Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Miaka ya hivi karibuni Baraza la Sanaa la Tanzania limekosa kazi ya kufanya isipokuwa kusubiri wasanii watoe nyimbo ndo likae vikao kuzifungia.
Hata Rais Magufuli amewahi kutishia kulifuta Baraza hili kwa sababu aliona halina kitu chochote cha maana kinalofanya isipokuwa tu kugeuka na kuwa chombo cha kisiasa, nyapala wa kuzuia wasanii kutoa nyimbo ambazo zinakera watawala.
Baraza hili limeshindwa kuzuia miziki na sinema zenye kuhamasisha ngono lakini liko mbiombio kutisha na kusumbua wasanii wenye mrengo wa kuzungumzia mambo makubwa ya nchi.
Nataka niikumbushe BASATA kuwa ibara ya 8 ya Katiba ya nchi inatoa Uhuru wa maoni na haijazuia mtu yeyote kutumia sanaa kutoa Maoni yake.
Kwa hiyo nalitaka Baraza liache kumsumbua na Kumsakama kijana Ney wa Mitego kwa kutoa maoni yake juu ya nchi inavyokwenda.
Si kazi ya Baraza kukataza wasanii wasiongee kuwa nchi inakwenda pabaya, au tunaongozwa vibaya.
Baraza liache kufanya kazi ya watawala na badala yake lijikite katika kukuza na kuendeleza sanaa nchini.