BASATA lamfuta usajili “Dudubaya”

BASATA lamfuta usajili “Dudubaya”

Hziyech22

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
15,351
Reaction score
21,362
Baraza la Sanaa Tanzania lamfutia usajili msanii Godfrey Tumaini maarufu Kama "Dudu baya" kwa kosa la kutumia mtandao wake wa Instagram kuwatukana wadau wa mziki.

Hivi karibuni msanii huyo alitumia maneno mabaya na kauli chafu kumtupia Mkurugenzi Mkuu wa Benchmark "Madam Rita" kwenye sakata lake la BSS anapodaiwa kutomlipa mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2019 kiasi cha milioni 50 alizoahidiwa.

Hii inakuwa Mara ya pili kwa msanii huyo kufutiwa usajili wake na BASATA baada ya hapo awali kusamehewa.
 
hawa basata wanayumba tu, mbona akina diva, mwijaku na lokole wanatukana watu daily hawajafutiwa leseni za kazi?? huyu bwana anaonewa inshort
Ukitaka kufuata utaratibu, anaetukanwa alipaswa kwenda kushtaki na siyo kuibuka vigenge vya watu na kujifanya wao ndio kila kitu.
 
Tanzania kuna miungu watu.

Huku Basata Wana Total Authority Kwa Msanii.

Huku TCRA wana full authority kwa Media.

Sasa Mahakamani za Nini ?

Zifutwe tu.
Kwa maana yako we popoma mahakama ni za kuendesha kesi za wasanii na media pekee.
Acha ujinga popoma we.
 
Dudubaya Wanachi washamkataa , amebakiza kuwa kichekesho mtu kama Dudubaya mwenye miaka 50 anashindwa kuacha bangi na pombe akawa kama Prof Jay au AY / yeye anaona labda kuwa anapata attention kumbe ndo tiyar ameshakuwa kichekesho .
 
hawa basata wanayumba tu, mbona akina diva, mwijaku na lokole wanatukana watu daily hawajafutiwa leseni za kazi?? huyu bwana anaonewa inshort
Jamaa hawajamuonea sio kwa matusi yale!! Nilimshangaa sana mshikaji nadhani ana tatizo la akili. Binadamu mwenye hekima na busara huwezi tukana vile!!
Mbona akina Prof Jizo na akina AY wana busara na hekim.Jamaa anajiendekeza kuna kazi nying mziki umemshinda na majira yamebadilika
 
Wame chelewa sana kumfungia maana hata mziki wenyewe umesha mshinda
 
Lakini basata ndo inayoangalia maadili ya wasanii,dudubaya alivuka sana mipaka na pia zile pombe ni stress kwamba kwenye mziki pamoja na kupambana amefeli,mengine anayopambana kwenye harakati zake ni za kweli na mengi ni kuchafua watu na njia anazotumia kuwasilisha kwa watu ndo anapokosea.TCRA bado ina uwezo wa kumshitaki.

Hivi kwa matusi kama yale bado unaona basata wamekosea?
Kutukana K za mama za watu ni kukosa heshima na kusamehewa na basata ameshasamehewa sana
Tanzania kuna miungu watu.

Huku Basata Wana Total Authority Kwa Msanii.

Huku TCRA wana full authority kwa Media.

Sasa Mahakamani za Nini ?

Zifutwe tu.

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Wale hawatumii lugha chafu ,dudubaya anatumia lugha chafu sana
hawa basata wanayumba tu, mbona akina diva, mwijaku na lokole wanatukana watu daily hawajafutiwa leseni za kazi?? huyu bwana anaonewa inshort

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Wasafi wenyewe sometimes anawatusi,alisema walimwekea sumu kwenye wasafi festival,hivi watu wakupe shavu halafu wamwekee sumu tena?
Wasafi waliishia wapi na huyu mzee

♡♤Life belongs to all who struggle for it♤♡♧
 
Back
Top Bottom