Mimi ninachojiuliza ni hivi mtu yeyote huko duniani akitunga wimbo wenye 'maudhui' yaliyo tofauti na Tanzania hairuhusiwi kuusikiliza hapa!? Tuchukulie uko katika lugha tofauti na kama tunavyojua wanamuziki ni wengi duniani na kila mmoja anatoa wimbo wake. Sasa Ney wa Mitego sijui akienda akarekodi wimbo tuseme Amerika, Ulaya, Asia nk wakaupenda alafu TZ na basata yetu tukaupinga, hao basata wataenda huko duniani kuwaambia wamiliki wa tv, maredio na mitandao kuwa "huo wimbo mnaupenda lakini sisi TZ tumeupiga marufuku na nyie hamruhusiwi kuusikiliza"!