tuu, uvumilivu wetu ni wa milele, hauna mwisho ndio maana CCM itatawala milele.
P
 
Umemkumbusha vizuri ila umesahau kumwomba aondoe alama ya polisi wetu yenye jembe na nyundo ambayo ni alama ya chama cha siasa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hayo yote uliyosema IGP anayajua, ila katiba haimpi nafasi ya kufanya unachoshauri. Kama rais alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi mbele ya CDF, huyo IGP ni nani? Kamuulize Mangu kilichomfanya atolewe kwenye uIGP. Katiba ndio inayomgeuza IGP kupelekwa kama gari bovu na wanasiasa. Na akilogwa akafuata huu ushauri wako, ataishia kusoma magazeti makao makuu, na hicho cheo atapewa mtu wa ndio mzee. Analinda maslahi yake binafsi sio haki.
 
Safi sana, Ujumbe upo nyuzi 360,tena bila matusi wala kejeli Hongera Mkuu @Abdulnondo
 
awali ya yote naunga mkonyo hoja a samahani naumga mkono hoja kuna askali anafanya kitengo kwa RPC hapa Mbeya alikuwa katibu wa ccm tawi LA SAUT Mbeya na siku ya uchaguzi alileta defenders na mapoti kibao kumpa Ushindi mgombea wa ccm bwa mahimbo Bahati ilhali alibuluzwa na mwana ufipa havillah mmali paka sasa ni mwana ccm na kapandishwa cheo tola private now officer in RPC office hahaaaaa policeccm nondo utayaona mengi tu
 
My friend you shouldn't be wasting your precious time to lecture the guy, he probably knows better than you do. Instead you should be addressing motivations and root causes of why this impunity? And simple answer is as a country we have wrong system of governance, period! And simple solution is radical reform of governance system that begins with writing new constitution, nje na hapo expect no change.
 
Ujumbe murwaa!
Lakini hapo ni Sawa na kuambiwa upake rangi upepo!

Ova
 
Naona wengi tumeishia kusema Siro anajua, ni kweli anayajua tena vizuri lkn tena nami naamini Nondo naye anajua kuwa Siro anajua haya yote na chanzo chake ni nn.

Pamoja na hayo yote nafikiri Nondo ameamua kumkumbusha kamanda Siro kama waumini tukumbushwavyo juu ya dhambi na wachungaji /mashehe wetu. Hakika Siro ajue yeye ni miongoni mwa watu wachache sana wenye kuweza kuleta matumaini na haki nchi hii. Dam za watu zinamlilia na hakika atafakari ubinadam na taaluma yake.

Kusema tatizo si Siro bali ni mfumo nakubaliana na hili. Lkn ili tutoke lazima tuanze na watu tena wachache. Siro anauwezo wa kutuanzishia hii safari ngum. Sema tu kuna mgogoro wa masrahi na Mali pia cheo, kweli si rahisi lkn inawezekana.

Kwa mara ya kwanza naomba kupingana na mayala tena kwa sehemu kubwa sana. Nafikiri pia harufu ya madaraka na vyeo imeanza kumlevya, tena kwa kasi kubwa kupindukia. Hakuna Subira isiyo tamati hususani kama hakuna heri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…