Bashe aeleza mafanikio kupitia uanzishwaji wa vituo vipya vya umahiri kwenye kilimo

Bashe aeleza mafanikio kupitia uanzishwaji wa vituo vipya vya umahiri kwenye kilimo

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Arusha, Tanzania.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ameeleza mafanikio yatakayopatikana kutokana na kufunguliwa Kwa vituo vipya vitano vya umahiri kwenye mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambavyo vimefadhiliwa na shirika la Maendeleo la Umoja wa mataifa yaani UNDP.

Naibu Waziri Bashe anasema “Tumezindua vituo vya umahiri vitano (Centre of excellency) katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambavyo vimefadhiliwa na UNDP na kusimamiwa na TAHA.”

Mradi huu ni mmojawapo ambao unawekezwa katika sekta ndogo ya kilimo cha mbogamboga na matunda (Horticulture). Kituo hiki cha ‘Tengeru Horticulture Centre of excellency’ kitakua na Maabara, Cold facilities (vifaa vya ubaridi), vitalu vya miche kwa ajili ya wakulima, kituo cha mafunzo, sehemu ya kuhifadhi na kufungasha mazao ambapo wakulima na wafanya Biashara watatumia kuandaa mazao yao.

Pia hiki kituo kina hati zote za kimataifa Kwa maana ile ya “Global Gap certification” na “BRC ithibati” maana yake ni zao linalotoka hapa linaweza kuuzwa kwenye soko lolote duniani.

Nimejadiliana na muwakilishi wa nchi (Country Representative) wa UNDP Ms. Christine Musisi ili tuweze kuanzisha ‘Common user facility’ nyanda za juu kusini katika mikoa ya Iringa na Njombe ili itumike kuhifadhi, kufungasha na kuweka lebo ya mazao yetu yanayonunuliwa na wanunuzi wa nchi za Kenya ili kuonyesha mahala bidhaa imetoka yaani country of origin haswa zao la parachichi. Hivyo, Kituo hicho kitakua ni cha kutoa huduma zote muhimu Kwa wanunuzi wanaopeleka mazao nje ya nchi.

Nawashukuru sana UNDP na TAHA kwakukubali kuwekeza zaidi kwenye ujenzi wa miundombinu badala ya miradi ya uwezeshaji (capacity building) ambazo zimekuwepo kwenye kilimo kwa miaka mingi

Mheshimiwa Bashe ameendelea kuwasihi wadau wa Kilimo pamoja na marafiki wa Maendeleo kuendelea kushirikiana na Wizara ya kilimo kwenye ujenzi wa miundombinu wezeshi badala ya kuwekeza fedha kwenye semina nyingi huku akitaja maeneo yenye uhitaji kama;

i) Kujenga mifumo ya uhifadhi na ya umwagiliaji
ii) Miundombinu ya uchakataji
iii) Miundombinu ya ufungishaji
iv) Miundombinu ya masoko ya miji na mipakani

Bashe anamalizia Kwa kusema kuwa “Hata hivyo, tumekubaliana mwezi November kukutana pamoja kujadiliana juu ya jambo hili Kwa zaidi huku lengo letu likiwa ni kuhakikisha kilimo kinamkomboa mkulima na kukuza pato la taifa.”
 
Back
Top Bottom