Barua za maombi ya kazi kuchanwa maofisini

BM-40 OPERATOR

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
153
Reaction score
55
Habari zenu ndugu watanzania wenzangu. Katika hali isiyo ya kawaida, jana nilipokuwa ofisini kwangu mida ya saa tano na nusu asubuhi alikuja dada mmoja ambaye ni graduate, alikuwa anaonekana amechoka na kweli anashida ya kazi. Alitela barua yake ya maombi ya kazi then akaikabidhi kwa ofisi ya human resources ambayo tumetenganishwa na partition za vioo, hivyo mnaweza kuona kinachoendelea ofisi nyingine. Baada ya yule dada kukabidhi ile barua kwa HR na kuondoka, barua ile ilichanwa muda ule ule bila wao kufahamu kama nilikuwa ninawaona. Na inasemekana nafasi ile ya assistant accountant tayari mtoto wa dada yake huyu HR manager wetu hapa ofisini tayari ameshachukuliwa. Poleni sana graduates mnaohangaika kutafuta kazi, haya ndio yanayowakuta ambayo mlikuwa hamyafahamu!
 
Duh! Tutatoboa kweli kwa mtindo huu
 
kama kuna uwezekano wa kujiajiri inakuwa bora zaidi kuliko kutafuta vibarua ofisini kwa watu
 
huo ni unafiki km kweli ulichukizwa ili bidi uchukue maamuzi instantly na si kuja humu na kutuletea udaku
 

very bad....anyway_time will tell
 
huo ni unafiki km kweli ulichukizwa ili bidi uchukue maamuzi instantly na si kuja humu na kutuletea udaku

hajafanya unafiki mkuu..angalau katufumbua macho watu wengine kwa uozo huu wa ma..hr wetu
 


daah,,aisee
sio vizuri lakini
and god is watching,,,
 
musa chizi sio mpaka atembee uchi ulchoandika pia ni uchizi. jamaa katueleza alichoona unataka afanye nini kingine. mijitu mingine imengia ktk JF labda kwa sababu rafiki yake nae yupo humu nae anafuata mkumbo.
 
Hayo mambo yana mwisho wake. Atachana barua za watu za maombi ya kazi lakini ipo siku na yeye atachanwa kwa satyle yake ya utendaji kazi. FISADI MKUBWA NA KWELI HII VITA DHIDI YA MAFISADI INAELEKEA KUZIDI KUWA NGUMU COZ KAMA TUNA MA HR WA AINA HII TUTAFIKA WAPI?
 
duh pole sana kwa yeye but we should always soma wenyewe ili tuweze kujiajili jaman tatizo kila mtu anataka kuajiliwa.

if you real need to success you should enc our risk
 
Huyo aliamua kuchana, ila wale wa siku hizi waliowengi wanatoa mojawapo ya document muhimu katika application yako ili uonekane umesubmitt incomplete application docs. Ni mchezo wa masecretary lakini leo naambiwa Hr mwenyewe anafanya.. very bad.

Mwambie mtu hamna kazi ili akatumie docs zake kuombea mahari pengine. Stationery ni gharama kwa mtu asiye na kazi!!! Huruma jamani
 
asante kwa kutujuza yanayotokea ofisinii kwenu...Ingawa mgeni Jamvini siku nyingine ukiingia piga hodi
 
Duh!Aisee,inauma saana.Kwa mfano huyo Hr wenu nae ni member humu jamvini,na ktk fukua fukua zake akafanikiwa ku uona huo uzi uliou post huoni kua utakua umekiotesha nyasi kibarua chako?Cause,obvious atajua ni wewe.
 
ipo siku Mungu atachana mifile yao mbinguni na kuprove we all at the same level.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…