Kahangile
New Member
- Sep 1, 2025
- 3
- 2
Barua ya Wazi
Na: Mteule G. Kahangile
Musoma, MARA TZ
10 Novemba 2025
KWA:
* VIONGOZI WA SERIKALI,
* VIONGOZI WA VYAMA VYOTE VYA SIASA,
* VIONGOZI WA DINI ZOTE.
Ndugu Viongozi,
YAH: WITO WA MARIDHIANO NA MAZUNGUMZO KWA AJILI YA TAIFA
Kwa moyo wa kizalendo na nia njema ya kuona taifa letu likisonga mbele kwa amani, mshikamano na maelewano ya kitaifa, ninatoa wito huu kwenu ninyi viongozi wetu wakuu.
Nashauri wakutane katika meza ya mazungumzo, tukitanguliza utaifa na ustawi wa Tanzania kuliko tofauti zetu za kiitikadi au kimtazamo.
“Tujenge nyumba moja, si busara kugombania fito.”
Hekima hii itukumbushe kuwa tofauti si sababu ya mgawanyiko, bali ni nafasi ya kujifunza, kuelewana na kujenga kwa pamoja.
Viongozi wa kisiasa wanapaswa kuwa tayari kuweka tofauti zao pembeni kwa ajili ya kulijenga taifa. Viongozi wa dini nao wachukue nafasi yao kama watu wa kati, wasuluhishi, na daraja la maridhiano.
Maandiko Matakatifu yanasema:
“Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Mathayo 5:9
“Na shaurianeni katika mambo yenu; kisha mkisha azimia, mtegemee Mwenyezi Mungu.” Qur’an, Surah Ash-Shura (42:38)
Tukubaliane katika tofauti zetu kwa sababu amani ya kweli hujengwa katika haki, na haki huimarishwa kwa mazungumzo ya wazi na ya heshima.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mola Alete Amani ya Kudumu kwa Taifa letu.
Wako mzalendo,
Mteule G. Kahangile
Mwananchi
Fuatilia kituo cha KILINGENI kwenye WhatsApp: KILINGENI | WhatsApp Channel