Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Baada ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) kukifungia kituo cha televisheni cha Wasafi kwa kurusha maudhui ya utupu yanayomuonyesha msanii Gift Stanford Jushua maarufu kama Gigy Money, nalo baraza la sanaa Tanzania(BASATA) limeibuka na kumlamba adhabu ya miezi sita msanii huyo kutojihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi.
Pia BASATA imemtaka msanii huyo kulipa faini ya milioni 1. Sehemu ya taarifa yake imesema Gigy alishaitwa na baraza na kuonywa mara kadhaa na aliahidi kutorudia tena.
PIA, SOMA => RUNGU: TCRA imeitaka Wasafi TV kusitisha matangazo kwa Miezi Sita (6) kuanzia leo kwa kurusha Maudhui ya utupu