kina kirefu
JF-Expert Member
- Dec 14, 2018
- 15,188
- 18,583
Hilo shart itakua kutunga nyimbo zakuhamasisha kuichagua ccm 2020.tue makini na hizi sarakasi wasafi vs baraxa
Kwa mujibu wa Diamond wakati anaongea na vyombo vya habari nchini Kenya amesema BASATA wamewaruhusu kuendelea na show kwa masharti.
Diamond amesema mara baada ya kupigwa pini ambapo ilikua ni halali kabisa kwa kosa walilolitenda,walichukua hatua ya kuwaandikia barua Baraza hilo la.sanaa kuomba wawasamehe na kuwaruhusu kuendelea na show nyingine jambo ambalo walikubaliwa na kupewa sharti ambalo hakulisema wazi japo aliligusia kwamba wakirudi nyumbani watatakiwa kuteleza.
Mapema leo Wasanii hao ambao wako jijini Nairobi kwa ajili ya show yao ya wasafi festival jijini Mombasa na Nairobi,walionekana kwenye video fupi wakiomba radhi kwa serikali na watanzania kwa ujumla kufuatia kuperform wimbo wa Mwanza uliofungiwa na mamlaka hiyo ya maswala ya Sanaa nchini.
Hata hivyo serikali kupitia BASATA hawajaweka wazi jambo hili la kuwafungulia wasanii hao.
View attachment 973980