Bashe apiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kuingizwa nchini

Bashe apiga marufuku mazao ya kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini kuingizwa nchini

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Tamko la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Biashara
ya Mazao ya Kilimo na nchi za Malawi na Afrika Kusini.

Pia soma: Malawi yazuia unga na mchele kutoka Tanzania, Serikali yaitaka nchi hiyo kufungua masoko, yatishia kuzuia
===

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, ametangaza uamuzi mgumu dhidi ya nchi ya Malawi na Afrika Kusini kwa kuzuia mazao yoyote ya kilimo kuingia nchini kutoka na nchi hizo kukakataa kubadili msimamo wao wa kuruhusu mazao kutoka Tanzania kuingia kwenye nchi zao.

Waziri Bashe ametangaza uamuzi hu leo usiku Aprili 23, 2025, huku akisema msimamo ni kupiga marufuku matunda kama apples na mengine kutoka Afrika Kusini kuingia nchini, hadi watakapoondoa zuio kwa Tanzania.

“Kuanzia usiku huu Aprili 23, 2025, hautaruhusu zao lolote linalotoka Afrika Kusini linalohusiana na kilimo kuingia nchini kwetu,

“Malawi hadi sasa hawajafuta notisi waliyoitoa dhidi ya Tanzania, Natangaza rasmi ni marufuku kwa mazao yoyote ya kilimo kuingia ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia leo. Kwa nchi zote mbili hasa Malawi hatutaruhusu zao lolote kupita nchini kwetu,”amesema.

Aidha, amesema wakati Malawi inawakatalia wafanyabishara wa Tanzania kupita lakini wao (Malawi) kupitia Shirika la Moja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wananunua mahindi kwa hoja ya njaa, kwahiyo mahindi yote waliyonunua kwa ajili ya kutatua tatizo la njaa kwao hayatoenda Malawi, hatutayapeleka na wala hatutaruhusu WFP kuyapeleka hadi watakapofungua soko.

Waziri Bashe amesema Mei 1, 2025 walikuwa wanaanza kuchukua mbolea kutoka Tanzania kwa ajili ya msimu wa kilimo, hatutaruihusu mbolea yoyote kwenda Malawi.

“Hatua hii haihatarishi usalama wan chi wala usalama wa chakula , hakuna mtanzania atakufa kwa kukosa zabibu ya Afrika Kusini, hakuna mtanzania atakufa kwa kukosa Apple kutoka Afrika Kusini, Tunachukua hatua hii kulinda biashara yetu,”amesema Bashe.

Aprili 17, mwaka huu, Waziri Bashe alitoa siku saba kwa nchi za Afrika Kusini na Malawi kuondoa zuio la mazao ya Tanzania, vinginevyo hatua kali zitachukuliwa.
 
14 Aprili 2025

BEI YA MAHINDI TANI MOJA TOKA TANZANIA US$ 318 KWA WASTANI

Viwango vya vei ya Mahindi Tanzania - 14 Apr 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=CkbUg5L4ucM

Je, Tanzania ina akiba kubwa ya mahindi?

Katika Muhtasari wa Kilimo wa eneo la mazuwa makuu, Afrika Mashariki na Kusini mwa afrika wa wiki hii, unaoletwa kwenu kwa fahari kubwa na Collateral Management International na Zimmatic, tunachunguza.

Ripoti hii imewezeshwa na Zimmatic na CMI Promotions, Social Media & Reports:
 
TOKA MAKTABA :

17 Machi 2025

Malawi: Bei za Bidhaa Zinazodhibitiwa

View: https://m.youtube.com/watch?v=Q2xW7csVc1A
- serikali imepanga sheria maalum ya kudhibiti bei za bidhaa. Karibu kwenye Muhtasari wa Kilimo wa Kiafrika wa wiki hii, unaoletwa kwako kwa fahari na Collateral Management International na Mifumo ya Umwagiliaji ya Zimmatic.

Katika kipindi chetu cha leo, Jacques anaangalia kwa karibu soko la mahindi nchini Malawi na pia kutoa maelezo zaidi kuhusu sheria maalum ambayo rais anataka kuitekeleza, hivyo kaa mkao wa kula ili kupata ufahamu wote. Ripoti hii imewezeshwa na Zimmatic na CMI Promotions,
 
Kuna matunda mazuri sana toka south africa tutayapataje? Maana ya kwetu hayana ubora huo na si mengi, nazungumzia ma apple na maembe
 
Back
Top Bottom