Mtumishiwetu
Senior Member
- Jul 13, 2022
- 196
- 346
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa mara ya kwanza amejitokeza hadharani kuomba msaada wa mawazo na ushauri wa namna ya kuendesha Wizara ya Kilimo.
"Ukiwa na muda tafadhali nipe mawazo yako kuhusu Kilimo na usalama wa Chakula kwa nchi za Afrika haswa hapa nyumbani kwetu Tanzania Nini kifanyike? Nini kiboreshwe?" amesema Bashe
Maswali ya kujiuliza Bunge la Bajeti limemalizika mwezi Juni. je mambo yote yaliyoshauriwa na wabunge kuhusu Kilimo ameshayamaliza kuyafanyia kazi.?
Je anamuonesha Mhe. Rais kuwa alimteua mtu ambaye hajui cha kufanya Wizara ya Kilimo hadi aanze kuokoteza mawazo kwenye mitandao? na je anaamini wakulima wako Instagramu?
Au ndio ile kauli ya mfa maji haishi kutapata baada ya usimamizi mbovu wa wizara na kusababisha nchi kukumbwa na baa la njaa kutokana na usimamizi mbovu kuruhusu wananchi wa mataifa mengine kuingia vijijini mashambani na kununua mazao moja kwa moja hadi Japan kuamua kuingia kati kusaidia Tanzania fedha kwa ajili ya ununuzi wa chakula?
Mimi nadhani ni muda sasa kwa Waziri Bashe kujiuzulu ili kumpa nafasi Mheshimiwa Rais kutafuta mtu mwingine atakayeweza kusimamia sekta ya kilimo na tuondokane na baa la njaa alilolisababisha Bashe