BASATA yalaani vitendo alivyofanyiwa msanii Zuchu jukwaani

Nilitaka kusema sio sawa. Lakini baada ya kusikia alileta siasa kwenye tamasha la muziki. Kama mtu asiyependa siasa uchwara nasupport hicho kitendo.

Hawa wasanii hawajui machungu wanayopitia wananchi. Miaka 60 ya uhuru nchi bado haina chanzo imara cha maji.
 
Ko Dole la Kati hawajaliona au Mi5 tena kwa Mama Abdul imefuta dhambi za Zuchu zote?
 
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelaani vikali kitendo alichofanyiwa Mwimbaji wa Bongo Flava, Zuhura Othman Soud cha Mashabiki kumtupia vitu jukwani katika Tamasha la Wasafi Festival lililofanyika Septemba 28, 2024 Mkoani Mbeya.

Katika taarifa yake kwa Umma, BASATA imetoa rai kwa Wadau wa Sanaa na Wasanii kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyokua na tija na kuwataka pia Waandaaji wa matukio ya Muziki kuzingatia mazingira salama kwa Wasanii na Wadau wake katika matamasha ya Muziki.

“Baraza la Sanaa la Taifa linalaani tukio lililovuruga utumbuizaji kwa Mwanamuziki Zuhura Othman Soud (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na Mashabiki” - imeeleza taarifa ya BASATA.

Pia, soma: Wasafi Festival Mbeya hali imekuwa tete, Zuchu akimbia jukwaa
Je mbona hawaja laani ZUCHU kuchomekea siasa jukwaani au mambo ya P Didy?
 
Attachments

  • Putin.jpg
    Putin.jpg
    3.4 KB · Views: 3
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limelaani vikali kitendo alichofanyiwa Mwimbaji wa Bongo Flava, Zuhura Othman Soud cha Mashabiki kumtupia vitu jukwani katika Tamasha la Wasafi Festival lililofanyika Septemba 28, 2024 Mkoani Mbeya.

Katika taarifa yake kwa Umma, BASATA imetoa rai kwa Wadau wa Sanaa na Wasanii kuheshimu misingi ya kiungwana ili kuepusha migongano isiyokua na tija na kuwataka pia Waandaaji wa matukio ya Muziki kuzingatia mazingira salama kwa Wasanii na Wadau wake katika matamasha ya Muziki.

“Baraza la Sanaa la Taifa linalaani tukio lililovuruga utumbuizaji kwa Mwanamuziki Zuhura Othman Soud (Zuchu) baada ya kutupiwa vitu jukwaani na Mashabiki” - imeeleza taarifa ya BASATA.

Pia, soma: Wasafi Festival Mbeya hali imekuwa tete, Zuchu akimbia jukwaa
Ila alivyoleta siasa kwenye burudani waliona sawa
 
Msanii alishindwa kufanya kazi yake Kwa kuzingatia muktadha ,kapata fundisho na wasanii wengine wajifunze kupitia kilochotokea mbeya
 
BASATA haijitambui. Msanii ndiye anapaswa kuchukuiwa hatua haraka. Walichofanya BASATA hakina weledi ndani yake bali ni maaamuzi ya kukurupuka na kutafuta kujipendekeza kwa wateule wao, bora wangekaa kimia.
BASATA wafundeni wasanii wenu, wakiendekeza huu ujinga maeneo kama ARUSHA, MARA NA MBEYA ambako raia hawapendi uongo na kujipendekeza mtakuja kuzika msanii kwa ujinga huu.
 
Back
Top Bottom