Tumbo Tumbo
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 1,278
- 1,553
Sitaki Kusema kuwa Sanaa imeingiliwa na wahuni, Inawezekana kuwa walikuwa wahuni kabla hata ya kuanza sanaa Sema hatukutupia jicho kabla lakini pia usisahau kuwa huu Muziki wa hawa vijana uliitwa Muziki wa Kihuni hapo kabla na ni wao wameufanya mpaka sasa uonekane ni Muziki na watu wakaanza kuwekeza hapo.
Hakuna njia sahihi ya kuwasaidia hawa vijana zaidi ya kuwa chanya kwao, kutoa uhasi wao dhidi ya Basata na kuwasaidia katika changamoto zinazowakabili.
Kusema vijana wana viburi, vijana tuliowakuza wenyewe, wamekuwa ndani ya jamii yetu, wanatuwakilisha sisi, wanawakilisha tabia zetu katika mazingira yao.
Ni kama pale Machinga Complex, Serikali ilikuwa na wazo nadhifu kuwasaidia vijana wetu ambao ni wafanyabiashara wadogo, waache kuzunguka na wafanye biashara katika ofisi,wengi wao wamepakimbia, sio kwamba ni viburi, la hasha, mazingira yao, uzoefu wao, makuzi yao, Elimu yao na mitaji yao vikawafanya washindwe kukaa pale ila muda utafika na watalielewa lile wazo zuri la Serikali.
Unapokuwa kiongozi, tambua unayemuongoza yukoje, msikilize, muelewe, msaidie na muongoze.
Narudia, Basata wanapaswa kuwepo humu watusaidie, watupe uhalali wa vifungo vyao, uwezo wao wa kushtaki na kuhukumu wao kama wao, usimamizi wao katika sanaa, tafsiri sahihi za sanaa, mazingira ya sanaa, kama kuna tahadhari ya sanaa kwa hadhira yetu nk.
Changamoto/Mgogoro huu ni Mzuri sana katika ukuaji na utambuzi wa sanaa hii, naamini kuwa siku ya mwisho mrejesho utakuwa mzuri, haina haja ya kuhukumiana kisa mtu katoa hoja usiyoiafiki, siku ya mwisho tunajenga nyumba moja! Tujitathmini, hakuna mtu anayependa kuharibu kazi yake inayompa heshima na ujira, kuna changamoto zinamkabili ambazo "reaction" yake inatofautiana na mawazo ya kila mmoja wetu.
Tubadilishane Viatu ili tuelewe zaidi.
Wasalaam.