TAARIFA za kuumwa kwa Mheshimiwa Hussein Bashe zimetangazwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lakini hadi sasa haijawekwa wazi anaumwa nini na amelazwa hospitali gani ili watanzania wenye nafasi waweze kumtembelea kama ni hospitali.
Kwanini maradhi ya viongozi inakuwa siri lakini mtu akifa ndio mnakuja kutangaza na kutoa ratiba ya mazishi kumbuka vifo kama vya Dk. Ndugulile, Mafuru, Meja Jenerali Charles Mbuge na wengine tulikuja kutangaziwa msiba na ratiba ya mazishi.
Serikali itoke hadharani ieleze Bashe anaumwa nini na amelazwa hospitali gani kama ni ndani ya nchi au nje ya nchi ili watanzania wajue hali ya kiongozi wao.