BM-40 OPERATOR
Senior Member
- Oct 13, 2012
- 153
- 55
Habari zenu ndugu watanzania wenzangu. Katika hali isiyo ya kawaida, jana nilipokuwa ofisini kwangu mida ya saa tano na nusu asubuhi alikuja dada mmoja ambaye ni graduate, alikuwa anaonekana amechoka na kweli anashida ya kazi. Alitela barua yake ya maombi ya kazi then akaikabidhi kwa ofisi ya human resources ambayo tumetenganishwa na partition za vioo, hivyo mnaweza kuona kinachoendelea ofisi nyingine. Baada ya yule dada kukabidhi ile barua kwa HR na kuondoka, barua ile ilichanwa muda ule ule bila wao kufahamu kama nilikuwa ninawaona. Na inasemekana nafasi ile ya assistant accountant tayari mtoto wa dada yake huyu HR manager wetu hapa ofisini tayari ameshachukuliwa. Poleni sana graduates mnaohangaika kutafuta kazi, haya ndio yanayowakuta ambayo mlikuwa hamyafahamu!