Basata Yampiga Stop Steve Nyerere

Basata Yampiga Stop Steve Nyerere

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Baraza la Sanaa (BASATA) limesema kuwa Msemaji wa Shirikisho hilo aliyeteuliwa, Steven Mengere asianze kutekeleza majukumu yake hadi hapo itakapoamuliwa na Baraza hilo.

BARUA YA BASATA KWA KATIBU MKUU (FID - Q) WA SHIKISHO LA MUZIKI

Tafadhali rejea somo tajwa hapo juu. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kwa mujibu wa Vifungu 4(1), (i) na (p) na 4A vya Sheria (Sura 204) vikisomwa kwa pamoja na Kanuni ya 19 ya Kanuni za Baraza (G.N 43/2018), limepewa mamlaka ya kusajili na kusuluhisha migogoro ya wasajiliwa wake yakiwemo mashirikisho ya Sanaa nchini.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni kuliibuka mgogoro katika Shirikisho la Muziki Tanzania uliohusisha uteuzi wa msemaji wa Shirikisho hilo Bw. Steven Mengere (Steve Nyerere). Kutokana na mgogoro huo, Baraza liliitisha kikao mnamo tarehe 23 Machi, 2022 kilichofanyika katika ofisi za Baraza. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kupata kiini cha mgogoro huo ili kutafuta ufumbuzi kwa mujibu wa Sheria na Katiba ya Shirikisho.

Aidha; viongozi wa Shirikisho walieleza kuwa uteuzi wa Bw. Steven Mengere, ulifanyika tarehe 1 Machi, 2022 ambapo viongozi wa Shirikisho ambao ndio Bodi ya Utendaji, walikaa kikao na kufanya uteuzi huo kwa mujibu wa Kipengele cha 6.2.8 (a) cha Katiba ya Shirikisho

Kutokana na maelezo tajwa hapo juu, Baraza limejiridhisha kuwa Bodi ya utendaji ya Shirikisho ilifanya kikao chake mnamo tarehe tajwa katika ukumbi wa Bodi ya Filamu na kufanya uteuzi huo.

Hivyo Baraza linaendelea kufanyia kazi taarifa zilizowasilishwa na viongozi wa Shirikisho pamoja na kufanyia kazi hoja za wajumbe waliohudhuria kikao hicho na litatoa uamuzi wake mapema iwezekanavyo.

Kuhusu msemaji wa Shirikisho aliyeteuliwa (BW. Steven Mengere), Baraza linatoa maelekezo asianze kutekeleza majukumu ya nafasi hiyo hadi hapo itakapoamuliwa na Baraza.

Nakutakia kazi njema.
 
Vema sana.

Tivu ake amepigwa stop na Basata,,Basata ni pua,,,pua,,,pua tena pua kabisa.
 
ipe maneno

1648064399739.png
 
Ile press ya juzi imempunguzia credibility, hata kwa waliodhani kuwa anatosha kwenye ile nafasi.
 
"Ommy hatoimba tena"
"Ommy hatoimba tena"
"Tatizo vocal'

Steve nyerere 8:7_10
 
Back
Top Bottom