Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,745
Ndugu wanajamvi kumeibuka mjadala mkali sana nchini Tanzania kuhusiana na sakata la kufungiwa kwa nyimbo za wasanii mbalimbali sababu kubwa ikiwa ni utovu wa maadili na utamaduni .Swala la maadili na utamaduni wa jamii ya kitanzania kama taifa ni swala ambalo huwa linaibua mjadala mzito sana mara zote linapoibuliwa.
Maswali kama utamaduni wetu ni upi? Maadili ya mwafrika hususani mtanzania ni yepi? Nk hayo ni baadhi ya maswali yanayoshughulisha akili za walio wengi, kiufupi maadili na utamaduni ni maswala ambayo yapo wazi kwa mjadala wa taifa.
Je utamaduni wa mtanzania ni kuvaa nguo kufunika mwili mzima au ni kuacha viungo vyake wazi?
Je utamaduni unabadilika au utamaduni ni uleule wa miaka ile ya kale mpaka sasa? Nakumbuka enzi zile naoma tulikuwa tunaambiwa culture is dynamic, how and to what extent.
Je huu tunaouita mmomonyoko wa maadili siyo sehemu ya utamaduni wetu kukua na kubadilika (dynamism)
Yafuatayo ni maoni aliyopata kuyatoa Profesa Tibaijuka kuhusiana na mavazi na maadili ya mwanamke wa kitanzania;
MAONI YA PROFESA TIBAIJUKA KUHUSU MAVAZI
"Ukiona watu wanahangaika na suala la mavazi hasa kukazania yale yanayoficha mwili wa mwanamke ujue wana matatizo yao wamelishwa kasumba ya wageni.
Dhana ya kuficha mwili ni kweli haina Uafrika wowote ndani yake. Mwafrika katika asili yake haangaiki kuficha mwili wa mwanamke. Hauoni kama chombo cha kumfurahisha mwanaume bali kiungo muhimu kumruhusu mwanamke kutimiza wajibu wake. Kwa mfano wakati mwanamke wa kizungu anahangaika kujificha kunyonyesha mtoto Mwafrika asili anatoa ziwa mtoto ananyonya hadharani. Hapa titi ni mali ya mtoto siyo ya mume!
Kwa hiyo kabla ya wakoloni kufika na wamisionari walioandamana nao wakiwa wamevaa nguo ndefu watoto walikuwa uchi wasichana walipewa ngozi kujisitiri sehemu za siri wakivunja ungo na wanawake nao yalikuwa hayo hayo. Kulikuwa hakuna ubakaji kwa sababu hiyo.
Ni kweli utasema jamii ilikuwa haijaendelea na maskini. Unaweza pia kusema hali ya maendeleo ilikuwa duni.Nguo hakuna.
Lakini hoja hapa ninayolenga kupangua ni ile kwamba wanawake wakijifunua kwa kuonyesha uso au mikono au matiti au miguu yao au mapaja wanawakwaza wanaume. Sio kweli. Mbona mababu zetu hawakukwazika hizo enzi nilizoelezea? Mbona hawakubaka watoto na wasichana kama ilivyo sasa?
Dhana kwamba mwili wa mwanamke ni chombo cha anasa kwa mwanaume zimepandikizwa katika jamii ya Kiafrika na ziko katika fikra. Kuwafunika wanawake kwa mavazi marefu na shungi hakuondoi tamaa na mawazo ya anasa juu yao kwa wenye nia hiyo. On the contrary kunachochea jambo hili.Wanaume wanabaki kufikiri huyu sasa huko ndani yukoje? Hii inaweza kuchochea mashambulizi ya ubakaji kuliko kusaidia kuyaepusha.
Angalia Ulaya ambapo hakuna anayehangaika na kuthibiti mavazi. Hata uvae mini skirt ya namna gani hakuna anayejali. RUKSA. Wasichana wanavaa kaptula no problem. Jamii imejikomboa kimawazo na kifikra. Wanajua jinsi mwili na maumbile ya mwanamke yalivyo.
Kwa hiyo kama hupendi kuwanyanyapaa wanawake huwezi kuwalazimisha au kuwapangia mavazi na muonekano. Wacha waamue wenyewe wanavyotaka kwa sababu zao. Wengine utamaduni na dini wengine siasa (kutafuta kukubalika) wengine sheria za kazi au shughuli yao na waliowengi kutaka kupendeza tu. Let the women be free in deciding for themselves what to wear. Trust their judgement."
Nawasilisha
Zifuatazo ni baadhi ya picha za wacheza ngoma za asili pamoja na jamii za kiafrika zinazoshikilia utamaduni wa mwafrika;
Hapa chini ni picha ambazo zinaonekana hazina maadili za mwanamke wa kisasa
NINI MAONI YAKO? UPI NI UTAMADUNI NA MAADILI HALISI YA ASILI YA MTANZANIA YANAYOTAKIWA KULINDWA NA SERIKALI?
UPDATES
Maoni ya Msukuma bungeni April 27, 2018