KWELI Bashe alichapisha ujumbe kuwa Utumike utaratibu Sahihi na Sio utekaji

KWELI Bashe alichapisha ujumbe kuwa Utumike utaratibu Sahihi na Sio utekaji

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kumekuwa Na Picha Ambayo Inasambaa Kwenye Mitandao wa Kijamii Wa Facebook Ukichapishwa Na Baadhi Ya Account za watumiaji zikionesha Chapisho La Hussein Bashe
" Sote Tusimame Tuseme hapana Kwa Mfumo huu unaoanza Kutoa Mzizi kama Mtu Ana Kosa Makosa Ufuatwe utaratibu Wa kisheria kumkamata sio utekaji."
Tunaomba uhakiki Wa Taarifa hii

1759846953898.jpg

​
 
Tunachokijua
Hussein Bashe ni mwanasiasa na kada wa chama cha mapinduzi (CCM), mbunge aliyemaliza muda wake kupitia jimbo la Nzega na waziri wa kilimo.

Madai
Kumekuwapo na 'screenshot' inayosambaa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikionekana kuwa ni kutoka katika ukurasa wa wa aliyekuwa mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akieleza kuwa utaraatibu sahihi utumike kwa watu wenye makosa na siyo utekaji.

Uhalisia wa 'Screenshot' hiyo

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhsisha kuwa ni kweli ujumbe huo ulichapishwa na kiongozi huyo.

Utafutaji kwa kutumia maneno muhimu kupitia ukurasa rasmi wa X wa Bashe unaonesha kuwa ujumbe huo aliuchapisha April 7, 2017 ambao upo hadi sasa wakati tipoti hii inaandikwa (Oktoba 7, 2025) na umehifadhiwa hapa.

Ujumbe huo wa Saa 3 na dakika 3 asubuhi, Aprili 7, 2017 unasomeka;

"Sote tusimame tuseme hapana kwa mfumo huu unaoanza kuota mizizi Kama mtu Ana makosa ufatwe utaratibu wa kisheria kumkamata sio utekaji." - Hussein Bashe

Itakumbukwa kuwa kipindi hicho Bashe hakuwa Waziri bali mbunge tu, safari yake ya uwaziri ilianza 2019 akiwa kama naibu Waziri wa Kilimo na baadaye kupanda hadi kuwa Waziri wa wizara hiyo.

Aidha mwaka 2017 ni miongoni mwa vipindi ambavyo Tanzania ilishuhudia wimbi la utekwaji nyara kwa baadhi ya watu akiwemo msanii wa HipHop Ibrahim Musa (Roma Mkatoliki)​
Back
Top Bottom