Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Hawa viongozi wa Bar-Sata ni wa kukemewa na kila mtanzania mwenye akili timamu. Wamefungia wimbo wa Ney wa mitego kwa sababu ameimba "wanaokuja kututeka wanakuja kama Polisi" yaani kwa utashi wao wanadai na wanasema ni maneno yenye uchochezi.
Lakini upande wa Polisi wenyewe wanakiri wazi kwamba baadhi ya watekaji hujitambulisha kama Polisi. Yani ni ajabu kuona namna Dkt Mapana na wenzake wa Bar-Sata wakiwa wameumizwa sana Polisi kutajwa kuliko polisi wenyewe, ni ajabu sana, kali ya mwaka!
Dkt. Mapana nina imani kuwa juzi kati kwenye kongamano la TLS Afande Muliro alikiri kwamba baadhi ya Watekaji ni wahalifu ambao hujitambulisha kama Polisi, yaani ni wahalifu wanaotembelea kivuli cha utambulisho wa polisi, ili wapate kufanikisha uhalifu wao.
Lakini Bar-Sata wanakataa kuwa hawa watekaji sio polisi kama ambavyo Afande Muliro alivyodai. Yaani tumepata kuona mambo ya ajabu sana Bar- Sata wanawakatalia hata hao Polisi wenyewe, wanapinga kauli za chombo cha polisi.
Ukisikia kiwango cha juu cha kujipendekeza, unafiki na uchawa basi ndio hiki. BAR-SATA mmefeli sana ama mfanye kubadilisha malengo yenu mkachukue nafasi ya polisi sasa.
Kitu ambacho Bar-Sata hawawezi kuelewa ni kuwa ukienda kwenye baadhi ya familia za wahanga wa utekaji huu unaoendelea, watakuambia waliowateka ndugu zao walijitambulusha kama maafisa wa Polisi. Kwa ufupi ni kwamba waliowateka akina Soka, Robert Mushi, mzee Kibao na wengine walijitambulusha kuwa wao ni Polisi.
Sasa Bar-Sata tatizo lenu nini? Mnataka watu waendelee kutekwa na hao wanaojiita Polisi? Au unataka wajitambulishe kama majambazi ili Ney akitoa nyimbo iwe nzuri kusikiliza katika masikio yenu.
Lazima muelewe jambo moja kwamba si kila anayejiita Polisi ni Polisi kweli hivyo haina maana kwamba ni lazma uongozane naye. Wengine ni wahuni na wahalifu wanaovaa identity za uongo kama polisi kama alivyosema Kamanda Muliro.
Kwahiyo uwepo wa wimbo wa Ney utawasaidia Polisi wajue kuna wahuni na wahalifu wanaotumia title zao kuteka watu, lakini pia unawasaidia wananchi wasikubali kuongozana na watu wanaojiita Polisi bila kujiridhisha kuwa ni maafisa wa polisi.
Dkt. Mapana nina imani kuwa juzi kati kwenye kongamano la TLS Afande Muliro alikiri kwamba baadhi ya Watekaji ni wahalifu ambao hujitambulisha kama Polisi, yaani ni wahalifu wanaotembelea kivuli cha utambulisho wa polisi, ili wapate kufanikisha uhalifu wao.
Ukisikia kiwango cha juu cha kujipendekeza, unafiki na uchawa basi ndio hiki. BAR-SATA mmefeli sana ama mfanye kubadilisha malengo yenu mkachukue nafasi ya polisi sasa.
Kitu ambacho Bar-Sata hawawezi kuelewa ni kuwa ukienda kwenye baadhi ya familia za wahanga wa utekaji huu unaoendelea, watakuambia waliowateka ndugu zao walijitambulusha kama maafisa wa Polisi. Kwa ufupi ni kwamba waliowateka akina Soka, Robert Mushi, mzee Kibao na wengine walijitambulusha kuwa wao ni Polisi.
Sasa Bar-Sata tatizo lenu nini? Mnataka watu waendelee kutekwa na hao wanaojiita Polisi? Au unataka wajitambulishe kama majambazi ili Ney akitoa nyimbo iwe nzuri kusikiliza katika masikio yenu.
Lazima muelewe jambo moja kwamba si kila anayejiita Polisi ni Polisi kweli hivyo haina maana kwamba ni lazma uongozane naye. Wengine ni wahuni na wahalifu wanaovaa identity za uongo kama polisi kama alivyosema Kamanda Muliro.
Kwahiyo uwepo wa wimbo wa Ney utawasaidia Polisi wajue kuna wahuni na wahalifu wanaotumia title zao kuteka watu, lakini pia unawasaidia wananchi wasikubali kuongozana na watu wanaojiita Polisi bila kujiridhisha kuwa ni maafisa wa polisi.
Sasa wimbo kama huu badala ya kuubariki huu wimbo nyie mnaufungia? Akili za ajabu kweli. Siku wakitekwa watoto wenu ndio mtajua umuhimu wa wimbo huu, siku mke au mume wako akichukuliwa na hawa wahalifu na kupotea, mtajua kuwa maamuzi yenu sio ya busara kabsa! Na ajabu ni kuwa kwa jamii yetu ya Watanzania baada ya kuufungia huu wimbo ndo mmeupigia promo zaidi. Hapo tunasema ni GG! Hongereni, mnaendelea kuharibu tu utendaji kazi wenu! Shame on you.